Kampuni ya Reli Tanzania(TRL) yavikana vichwa vya Treni, yataka virudishwe vilipotoka

Kampuni ya Reli Tanzania(TRL) yavikana vichwa vya Treni, yataka virudishwe vilipotoka

Tusubiri mtu kutumbuliwa kwa kiki

Mkuu,
Hatari sana hawa vigogo, Sifa moja ya CEO, Mkurugenzi Mkuu, Mkurugenzi Mtendaji ni kuwa na taarifa zote sahihi katika meza yako + kujiamini, sasa huyu jamaa kumwambia Mh. Rais kuwa vichwa vya treni havina mwenyewe na Rais akamuamini na kutangazia taifa kuwa amegundua ''mali ya mamilioni'' ikiwa bandarini bila kuwa na mwenyewe hii ni kashfa kubwa.

Mzigo huu wa vichwa vya treni vyenye thamani ya mamilioni toka 2015 http://www.mwananchi.co.tz/habari/-Vichwa-vya-treni-vyaibua-utata-/1597578-3998850-13wy1ww/index.html Mkurugenzi wa TPA hana taarifa nao wala ripoti sahihi haipo ktk meza yake hii ni hatari sana kwa shirika letu la umma. Nashauri ma-CEO wafuate utendaji wa staili ya MBWA (Management by Wandering Around, or MBWA) waachane na kujifungia ofisini.
 
Sasa ilikuwaje TPA wakakubali kushushwa kwa kitu ambacho mmiliki hajatajwa kwenye bill of landing

Ukirudi kwa shipper atakuwmbia Consignee ni nani.

Ukienda kwa mwenye vessel ( maersk, cma, Msc, ) ukaomba PL , CI, DN lazima tu utamjua owner .

BOL, INvoice , MBL zote zina majibu
 
Nimetafakari sana maelezo ya Kakoko nikakumbuka zile tambo za juzi kwamba tumekamata vichwa vya treni ambavyo havina mwenyewe. Nikajiuliza lengo la tambo zile lilikua nini? Kama Kakoko alijua vichwa ni vya TRL ilikuaje "mwenye nyumba" akasema havina mwenyewe? Hakumuuliza Kakoko? Alidanganywa? Alijua ukweli lakini akatupotosha? Ili iweje? Kwa faida ya nani?
Tambo zimetoka wapi?alichofanya Rais ni kuonesha mshangao,kuwa kuna vichwa havina mwenyewe,akaamuru uchunguzi ufanyike.
TRL walitaka kupiga dili waliivyoona limebumbuluka wakakimbia mzigo kama unavyokimbiwa mzigo wa meno ya tembo
 
Na wewe umekosea ni BILL OF LOADING
Wacha kutia aibu wewe!"bill of lading" ndio sahihi na ukiendelea kubisha tutakutaka itutafsirie bill of loading nasi tutakusomesha bill of lading na inafanyaje kazi katika shopment na inventory zake!
 
Mkuu,
Hatari sana hawa vigogo, Sifa moja ya CEO, Mkurugenzi Mkuu, Mkurugenzi Mtendaji ni kuwa na taarifa zote sahihi katika meza yako + kujiamini, sasa huyu jamaa kumwambia Mh. Rais kuwa vichwa vya treni havina mwenyewe na Rais akamuamini na kutangazia taifa kuwa amegundua ''mali ya mamilioni'' ikiwa bandarini bila kuwa na mwenyewe hii ni kashfa kubwa.

Mzigo huu wa vichwa vya treni vyenye thamani ya mamilioni toka 2015http://www.mwananchi.co.tz/habari/-Vichwa-vya-treni-vyaibua-utata-/1597578-3998850-13wy1ww/index.html Mkurugenzi wa TPA hana taarifa nao wala ripoti sahihi haipo ktk meza yake hii ni hatari sana kwa shirika letu la umma.
Ni hatari sana kwa Taifa
 
Tambo zimetoka wapi?alichofanya Rais ni kuonesha mshangao,kuwa kuna vichwa havina mwenyewe,akaamuru uchunguzi ufanyike.
TRL walitaka kupiga dili waliivyoona limebumbuluka wakakimbia mzigo kama unavyokimbiwa mzigo wa meno ya tembo
Unadhani Rais hakuwa na taarifa sahihi wakati anaongea??
 
Mbona rahisi sana hii
MTU AWAITE WATENGENEZAJI,WASAFIRISHAJI WAJE WATUAMBIE VIMETOKA WAPI NA VINAKWENDA KWA NANI
Ile bill of Lading inaeleza yote hayo maana ni mkataba kati ya msafirishaji na mtengenezaju au muuzaji inaeleza ni mzigo gani kwa idadi au kiasi gani na unakwenda wapi na kwa nani!
 
Kuna wakati Mzungu aliwahi kusema hakuna bandari nzuri kama Dar es Salaam. Sasa wakati muafaka kuweka heshima ya bandari yetu hata kama kuna wachache walijinufaisha wawekwe hadharani.

Mh. waziri aunde tume kuchunguza hayo mabehewa na vichwa chake Watanzania wajiridhishe ni vya nani.

Natanguliza shukrani!

[HASHTAG]#tmtanzaniakwanza[/HASHTAG]
 
cf969d6e1bb3064bac4cd3b52a42b0ec.jpg

View attachment 535327
KAMPUNI ya Reli Tanzania (TRL) imekanusha kuhusika na vichwa 11 vilivyoshushwa na kutelekezwa katika Bandari ya Dar es Salaam hivi karibuni. Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Deusdedit Kakoko, vichwa hivyo vilivyoshushwa na meli ya Mesina Line tangu wiki iliyopita, na kwamba ni mali ya TRL.

Akizungumza na gazeti hili Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo, Masanja Kadogosa alisema TRL haihusiki kwa namna yoyote na vichwa hivyo kwa kuwa hakuna taarifa zozote zinahusu uagizwaji wake.

Alisema pia kwa mujibu wa Sheria ya Manunuzi, kampuni hiyo inapofanya manunuzi yoyote lazima kuwepo na mkataba wa makubaliano na kampuni husika inayouza bidhaa, lakini haina mkataba wowote unaohusu ununuzi wa vichwa hivyo.

Alieleza kuwa taratibu za manunuzi zinafahamika kwani endapo kampuni hiyo ingeagiza vichwa hivyo ingetakiwa kupeleka mtu wake kwa ajili ya ukaguzi wakati vinatengenezwa na mara baada ya kutengenezwa kabla ya kupakiwa kwenye meli. “Lakini hiyo kitu hakuna, hatukuwa na watu wetu kwa kuwa si mali yetu,” alieleza.

Pamoja na hayo, alisema ili mzigo wowote umfikie mhusika lazima kuwepo na nyaraka ya kutolea mzigo bandarini ambayo pia huwa na makubaliano mengine baina ya mnunuzi na muuzaji ambayo katika sakata hilo, TRL wamesisitiza hawana nyaraka hiyo.

Alisema TRL haivitambui vichwa hivyo kwa kuwa si mali yake. “Hivi ni vichwa vikubwa sasa kwanini tuvikatae kama ni vyetu, ila ukweli ni kwamba hatuvitambui kabisa,” alieleza mkuu huyo wa reli nchini.

Juzi wakati akizundua Mradi wa Uboreshaji wa Bandari ya Dar es Salaam (DSMGP), Rais John Magufuli aliibua hoja hiyo ya vichwa vya treni kushushwa bandarini na kutekelezwa bila kuwa na mwenyewe na kuitaka TPA pamoja na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, kufuatilia kwa kina suala hilo.

Dk Magufuli alisema anazo taarifa za kushushwa kwa vichwa vya treni takribani 15 katika bandari hiyo, ambavyo mmiliki wake hafahamiki na meli iliyovileta imeshaondoka. Hata hivyo, mkurugenzi wa mamlaka hiyo ya TPA Kakoko pamoja na kuthibitisha kushushwa kwa vichwa hivyo kutoka kwa meli ya Mesina Line, iliyobeba mzigo huo kutoka kwa Komazi Trading Co, alibainisha wazi kuwa vichwa hivyo ni vya TRL.

Alisema vichwa hivyo ni awamu ya pili iliyoagizwa tangu serikali ya awamu ya nne miaka mitatu iliyopita, ambapo awamu ya kwanza ilishaletwa na vichwa vyake kuchukuliwa na hadi leo vinatumiwa na TRL.

Alifafanua kuwa baada ya uchunguzi wa TPA ilibaini kuwa kuna mgogoro unaoendelea kati ya TRL na kampuni ya Komazi na kwamba TRL ilishagoma kuvichukua vichwa hivyo lakini suala hilo, halikutaarifiwa kwa TPA

Chanzo: Habari leo

My Take:

Kama hawavitaki wamgawie Askofu Gwajima wa ufufo na Uzima kwani anatafuta vichwa Treni.

Hivi vichwa si ndio aliagizaga Mwakyembe kipindi yupo wizara ya uchukuzi au?? Washukuru mheshimiwa Rais kachoka kutumbua...
 
Tume ya nini wakati documents zina details za kutosha.
 
!
!
Huku wanaume wanaona, kule kuna majambazi sijui Ugadi sijui ujinga gani, huku polisi wana haha na chadema, kule kuna vichwa vya treni havina mwenyewe khaaaa
Huku tunasubiri matrilioni ya makinikia. Na pia mashehe wa uamsho wanahusika na mauaji ya kibiti
Kwa jinsi nchi ilivyo na mauzauza hata hizi bomberdia iko siku tutakuja kuzikataa
 
wakivikataa tuviyeyushe chuma chakavu, au vigeuzwe mashine za kuzalisha umeme ambako haujafika
 
Back
Top Bottom