Kampuni ya MOFAT ya Tanzania yapewa tenda ya kuendesha Mwendokasi kipande cha Gerezani-Mbagala kwa miaka 12

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
83,659
Reaction score
90,151
My Take
Naunga mkono dhana ya uwekezaji wa ndani kuliko wa Nje.

Wawekezaji wa ndani wenye uwezo jitokezeni mkamate tenda na muoneshe ufanisi tusiwe kama Mwendokasi ya UDART.

View: https://www.instagram.com/p/DLPL2x6IBJ2/?igsh=ejdmNzRuMzZuY3k5

---
KAMPUNI ya Kizalendo ya Mofat imepewa mkataba wa miaka 12 na Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka Dar es Salaam (Dart) kwa ajili ya kuendesha Awamu ya Pili ya mfumo wa Mabasi Yaendayo Haraka (BRT), unaotoka Gerezani hadi Mbagala.

Kampuni hiyo ya Kizalendo ya Mofat inatarajiwa kuanza kutumia mabasi 255 yanayotumia gesi ifikapo Agosti 2025.

Akizungumza hayo hivi karibuni Mkurugenzi Mtendaji wa Dart, Dkt. Athuman Kihamia, alithibitisha kuhusu mkataba huo jana katika mahojiano ya simu akiwa nje ya nchi.

Alisema maendeleo yanakuja wakati serikali ikihamia rasmi katika kuhamisha uendeshaji wa awamu ya kwanza na ya pili ya mfumo wa BRT kwa sekta binafsi, ikiwa ni juhudi za kuongeza ufanisi na kushughulikia changamoto za muda mrefu za usafiri kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam.

''Hii ni kampuni ya kizalendo na tayari imepata mitaji na dhamana zinazohitajika kuendesha huduma hii.

"Hivyo hii ni hatua kubwa katika juhudi zetu za kutoa huduma za usafiri wa uhakika na bora kwa wakazi wa jiji. Kampuni hiyo imejitolea kuleta mabasi ndani ya muda tuliokubaliana,"alisema Dkt. Kihamia.

Mwelekeo wa kuwashirikisha zaidi waendeshaji wa ndani ulisisitizwa pia Jumatatu na Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu, aliyewaambia wahariri jijini Dar es Salaam kuwa Dart sasa inalenga kuvutia wawekezaji zaidi—hasa kwa kuwa ujenzi wa Awamu ya Kwanza na ya Pili umekamilika, huku Awamu ya Tatu ikitarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka huu.

Kwa mujibu wa mfumo mpya, mfumo wa BRT utaendeshwa na kampuni kati ya nne hadi sita, badala ya mfumo wa sasa wa mtoa huduma mmoja unaoongozwa na UDA Rapid Transit (Udart).

View: https://youtu.be/Wdo4iyyC_HA?feature=shared
 
Historia ya MOFAT imekaaje, ilianzishwa lini?

Je, ina uzoefu wa kuendesha mradi wa mabasi hadi 255?

Je, imefanya wapi kazi ya kuendesha mradi kama huo?

Je, mmiliki ni nani?

Mtaji wake ni kiasi gani?

MOFAT ina tofauti gani na Emirates National Group (ENG) kutoka Abu Dhabi?

Au ndo wamegawana njia (awamu ya kwanza na awamu ya pili) ?
 
KAMPUNI ya Kizalendo ya Mofat imepewa mkataba wa miaka 12 na Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka Dar es Salaam (Dart) kwa ajili ya kuendesha Awamu ya Pili ya mfumo wa Mabasi Yaendayo Haraka (BRT), unaotoka Gerezani hadi Mbagala.

Kampuni hiyo ya Kizalendo ya Mofat inatarajiwa kuanza kutumia mabasi 255 yanayotumia gesi ifikapo Agosti 2025.

Akizungumza hayo hivi karibuni Mkurugenzi Mtendaji wa Dart, Dkt. Athuman Kihamia, alithibitisha kuhusu mkataba huo jana katika mahojiano ya simu akiwa nje ya nchi.

Alisema maendeleo yanakuja wakati serikali ikihamia rasmi katika kuhamisha uendeshaji wa awamu ya kwanza na ya pili ya mfumo wa BRT kwa sekta binafsi, ikiwa ni juhudi za kuongeza ufanisi na kushughulikia changamoto za muda mrefu za usafiri kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam.

''Hii ni kampuni ya kizalendo na tayari imepata mitaji na dhamana zinazohitajika kuendesha huduma hii.

"Hivyo hii ni hatua kubwa katika juhudi zetu za kutoa huduma za usafiri wa uhakika na bora kwa wakazi wa jiji. Kampuni hiyo imejitolea kuleta mabasi ndani ya muda tuliokubaliana,"alisema Dkt. Kihamia.

Mwelekeo wa kuwashirikisha zaidi waendeshaji wa ndani ulisisitizwa pia Jumatatu na Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu, aliyewaambia wahariri jijini Dar es Salaam kuwa Dart sasa inalenga kuvutia wawekezaji zaidi—hasa kwa kuwa ujenzi wa Awamu ya Kwanza na ya Pili umekamilika, huku Awamu ya Tatu ikitarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka huu.

Kwa mujibu wa mfumo mpya, mfumo wa BRT utaendeshwa na kampuni kati ya nne hadi sita, badala ya mfumo wa sasa wa mtoa huduma mmoja unaoongozwa na UDA Rapid Transit (Udart).

IMG-20250604-WA1078.jpg
IMG-20250604-WA1079.jpg
IMG-20250604-WA1081.jpg
IMG-20250604-WA1082.jpg
 
Safi sana. Watakuja kuuliza ni dini gani? Kama unabisha subiri.
 
Back
Top Bottom