Yaani upumbavu wako na BM wako usababishe wenye mabasi na abiria wanaojitambua na kujiheshimu waache kutoa na kupata huduma bora tulizozoea turudi kukanyagana na wapiga debe wenu Mbezi hizo ni akili au tope?
Nilidhani utamshauri BM aache kufanya kazi na wajinga afanye kazi na wanaojitambua kuinusuru kampuni yake kwasababu siyo mara ya kwanza huduma za BM kulalamikiwa, huko nyuma alikuwa anasema mabasi yana AC, mnapanda bus anawasha AC mpaka Mlandizi au Mikese kama mmetokea Morogoro, anazima mnaambiwa fungueni madirisha mafuta yanakwisha amawaona wasafiri wote wajinga, kwahiyo wewe ndugu huenda ni miongoni mwa wale masalia wachache