Kampuni ya MOFAT ya Tanzania yapewa tenda ya kuendesha Mwendokasi kipande cha Gerezani-Mbagala kwa miaka 12

Kampuni ya MOFAT ya Tanzania yapewa tenda ya kuendesha Mwendokasi kipande cha Gerezani-Mbagala kwa miaka 12

Heche na Lissu huwa wanalalamika huku wanatembea kwenye lami ya Samia, mahotelini wanaoga maji safi ya Samia, na wakiumwa wanafaidi matunda ya mifumo mizuri ya afya
 
Hao mafukara ndio wanawatajirisha hao wezi, hao mafukara ndio wamenunua ndege, wamejenga barabara, madaraja, airports n.k...

Pumbaf acha dharau...
Hawawatajirishi kupitia sadaka kama gwajima,hao matajiri waliumiza vichwa kubuni bidhaa/huduma kwa hao fukara
 
Hawawatajirishi kupitia sadaka kama gwajima,hao matajiri waliumiza vichwa kubuni bidhaa/huduma kwa hao fukara
Gwajima hawalazimishi kutoa sadaka..
Kwenye siasa ndipo wezi walipo...

Kesi ya Richmond 2006.. USD milioni 179...

Akaunt ya Tegeta escrow.. USD milioni 180 wakabugia hao unaita matajiri.. 2014 hio


Kesi ya EPA benki kuu .. Tshs bilioni 133 watu wakalala nazo mbele kwa mbele... Tukapigwa chenga ya mwili eti Bilali sijui kafariki blah blah bah.... 2005/2008

Kesi ya radar 2002.. hapa ilipigwa pesa ndefu ikabidi serikali ya uingereza iingilie kati...

Kwa namna hio kwanini usiwe tajiri? kama wanaiba kiasi hiko utajiri lazima.
 
Wanashindwa kusema ni CCM ndio kawazunguka watanganyika kwenye KAZI hii.
Kazi ni kipimo cha utu
 
Gwajima hawalazimishi kutoa sadaka..
Kwenye siasa ndipo wezi walipo...

Kesi ya Richmond 2006.. USD milioni 179...

Akaunt ya Tegeta escrow.. USD milioni 180 wakabugia hao unaita matajiri.. 2014 hio


Kesi ya EPA benki kuu .. Tshs bilioni 133 watu wakalala nazo mbele kwa mbele... Tukapigwa chenga ya mwili eti Bilali sijui kafariki blah blah bah.... 2005/2008

Kesi ya radar 2002.. hapa ilipigwa pesa ndefu ikabidi serikali ya uingereza iingilie kati...

Kwa namna hio kwanini usiwe tajiri? kama wanaiba kiasi hiko utajiri lazima.
Kivipi escrow ni pesa ya serikali?..epa ni pesa ya kampuni za far east..radar mzee benja...halafu hadi kilaini alikula escrow,ni tajiri?!..chenge ni tajiri?.. azam,mo,gsm,manji etc walipata hiyo migao!!
 
KAMPUNI ya Kizalendo ya Mofat imepewa mkataba wa miaka 12 na Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka Dar es Salaam (Dart) kwa ajili ya kuendesha Awamu ya Pili ya mfumo wa Mabasi Yaendayo Haraka (BRT), unaotoka Gerezani hadi Mbagala.

Kampuni hiyo ya Kizalendo ya Mofat inatarajiwa kuanza kutumia mabasi 255 yanayotumia gesi ifikapo Agosti 2025.

Akizungumza hayo hivi karibuni Mkurugenzi Mtendaji wa Dart, Dkt. Athuman Kihamia, alithibitisha kuhusu mkataba huo jana katika mahojiano ya simu akiwa nje ya nchi.

Alisema maendeleo yanakuja wakati serikali ikihamia rasmi katika kuhamisha uendeshaji wa awamu ya kwanza na ya pili ya mfumo wa BRT kwa sekta binafsi, ikiwa ni juhudi za kuongeza ufanisi na kushughulikia changamoto za muda mrefu za usafiri kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam.

''Hii ni kampuni ya kizalendo na tayari imepata mitaji na dhamana zinazohitajika kuendesha huduma hii.

"Hivyo hii ni hatua kubwa katika juhudi zetu za kutoa huduma za usafiri wa uhakika na bora kwa wakazi wa jiji. Kampuni hiyo imejitolea kuleta mabasi ndani ya muda tuliokubaliana,"alisema Dkt. Kihamia.

Mwelekeo wa kuwashirikisha zaidi waendeshaji wa ndani ulisisitizwa pia Jumatatu na Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu, aliyewaambia wahariri jijini Dar es Salaam kuwa Dart sasa inalenga kuvutia wawekezaji zaidi—hasa kwa kuwa ujenzi wa Awamu ya Kwanza na ya Pili umekamilika, huku Awamu ya Tatu ikitarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka huu.

Kwa mujibu wa mfumo mpya, mfumo wa BRT utaendeshwa na kampuni kati ya nne hadi sita, badala ya mfumo wa sasa wa mtoa huduma mmoja unaoongozwa na UDA Rapid Transit (Udart).

View attachment 3355892View attachment 3355893View attachment 3355895View attachment 3355896
Hawa wazalendo mbona ni wanaccm tuu! Kwshiuo huu ni mradi wa CCM.
 
Kivipi escrow ni pesa ya serikali?..epa ni pesa ya kampuni za far east..radar mzee benja...halafu hadi kilaini alikula escrow,ni tajiri?!..chenge ni tajiri?.. azam,mo,gsm,manji etc walipata hiyo migao!!
Vyovyote ilivyokua hizo pesa ilipaswa zikafanye kazi kusaidia wananchi..
Ina maana huo mradi amepewa Mo, Gsm, Bakhresa n.k?

Mi nimesema huu mchongo ni wanasiasa...
 
Back
Top Bottom