Kampuni ya Reli Tanzania(TRL) yavikana vichwa vya Treni, yataka virudishwe vilipotoka

Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) imekanusha kuhusika na vichwa 11 vilivyoshushwa na kutelekezwa katika Bandari ya Dar es Salaam hivi karibuni.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Deusdedit Kakoko, vichwa hivyo vilivyoshushwa na meli ya Mesina Line tangu wiki iliyopita, na kwamba ni mali ya TRL.

Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo, Masanja Kadogosa jana alisema TRL haihusiki kwa namna yoyote na vichwa hivyo kwa kuwa hakuna taarifa zozote zinahusu uagizwaji wake.

Alisema pia kwa mujibu wa Sheria ya Manunuzi, kampuni hiyo inapofanya manunuzi yoyote lazima kuwepo na mkataba wa makubaliano na kampuni husika inayouza bidhaa, lakini haina mkataba wowote unaohusu ununuzi wa vichwa hivyo.

Alieleza kuwa taratibu za manunuzi zinafahamika kwani endapo kampuni hiyo ingeagiza vichwa hivyo ingetakiwa kupeleka mtu wake kwa ajili ya ukaguzi wakati vinatengenezwa na mara baada ya kutengenezwa kabla ya kupakiwa kwenye meli. “Lakini hiyo kitu hakuna, hatukuwa na watu wetu kwa kuwa si mali yetu,” alieleza.

Pamoja na hayo, alisema ili mzigo wowote umfikie mhusika lazima kuwepo na nyaraka ya kutolea mzigo bandarini ambayo pia huwa na makubaliano mengine baina ya mnunuzi na muuzaji ambayo katika sakata hilo, TRL wamesisitiza hawana nyaraka hiyo.

Alisema TRL haivitambui vichwa hivyo kwa kuwa si mali yake. “Hivi ni vichwa vikubwa sasa kwanini tuvikatae kama ni vyetu, ila ukweli ni kwamba hatuvitambui kabisa,” alieleza mkuu huyo wa reli nchini.

Juzi wakati akizundua Mradi wa Uboreshaji wa Bandari ya Dar es Salaam (DSMGP), Rais John Magufuli aliibua hoja hiyo ya vichwa vya treni kushushwa bandarini na kutekelezwa bila kuwa na mwenyewe na kuitaka TPA pamoja na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, kufuatilia kwa kina suala hilo.

Dk Magufuli alisema anazo taarifa za kushushwa kwa vichwa vya treni takribani 15 katika bandari hiyo, ambavyo mmiliki wake hafahamiki na meli iliyovileta imeshaondoka.

Hata hivyo, mkurugenzi wa mamlaka hiyo ya TPA Kakoko pamoja na kuthibitisha kushushwa kwa vichwa hivyo kutoka kwa meli ya Mesina Line, iliyobeba mzigo huo kutoka kwa Komazi Trading Co, alibainisha wazi kuwa vichwa hivyo ni vya TRL.

Alisema vichwa hivyo ni awamu ya pili iliyoagizwa tangu serikali ya awamu ya nne miaka mitatu iliyopita, ambapo awamu ya kwanza ilishaletwa na vichwa vyake kuchukuliwa na hadi leo vinatumiwa na TRL.

Alifafanua kuwa baada ya uchunguzi wa TPA ilibaini kuwa kuna mgogoro unaoendelea kati ya TRL na kampuni ya Komazi na kwamba TRL ilishagoma kuvichukua vichwa hivyo lakini suala hilo, halikutaarifiwa kwa TPA.

Credit: Mpekuzi huru.

Pia : Mmiliki wa vichwa 13 vya treni bandarini afahamika
Itaeleweka tu.
 
Sasa ilikuwaje TPA wakakubali kushushwa kwa kitu ambacho mmiliki hajatajwa kwenye bill of landing
Hapa lazima kutakuwa na UCHAWI, wewe subiri kwanza mchawi atafutwe kimyakimya...atapatikana tu. Kwa kweli itabidi niwasifu usalama wa taifa maana wamefanya kazi nzuri sana. Haya sasa ndio matumizi sahihi ya usalama wa taifa badala ya kutwa kucha kuwaandama CHADEMA tu.
 
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari nchini, Engineer Deusdedit Kakoko amesema vichwa vya treni vinavyodaiwa kutelekezwa bandarini ni mali ya shirika la Reli nchini TRL na kwamba vina nembo ya TRL (Tanzania Railway Limited). Kakoko amesema TRL walinunua vichwa hivyo bila kufuata utaratibu kutoka kampuni ya EMD ya nchini Marekani, lakini vimetengenezwa na kampuni ya DCD ya nchini Afrika Kusini.

Maelezo ya Kakoko yanahitimisha taarifa "zilizovumishwa" hivi karibuni kuwa vichwa hivyo havina mwenyewe. Kwa lugha rahisi ni kwamba Engineer Kakoko amesema SI KWELI kwamba vichwa hivyo havina mwenyewe. Kakoko anasema ni vya TRL na vina nembo ya TRL.

Source:
Mmiliki wa vichwa 13 vya treni bandarini afahamika

MyTake:
Nimetafakari sana maelezo ya Kakoko nikakumbuka zile tambo za juzi kwamba tumekamata vichwa vya treni ambavyo havina mwenyewe. Nikajiuliza lengo la tambo zile lilikua nini? Kama Kakoko alijua vichwa ni vya TRL ilikuaje "mwenye nyumba" akasema havina mwenyewe? Hakumuuliza Kakoko? Alidanganywa? Alijua ukweli lakini akatupotosha? Ili iweje? Kwa faida ya nani?

Kwani angesema ni vya TRL lakini vilinunuliwa bila kufuata utaratibu kungekua na tatizo gani? Kwanini aseme uongo kuwa havina mwenyewe wakati vina nembo ya TRL? Ina maana hakuona hata nembo? Au hiyo nembo iliwekwa baada ya "mwenye nyumba" kuondoka? Anyway tuendelee kumuombea.!!

Vichwa visivyojulijana ni vya nani vilivyopo bandarini
View attachment 535375

Treni ya TRL ikiwa kazini,hapo ilikua maeneo ya Dodoma. Hata kama tunadanganywa ila sasa imezidi

Nikifikiria nje ya box nadhani kuwa hivi vichwa vilikuwa on transit kwenda labda Kongo au nchi zingine ila vimekuwa branded kwamba ni mali ya TRL ili kuwepa kodi. Anyway, ngoja tuwasubiri wenye vichwa waje. Kama vikikosa mwenyewe, serikali itavitaifisha kwa manufaa ya wananchi.
 
Kusoma hatujui,picha tunaona ila kila mkubwa anajifanya hamnazo
 
Pamoja na hayo, alisema ili mzigo wowote umfikie mhusika lazima kuwepo na nyaraka ya kutolea mzigo bandarini ambayo pia huwa na makubaliano mengine baina ya mnunuzi na muuzaji ambayo katika sakata hilo, TRL wamesisitiza hawana nyaraka hiyo.
Huyu DG naye ni jipu anapaswa atueleze vizuri juu ya hii issue haiwezekani mzigo unashushwa bila documents. Lazima documents ziwepo ili mzigo ushushwe asijifanye hajui hili deal
 
cf969d6e1bb3064bac4cd3b52a42b0ec.jpg

View attachment 535327
KAMPUNI ya Reli Tanzania (TRL) imekanusha kuhusika na vichwa 11 vilivyoshushwa na kutelekezwa katika Bandari ya Dar es Salaam hivi karibuni. Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Deusdedit Kakoko, vichwa hivyo vilivyoshushwa na meli ya Mesina Line tangu wiki iliyopita, na kwamba ni mali ya TRL.

Akizungumza na gazeti hili Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo, Masanja Kadogosa alisema TRL haihusiki kwa namna yoyote na vichwa hivyo kwa kuwa hakuna taarifa zozote zinahusu uagizwaji wake.

Alisema pia kwa mujibu wa Sheria ya Manunuzi, kampuni hiyo inapofanya manunuzi yoyote lazima kuwepo na mkataba wa makubaliano na kampuni husika inayouza bidhaa, lakini haina mkataba wowote unaohusu ununuzi wa vichwa hivyo.

Alieleza kuwa taratibu za manunuzi zinafahamika kwani endapo kampuni hiyo ingeagiza vichwa hivyo ingetakiwa kupeleka mtu wake kwa ajili ya ukaguzi wakati vinatengenezwa na mara baada ya kutengenezwa kabla ya kupakiwa kwenye meli. “Lakini hiyo kitu hakuna, hatukuwa na watu wetu kwa kuwa si mali yetu,” alieleza.

Pamoja na hayo, alisema ili mzigo wowote umfikie mhusika lazima kuwepo na nyaraka ya kutolea mzigo bandarini ambayo pia huwa na makubaliano mengine baina ya mnunuzi na muuzaji ambayo katika sakata hilo, TRL wamesisitiza hawana nyaraka hiyo.

Alisema TRL haivitambui vichwa hivyo kwa kuwa si mali yake. “Hivi ni vichwa vikubwa sasa kwanini tuvikatae kama ni vyetu, ila ukweli ni kwamba hatuvitambui kabisa,” alieleza mkuu huyo wa reli nchini.

Juzi wakati akizundua Mradi wa Uboreshaji wa Bandari ya Dar es Salaam (DSMGP), Rais John Magufuli aliibua hoja hiyo ya vichwa vya treni kushushwa bandarini na kutekelezwa bila kuwa na mwenyewe na kuitaka TPA pamoja na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, kufuatilia kwa kina suala hilo.

Dk Magufuli alisema anazo taarifa za kushushwa kwa vichwa vya treni takribani 15 katika bandari hiyo, ambavyo mmiliki wake hafahamiki na meli iliyovileta imeshaondoka. Hata hivyo, mkurugenzi wa mamlaka hiyo ya TPA Kakoko pamoja na kuthibitisha kushushwa kwa vichwa hivyo kutoka kwa meli ya Mesina Line, iliyobeba mzigo huo kutoka kwa Komazi Trading Co, alibainisha wazi kuwa vichwa hivyo ni vya TRL.

Alisema vichwa hivyo ni awamu ya pili iliyoagizwa tangu serikali ya awamu ya nne miaka mitatu iliyopita, ambapo awamu ya kwanza ilishaletwa na vichwa vyake kuchukuliwa na hadi leo vinatumiwa na TRL.

Alifafanua kuwa baada ya uchunguzi wa TPA ilibaini kuwa kuna mgogoro unaoendelea kati ya TRL na kampuni ya Komazi na kwamba TRL ilishagoma kuvichukua vichwa hivyo lakini suala hilo, halikutaarifiwa kwa TPA

Chanzo: Habari leo

My Take:

Kama hawavitaki wamgawie Askofu Gwajima wa ufufuo na Uzima kwani anatafuta vichwa Treni.
Tutapiga sana kelele kifupi tatizo letu ni usanii wa serikali hii. Eti vichwa havina mwenyewe Messina Line walivishushaje,haya ni maajabu ya pekee sidhani kama kuna mahali yashawahi kutokea haya
 
Vichwa vikubwa "Heavy Duty" Tatizo deal imebuma maanake Reli inajengwa Standard Gauge.
Lakini vichwa 15 ni vingi mno kukosa mkataba ,tujiandae kushtakiwa japo tunakana.
 
Kwanini tuumize vichwa hali yakuwa tumeokota dodo kwenye mnazi,

Chamsingi magu ainue mikono juu kushukuru zawadi aliyo pewa na mungu,
Mkuu hapo wewe jenga Reli steshini - Mkuranga, stesheni - bagamoyo na kwingine ili kupunguza adha ya usafiri

Ukicheki maisha yenyewe yamekuwa magugu kidogo wananchi watapata ahuweni

Hivo vichwa zawadi ya Nchi yetu
 
cf969d6e1bb3064bac4cd3b52a42b0ec.jpg

View attachment 535327
KAMPUNI ya Reli Tanzania (TRL) imekanusha kuhusika na vichwa 11 vilivyoshushwa na kutelekezwa katika Bandari ya Dar es Salaam hivi karibuni. Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Deusdedit Kakoko, vichwa hivyo vilivyoshushwa na meli ya Mesina Line tangu wiki iliyopita, na kwamba ni mali ya TRL.

Akizungumza na gazeti hili Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo, Masanja Kadogosa alisema TRL haihusiki kwa namna yoyote na vichwa hivyo kwa kuwa hakuna taarifa zozote zinahusu uagizwaji wake.

Alisema pia kwa mujibu wa Sheria ya Manunuzi, kampuni hiyo inapofanya manunuzi yoyote lazima kuwepo na mkataba wa makubaliano na kampuni husika inayouza bidhaa, lakini haina mkataba wowote unaohusu ununuzi wa vichwa hivyo.

Alieleza kuwa taratibu za manunuzi zinafahamika kwani endapo kampuni hiyo ingeagiza vichwa hivyo ingetakiwa kupeleka mtu wake kwa ajili ya ukaguzi wakati vinatengenezwa na mara baada ya kutengenezwa kabla ya kupakiwa kwenye meli. “Lakini hiyo kitu hakuna, hatukuwa na watu wetu kwa kuwa si mali yetu,” alieleza.

Pamoja na hayo, alisema ili mzigo wowote umfikie mhusika lazima kuwepo na nyaraka ya kutolea mzigo bandarini ambayo pia huwa na makubaliano mengine baina ya mnunuzi na muuzaji ambayo katika sakata hilo, TRL wamesisitiza hawana nyaraka hiyo.

Alisema TRL haivitambui vichwa hivyo kwa kuwa si mali yake. “Hivi ni vichwa vikubwa sasa kwanini tuvikatae kama ni vyetu, ila ukweli ni kwamba hatuvitambui kabisa,” alieleza mkuu huyo wa reli nchini.

Juzi wakati akizundua Mradi wa Uboreshaji wa Bandari ya Dar es Salaam (DSMGP), Rais John Magufuli aliibua hoja hiyo ya vichwa vya treni kushushwa bandarini na kutekelezwa bila kuwa na mwenyewe na kuitaka TPA pamoja na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, kufuatilia kwa kina suala hilo.

Dk Magufuli alisema anazo taarifa za kushushwa kwa vichwa vya treni takribani 15 katika bandari hiyo, ambavyo mmiliki wake hafahamiki na meli iliyovileta imeshaondoka. Hata hivyo, mkurugenzi wa mamlaka hiyo ya TPA Kakoko pamoja na kuthibitisha kushushwa kwa vichwa hivyo kutoka kwa meli ya Mesina Line, iliyobeba mzigo huo kutoka kwa Komazi Trading Co, alibainisha wazi kuwa vichwa hivyo ni vya TRL.

Alisema vichwa hivyo ni awamu ya pili iliyoagizwa tangu serikali ya awamu ya nne miaka mitatu iliyopita, ambapo awamu ya kwanza ilishaletwa na vichwa vyake kuchukuliwa na hadi leo vinatumiwa na TRL.

Alifafanua kuwa baada ya uchunguzi wa TPA ilibaini kuwa kuna mgogoro unaoendelea kati ya TRL na kampuni ya Komazi na kwamba TRL ilishagoma kuvichukua vichwa hivyo lakini suala hilo, halikutaarifiwa kwa TPA

Chanzo: Habari leo

My Take:

Kama hawavitaki wamgawie Askofu Gwajima wa ufufuo na Uzima kwani anatafuta vichwa Treni.
Ama yatakuwa ni yale ambayo wahindi wali ya peleka India kutengeneza nadhani uchunguzi uanzie hapo
 
Inawezekana siyo vyao kweli,TRL inaweza kua{TOGO RAILWAY} hiyo meli imekosea tu kushusha.
 
Magu anajuwa fika!kuwa hivyo vichwa ni vyanani, Hiyo ni geresha ya nagu kutaka kiki za kijinga.Kitambo tu nimeshamstukia huyo jamaa.Ana fiks kishenzi!!.
 
Ni vya lowasa
 
Kwenye rasilimali za umma tuache utani,inakuwaje vichwa vya train vije bila kuagizwa inawezekana kweli?au kuna jambo gani nyuma ya pazia,niombe mamlaka zinazohusika zichukua hatu za haraka kudhibiti ufujaji huu wa mali za umma,hapa hakuna kudhani TRL management inahusika moja kwa moja
 
Hapa lazima kutakuwa na UCHAWI, wewe subiri kwanza mchawi atafutwe kimyakimya...atapatikana tu. Kwa kweli itabidi niwasifu usalama wa taifa maana wamefanya kazi nzuri sana. Haya sasa ndio matumizi sahihi ya usalama wa taifa badala ya kutwa kucha kuwaandama CHADEMA tu.

Huyu jamaa wa TRL anachekesha... eti taratibu ni kupeleka mtu.. kwa hiyo asipoenda mtu hawawezi kuagiza na mzigo ukaja? Ujinga mtupu..

Tatizo la kufanya kazi kwa uoga uoga...
 
Back
Top Bottom