Kampuni ya PAF Promotion yampeleka Mahakamani Mwakinyo, yamdai fidia ya mamilioni

Tatizo ni kwamba haujaangalia kwa mtazamo wa kisheria. Fidia ya mapato yaliyotazamiwa ni jambo la kawaida kisheria. Mtu anaweza akavamia kiwanja chako na kukuchelewesha kukiendeleza, unaweza ukamdai fidia ya mapato ambayo unakadiria ungeyapata. Huwa inakubalika, ila viwango vinaweza kurekebishwa na mahakama
 
Tatizo hiyo fidia ni exaggerated mtu umemuona anathamani ya USD 3,000 unawezaje kuprove kwamba amekutia hasara ya zaidi ya Dollar 50,000/= hawa jamaa ni wanyonyaji kishenzii na hapa wakakutana na kichwa cha mwenda wazimu...tukae kwa kutulia tuone Kesi itakavyoenda.
 
Hiyo USD 3,000 ni malipo aliyokabidhiwa Mwakinyo, na hiyo USD 50,000 ni hasara ya kukosa mapato iliyotegemea kutoka kwa wadhamini.
 
Kumbe ni makadirio ya mapato unayohisi ungepata but Jambo liko NDIVYO SIVYO
 
Kumbe ni makadirio ya mapato unayohisi ungepata but Jambo liko NDIVYO SIVYO
Mahakamani unaposhtakiwa jamaa anakuandalia mashtaka mengi mengi ili upoteze concentration. Anaweza asishinde hilo ila likasaidia ashinde mengine. Hebu fikiria umempiga mtu halafu unasomewa mashtaka kadhaa: shambulio la mwili, kusababisha maumivu, kumsababishia fedheha kubwa, kumvunjia heshima, kumsababishia hasara ya kupoteza simu na fedha nk
 
Hii kesi imenikumbusha uzi mmoja niliowahi kuusoma humu. Kuna dada aliweka bond nyumba yake,akachukua mkopo Bank fulani kwa ajili ya biashara yake ya vipodozi kutoka UK ile hati ya nyumba ikapotelea kwenye mikono ya bank. Akafungua kesi mahakamabi, sikumbuki iliishaje ila palikuwa na lundo la madai ya fidia kutoka kwa huyo dada dhidi ya Bank
 
Duuuh kumbe maisha ni magumu kote kote aseeeh, mtu kama Mwakinyo na CV yake nzito vile anapigana pambano kwa 3000 USD?! Sasa hawa mabondia wengine wa chini yake wanalipwaje?! Yani hela ya kulipia ukumbi ni kubwa (8M) kuliko anayolipwa Mwakinyo?!
 
iwe fundisho kuleta uswahili kwenye biashara za watu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…