Kampuni ya Mabasi ya Abood Bus Service Limited imezindua mabasi ya VIP

Mr Why

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2019
Posts
2,235
Reaction score
4,252
Kampuni ya Mabasi ya Abood Bus Service Limited imezindua mabasi ya VIP yanayofanya safari zake Dar- Mwanza-Dar, kuanzia tarehe 9 Juni 2023.

Hizi basi ni za kisasa na yenye viwango vya juu ikiwemo siti za luxury, air condition, tv, choo cha abiria, wahudumu wa kike, vinywaji na vitafunio.

Route hii imezinduliwa baada ya kupata maombi kwa wateja.
 
Kuhusu tv mbona kuna mabasi yana tv kila siti, kuna mabasi ya kawaida wanagawa mpaka soda na maji. Labda tv hizo zitakuwa zinatumia ving!amuzi unajichagulia chaneli ya kutazama. Kwenye choo hapo sawa. Wangeweka na misosi ya maana na kushiba ndani yake kama kukuz, chapati, maziwa, wali, ndizi, chips, nyama, matunda itapeneza sana
 
Wamekwambia kuna wadada wazuri wahudumu
 
Abood azingatie usafi, mabasi yake mengi ndani ni machafu sana.. gari namba E lakini chafu utadhani namba A
 
Anavamia ligi eeh,, hii ya Katarama na Ally's ni Bundesliga kama atakubali kuwa Schalke 04 mbele ya Bayern Munich na Dortmund sawa,,

Halafu sisi wasukuma tunachotaka ni kuwahi tu kufika mjini hayo mengine yakwenu,,
 
Yutong ni ile ile ikiwa vip au semi luxury ni majina tu ila ukipanda ndani yapo Sawa...
Ingekuwa vip imekuja kwenye Benz, scania au basi tofauti na hapo sawa
Hata dar express alikuwa na benz sikuwahi ona huo uvip zaidi ya kutoka sa2 asubuh na kufika sa2 usiku ndani baridi kali na kupewa maji barafu aiseeee
 
Hii nayo ni habari au Tabgazo la biashara?
 
Hili taifa lina wajinga sana, kwanza mimi kitu sipatani nacho no 1 ni TV kwenye basi, sipatani huo ujinga kabisa, sasa kama karine hii bado unashobokea Tv za kwenye mabasi utakuwa na matatizo
 
Utaharisha ndani ya basi
 
Hata dar express alikuwa na benz sikuwahi ona huo uvip zaidi ya kutoka sa2 asubuh na kufika sa2 usiku ndani baridi kali na kupewa maji barafu aiseeee
UVIO ni kitu gani? Choo? Kwa kifupi hakuba kitu hapo kinacho weza nishawahishi kupanda bus, Choo? Tv sipatani nazo kabisa, Sosa sinywagwi, biscut ni ufala kunipatia biscut
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…