Kampuni ya Maziwa ya unga ya Cowbell Matatani

Kampuni ya Maziwa ya unga ya Cowbell Matatani

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
BODI ya maziwa nchini imekamata tani tatu za maziwa ya unga ya 'Cowbell' yaliyokuwa yanakaribia kuishiwa muda wa matumizi yakiwa yameongezwa muda wa matumizi zaidi.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam Kaimu Msajili wa Bodi ya Maziwa Nchini Noel Byamungu amesema walibaini kitendo hicho katika kiwanda cha Kampuni ya Hawai Limited Kilichopo Keko Chang'ombe wakiwa katika majukumu yao ya ukaguzi na usimamizi wa kuhakikisha wananchi wanapata maziwa bora.

Amesema Maziwa hayo yalitakiwa kumaliza muda wake wa matumizi Mwezi June, Agosti na Oktoba mwaka huu lakini kiwanda hicho kilifanya kitendo cha Kufunga upya maziwa hayo katika vifungashio vipya vinavyoonesha mwisho wa matumizi ya maziwa hayo kuendelea kutumika hadi Mwezi Augusti Mwaka 2022.

Amesema watendaji wamewaachia Jeshi la Polisi mkoa wa Kipolisi Temeke ambao ni Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Ahemed Suleiman Mohamed pamoja na Meneja uzalishaji Ahmed Amanzi kujibu tuhuma zinazowakabili.

Kamishina Msaidizi wa Mkoa Kipolisi Temeke Amon Kakwale amesema tayari wanawashikilia watendaji wa Kampuni hiyo.

1610860482423.png
1610860481582.png
1610860429772.png
 
Kwahiyo ndugu yangu wewe hapo ungepokea mlungula, bila kujali maziwa haya yangeumiza watanzania wenzako!?

Naanza kuamini ni sisi kweli, tuliowauza ndg zetu utumwani...

🙂 Huenda hata Yuda alikuwa Mwenye asili yetu.
Mkuu mimi ni Afisa Afya, nazungumzia uhalisia. Kama hao Cowbell wanafanya hivyo ujue ni kawaida yao, siyo mara ya kwanza.

Na hao waliowakamata hawana budget, wanategemea fines na rushwa. Ukiona wanawekana wazi kwenye media na kupelekana polisi ujue hawakuelewana.

Ndio nchi yetu ilivyo. Hata kwenye maduka ya jirani na kwenye depots expired peoducts kibao tu. Supermarkets ndio huwa at least wanajitahidi kufanya ukaguzi.
 
Mkuu mimi ni Afisa Afya, nazungumzia uhalisia. Kama hao Cowbell wanafanya hivyo ujue ni kawaida yao, siyo mara ya kwanza...
Nashukuru kwa ufafanuzi Mkuu. Shida ninayoiona Cowbel na wengine wanajifunza kutoka kwetu wenyewe..

Watanzania tunajali sana vitu kuliko utu. Huwa nawatania watu kwenye bendera tulitakiwa kuwa na rangi nyeusi nyingi kuliko hizo nyingine zote...

Biggest and most valuable resource ilipaswa kuwa "Mtu" tuheshimu afya yake, uhai wake, uhuru wake, heshima yake nk. Wageni wangeogopa sana kuleta mzaha wa aina yoyote.

Sasa sisi ndio tunaongoza kwa kuuziana kila aina ya uchafu..kupigana changa ndio sifa.. kuibiana.. ndio ujiko... Na wageni wakifika kwa warumi sisi wanajifunza kuishi kama warumi.
 
Nashukuru kwa ufafanuzi Mkuu. Shida ninayoiona Cowbel na wengine wanajifunza kutoka kwetu wenyewe...
Mkuu yaani nchi hii ukiwa sensitive sana utaishi kwa shida sana. Hata huko kwenye depots za makampuni ya vinywaji kama Coca-cola, Pepsi expired products kibao ukiwauliza wanasema eti wanasubiria TFDA/sasa TMDA ndio huwa wanafanya disposal.

Huku mtaani ndio kabisa tunakula ng'ombe, mbuzi na kuku vibudu kila siku.

Kuna siku nilikuwa machinjioni, ng'ombe aliletwa akawa amefia kwenye roli: Wakapewa wagogo wazike, kumbe kule shimoni walikuwa wametega mfuko, wanakatakata vipande wanarusha kwenye mfuko halafu wanauza mitaani.

Hata samaki huko kwenye mabucha zinazoharibika huwa hazitupwi vile vile nyanya magengeni huko ndio bidhaa za mama ntilie hizo.
 
Mkuu yaani nchi hii ukiwa sensitive sana utaishi kwa shida sana. Hata huko kwenye depots za makampuni ya vinywaji kama Coca-cola, Pepsi expired products kibao ukiwauliza wanasema eti wanasubiria TFDA/sasa TMDA ndio huwa wanafanya disposal...
Yaani sijui tuko hivi by design au by decision!?

Unaweza kuhisi bado tunamalizia kubadilika kutok kwenye unyama... Akili kama za mbuzi
 
Back
Top Bottom