Kampuni ya Reli Tanzania(TRL) yavikana vichwa vya Treni, yataka virudishwe vilipotoka

Kampuni ya Reli Tanzania(TRL) yavikana vichwa vya Treni, yataka virudishwe vilipotoka

Hehehe wewe siku hizi umefulia, umeishiwa na hoja kiasi kwamba kwa kila mada unatafuta pa kutokea, hivi mnanunua vichwa vya treni kama karanga. Halafu they are very ugly ndio maana mumevikimbia.
Unaweka mada kibao hapa na zote ni upuuzi mtupu, kama hii sasa, uliluwa unajadili treni au watanazania? njaa itawamaliza jamani.

Hizo treni unazosema ugly umeona wapi au ni hizi picha za 2015.

JUST IN: TRL YAPOKEA Vichwa vya treni vipya viwili kutoka Afrika Kusini | Magazeti ya leo| Tanzania News |Tanzania Today
 
Vijana wa Lumumba wanazoza eti hivyo vichwa ni vywa Singa Singa wa IPTL
 
Hivi siyo viliagizwa wakati ule Mh.. Mwaki-Mango akiwa Waziri wa nani..?
 

Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) imekanusha kuhusika na vichwa 11 vilivyoshushwa na kutelekezwa katika Bandari ya Dar es Salaam hivi karibuni.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Deusdedit Kakoko, vichwa hivyo vilivyoshushwa na meli ya Mesina Line tangu wiki iliyopita, na kwamba ni mali ya TRL.

Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo, Masanja Kadogosa jana alisema TRL haihusiki kwa namna yoyote na vichwa hivyo kwa kuwa hakuna taarifa zozote zinahusu uagizwaji wake.

Alisema pia kwa mujibu wa Sheria ya Manunuzi, kampuni hiyo inapofanya manunuzi yoyote lazima kuwepo na mkataba wa makubaliano na kampuni husika inayouza bidhaa, lakini haina mkataba wowote unaohusu ununuzi wa vichwa hivyo.

Alieleza kuwa taratibu za manunuzi zinafahamika kwani endapo kampuni hiyo ingeagiza vichwa hivyo ingetakiwa kupeleka mtu wake kwa ajili ya ukaguzi wakati vinatengenezwa na mara baada ya kutengenezwa kabla ya kupakiwa kwenye meli. “Lakini hiyo kitu hakuna, hatukuwa na watu wetu kwa kuwa si mali yetu,” alieleza.

Pamoja na hayo, alisema ili mzigo wowote umfikie mhusika lazima kuwepo na nyaraka ya kutolea mzigo bandarini ambayo pia huwa na makubaliano mengine baina ya mnunuzi na muuzaji ambayo katika sakata hilo, TRL wamesisitiza hawana nyaraka hiyo.

Alisema TRL haivitambui vichwa hivyo kwa kuwa si mali yake. “Hivi ni vichwa vikubwa sasa kwanini tuvikatae kama ni vyetu, ila ukweli ni kwamba hatuvitambui kabisa,” alieleza mkuu huyo wa reli nchini.

Juzi wakati akizundua Mradi wa Uboreshaji wa Bandari ya Dar es Salaam (DSMGP), Rais John Magufuli aliibua hoja hiyo ya vichwa vya treni kushushwa bandarini na kutekelezwa bila kuwa na mwenyewe na kuitaka TPA pamoja na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, kufuatilia kwa kina suala hilo.

Dk Magufuli alisema anazo taarifa za kushushwa kwa vichwa vya treni takribani 15 katika bandari hiyo, ambavyo mmiliki wake hafahamiki na meli iliyovileta imeshaondoka.

Hata hivyo, mkurugenzi wa mamlaka hiyo ya TPA Kakoko pamoja na kuthibitisha kushushwa kwa vichwa hivyo kutoka kwa meli ya Mesina Line, iliyobeba mzigo huo kutoka kwa Komazi Trading Co, alibainisha wazi kuwa vichwa hivyo ni vya TRL.

Alisema vichwa hivyo ni awamu ya pili iliyoagizwa tangu serikali ya awamu ya nne miaka mitatu iliyopita, ambapo awamu ya kwanza ilishaletwa na vichwa vyake kuchukuliwa na hadi leo vinatumiwa na TRL.

Alifafanua kuwa baada ya uchunguzi wa TPA ilibaini kuwa kuna mgogoro unaoendelea kati ya TRL na kampuni ya Komazi na kwamba TRL ilishagoma kuvichukua vichwa hivyo lakini suala hilo, halikutaarifiwa kwa TPA.

Credit: Mpekuzi huru.

Pia : Mmiliki wa vichwa 13 vya treni bandarini afahamika
Ipo siku watu watakana hadi nguo walizovaa kuwa si zao na hawajui aliyewalisha, magufuli watu wana nidhamu ya woga si kwamba wanaku heshimu.
 
Nchi kumbe inaweza tekwa kupitia bandari yetu. Kama vichwa vya treni vinaingia then hatujui muingizani then tunasema nchi ina usalama?
 
Meneja TRC atumbuliwe hajuhi anafanya nini ni kusumbua akili tu.
Hiyo kaxi ndogo ukimuliza supplier anakupa jibu.
Na huenda kashalipwa si tunakataa vichwa.
Uchunguzi huu ni dakika sifuri ukipewa uifanye
 
Wakuu, salam kwenu.
Hili suala la vichwa vya treni vilivyoshushwa bandarini na kuambiwa hatujui mwenyewe ni jambo la aibu na fedhea sana kwa nchi inayojitawala kama Tanzania. Haingii akilini kwamba vichwa vya treni 11 vinashushwa na hatujui ni vya nani. Pamoja na vyombo vyote vya dola vinavyofanya usiku na mchana, mzigo mkubwa kiasi hicho usiwe na mwenyewe? Kwani, Bill of lading ya shehena hiyo inasemaje? Mzigo unakotoka ni wapi? Hakuna anuani? Hiki ni kiwanda kabisa ambacho bado kipo na kinaendelea.

Jambo linajitokeza hapa ni kwamba hii ni biashara ya watu ambayo ilipangwa kabla ya JPM kuingia madarakani. Sasa kimenuka kila mtu anakimbia mbali na dili. Hii ni biashara ya mabilioni, inawezekana ni biashara ya treni ya mwendo kasi airport mpaka mjni ya Mwakyembe. Vyombo vya usalama viingie kazini watueleze kulikoni.
 
Hapo kuna kidudu mtu wavichukue tu maana wenzetu huwa hawaweki vitu stock unatoa order unatengenezewa na hao komazi trading cyo vichaa wana akili timamu hata mikataba ya hyo biashara wanayo watakuja tu muda wa kulipwa ukifika
 
Hapo nina mashaka kuna mambo ya 10% yanahusika...
 
Back
Top Bottom