Kampuni ya PAF Promotion yampeleka Mahakamani Mwakinyo, yamdai fidia ya mamilioni

Kampuni ya PAF Promotion yampeleka Mahakamani Mwakinyo, yamdai fidia ya mamilioni

Hawa waliofungua kesi ni wajinga, yaani mtu umemlipa dola 3000 halafu unataka akurejeshee dola 50,000+ hapo wataambulia Dola 3000 tu na gharama za kesi, waache utapeli na wakumbuke kesi ya Madai hafungwi mtu, na kila biashara inapaswa iwe na Bima kuensure unforeseen liabilities kama hizi, kwahiyo wakawadai kampuni yao ya Bima.
Tatizo ni kwamba haujaangalia kwa mtazamo wa kisheria. Fidia ya mapato yaliyotazamiwa ni jambo la kawaida kisheria. Mtu anaweza akavamia kiwanja chako na kukuchelewesha kukiendeleza, unaweza ukamdai fidia ya mapato ambayo unakadiria ungeyapata. Huwa inakubalika, ila viwango vinaweza kurekebishwa na mahakama
 
Tatizo hiyo fidia ni exaggerated mtu umemuona anathamani ya USD 3,000 unawezaje kuprove kwamba amekutia hasara ya zaidi ya Dollar 50,000/= hawa jamaa ni wanyonyaji kishenzii na hapa wakakutana na kichwa cha mwenda wazimu...tukae kwa kutulia tuone Kesi itakavyoenda.
 
Hiyo USD 3,000 ni malipo aliyokabidhiwa Mwakinyo, na hiyo USD 50,000 ni hasara ya kukosa mapato iliyotegemea kutoka kwa wadhamini.
 
Tatizo ni kwamba haujaangalia kwa mtazamo wa kisheria. Fidia ya mapato yaliyotazamiwa ni jambo la kawaida kisheria. Mtu anaweza akavamia kiwanja chako na kukuchelewesha kukiendeleza, unaweza ukamdai fidia ya mapato ambayo unakadiria ungeyapata. Huwa inakubalika, ila viwango vinaweza kurekebishwa na mahakama
Kumbe ni makadirio ya mapato unayohisi ungepata but Jambo liko NDIVYO SIVYO
 
Kumbe ni makadirio ya mapato unayohisi ungepata but Jambo liko NDIVYO SIVYO
Mahakamani unaposhtakiwa jamaa anakuandalia mashtaka mengi mengi ili upoteze concentration. Anaweza asishinde hilo ila likasaidia ashinde mengine. Hebu fikiria umempiga mtu halafu unasomewa mashtaka kadhaa: shambulio la mwili, kusababisha maumivu, kumsababishia fedheha kubwa, kumvunjia heshima, kumsababishia hasara ya kupoteza simu na fedha nk
 
Hii kesi imenikumbusha uzi mmoja niliowahi kuusoma humu. Kuna dada aliweka bond nyumba yake,akachukua mkopo Bank fulani kwa ajili ya biashara yake ya vipodozi kutoka UK ile hati ya nyumba ikapotelea kwenye mikono ya bank. Akafungua kesi mahakamabi, sikumbuki iliishaje ila palikuwa na lundo la madai ya fidia kutoka kwa huyo dada dhidi ya Bank
 
Duuuh kumbe maisha ni magumu kote kote aseeeh, mtu kama Mwakinyo na CV yake nzito vile anapigana pambano kwa 3000 USD?! Sasa hawa mabondia wengine wa chini yake wanalipwaje?! Yani hela ya kulipia ukumbi ni kubwa (8M) kuliko anayolipwa Mwakinyo?!
 
Kesi dhidi ya bondia wa ngumi za kulipwa Nchini, Hassan Mwakinyo ambayo imefunguliwa na Kampuni ya PAF Promotion inatarajia kutajwa kwa mara ya kwanza Novemba 13, 2023 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu, A.H. Msumi ikiwa na jumla ya madai 8 ya msingi.

Kampuni hiyo imewasilisha madai hayo kupitia wito wa kesi uliotolewa na Mahakama ambapo PAF imeiomba Mahakama itamke kwamba bondia huyo amevunja mkataba wa kupigana.

Madai ya pili, PAF imeiomba Mahakama kumtaka Mwakinyo aombe radhi kwa kuichafua kutokana na kutoa taarifa za uongo kupitia Vyombo vya Habari alivyotumia kuichafua Kampuni na Wakurugenzi wake.

Madai ya tatu, PAF imeiomba Mahakama ilipwe fidia ya Shilingi 142,500,000 (Milioni 142.5) kutokana na hasara ya kukosa mapato iliyotegemea kutoka kwa wadhamini.

Madai ya nne, imeiomba Mahakama kumtaka Mwakinyo arejeshe fedha Dola za Marekani 3,000 alizopewa kuelekea pambano hilo alilotakiwa kupigana.
View attachment 2792048
Madai ya tano, PAF imeomba kurejeshewa Shilingi Milioni 8 yakiwa ni malipo ya kulipia ukumbi.

Madai namba sita, PAF imeomba kurejeshewa Shilingi 1,287,500 ikiwa ni gharama za malazi ya mpinzani wa bondia huyo.

Madai namba saba, PAF imeomba kurejeshewa Shilingi 3,832,000 ambayo ni gharama za tiketi za ndege za mpinzani wake pamoja na Wasaidizi wake.

Aidha, mbali ya madai hayo, PAF kupitia wakili wake, Herry Kauki wa Kampuni ya Wakili ya Shepron Attorneys ya Dar es Salaam, imeomba Mahakama kulipwa jumla ya Shilingi milioni 150 ikiwa ni madhara ya jumla waliopata baada ya bondia huyo kushindwa kupanda ulingoni tofauti na mkataba wake aliosaini.

Ikumbukwe Septemba 29, 2023, Mwakinyo hakupanda ulingoni katika pambano lililoandaliwa na PAF kwa kile alichonukuliwa akisema ni waratibu hao kukiuka masharti.

Chanzo: boxinghubtz
iwe fundisho kuleta uswahili kwenye biashara za watu
 
Back
Top Bottom