Kampuni ya Reli Tanzania(TRL) yavikana vichwa vya Treni, yataka virudishwe vilipotoka

Kampuni ya Reli Tanzania(TRL) yavikana vichwa vya Treni, yataka virudishwe vilipotoka

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari nchini, Engineer Deusdedit Kakoko amesema vichwa vya treni vinavyodaiwa kutelekezwa bandarini ni mali ya shirika la Reli nchini TRL na kwamba vina nembo ya TRL (Tanzania Railway Limited). Kakoko amesema TRL walinunua vichwa hivyo bila kufuata utaratibu kutoka kampuni ya EMD ya nchini Marekani, lakini vimetengenezwa na kampuni ya DCD ya nchini Afrika Kusini.

Maelezo ya Kakoko yanahitimisha taarifa "zilizovumishwa" hivi karibuni kuwa vichwa hivyo havina mwenyewe. Kwa lugha rahisi ni kwamba Engineer Kakoko amesema SI KWELI kwamba vichwa hivyo havina mwenyewe. Kakoko anasema ni vya TRL na vina nembo ya TRL.

Source:
Mmiliki wa vichwa 13 vya treni bandarini afahamika

MyTake:
Nimetafakari sana maelezo ya Kakoko nikakumbuka zile tambo za juzi kwamba tumekamata vichwa vya treni ambavyo havina mwenyewe. Nikajiuliza lengo la tambo zile lilikua nini? Kama Kakoko alijua vichwa ni vya TRL ilikuaje "mwenye nyumba" akasema havina mwenyewe? Hakumuuliza Kakoko? Alidanganywa? Alijua ukweli lakini akatupotosha? Ili iweje? Kwa faida ya nani?

Kwani angesema ni vya TRL lakini vilinunuliwa bila kufuata utaratibu kungekua na tatizo gani? Kwanini aseme uongo kuwa havina mwenyewe wakati vina nembo ya TRL? Ina maana hakuona hata nembo? Au hiyo nembo iliwekwa baada ya "mwenye nyumba" kuondoka? Anyway tuendelee kumuombea.!!

Vichwa visivyojulijana ni vya nani vilivyopo bandarini
View attachment 535375

Treni ya TRL ikiwa kazini,hapo ilikua maeneo ya Dodoma. Hata kama tunadanganywa ila sasa imezidi

Kwa ushahidi huu, hiyo picha ya hapo juu ni ya vichwa vya awamu ya kwanza vile viwili na si hii iliyosemwa sasa ya kumi na tatu. Registration 9001 na 9002 haiwezekani kurudiwa tena.
 
wawe makini yasije kuwa ni mabomu ya ya hatari tumeletewa.
 
Mkuu nakubaliana na wewe.

Wanachosahau ni kuwa kama vichwa viliagizwa na TRL hata kama ni management ya zamani, bado ni mali ya TRL.

Nadhani huyu Mkurugenzi mkuu anasahau kuwa TRL ni taasisi, hivyo anatakiwa kuheshimu mikataba iliyoingiwa na watangulizi wake hata kama yeye binafsi hakubaliani nayo.

hakuna mkataba mkuu
 
Nimewapigia kuwaarifu vichwa 15 vya treni vimeunguka bandararini Dar kutoka meli mesina. Tafadhali fanyeni haraka taratibu ya kuvichukua.
Ecellent work mkuu [emoji122] [emoji122] [emoji122] Hii ni era ya kidigitali. Hakuna haja ya kusafiri safiri angani Korea ya kaskazini wanatest makitu yao ya masafa marefu.
 
December 7, 2014
Dar-es-Salaam, Tanzania

Taarifa: Mabehewa 72 na kusubiri vichwa 13 vya Treni
Waziri wa Uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe amepokea mabehewa 50 ya kubebea mizigo na mengine 22 kwa ajili ya abiria.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam Dk. Mwakyembe alisema kupokelewa kwa mabehewa kumefanya idadi kufikia 100 kati ya 274.

Alisema ifikapo mwakani 2015 kutakuwa na mabadiliko makubwa katika njia ya reli ya kati kwani tayari wameshaanza kukifanyia kazi suala hilo ikiwa ni sehemu ya kuimarisha usafiri huo nchini.

Waziri alisema mbali na mabehewa hayo kuna vifaa vingine vitawasili hivi karibuni hapa nchini na vichwa vipya 13 vya treni ambavyo vitasaidia kuongeza kasi ya utendaji kazi.

Dk.Mwakyembe alisema usafiri wa treni utakapoimarishwa kampuni ya Reli nchini (TRL) itaanza kujiendesha bila kutegemea fedha toka serikalini.

Aliongeza kuwa idadi ya mabehewa 274 yanaletwa kutoka Korea ya kusini na yamegharimu zaidi ya Sh. bilion 200.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa TRL, Mhandisi Kipallo Kisamfu alisema mabehewa hayo yanatarajia kuanza safari zake kwa abiria ifikapo Januari mwakani na kwamba itakuwa ikielekea mikoa ya Kigoma na Mwanza.

Alisema kupokelewa kwa mabehewa hayo kutaongeza uwezo wa kampuni katika kusafirisha mizigo kwa njia ya reli kwenda maeneo mbalimbali.

Source: Mwakyembe apokea mabehewa 72 | KILI FM Radio 87.5
 
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari nchini, Engineer Deusdedit Kakoko amesema vichwa vya treni vinavyodaiwa kutelekezwa bandarini ni mali ya shirika la Reli nchini TRL na kwamba vina nembo ya TRL (Tanzania Railway Limited). Kakoko amesema TRL walinunua vichwa hivyo bila kufuata utaratibu kutoka kampuni ya EMD ya nchini Marekani, lakini vimetengenezwa na kampuni ya DCD ya nchini Afrika Kusini.

Maelezo ya Kakoko yanahitimisha taarifa "zilizovumishwa" hivi karibuni kuwa vichwa hivyo havina mwenyewe. Kwa lugha rahisi ni kwamba Engineer Kakoko amesema SI KWELI kwamba vichwa hivyo havina mwenyewe. Kakoko anasema ni vya TRL na vina nembo ya TRL.

Source:
Mmiliki wa vichwa 13 vya treni bandarini afahamika

MyTake:
Nimetafakari sana maelezo ya Kakoko nikakumbuka zile tambo za juzi kwamba tumekamata vichwa vya treni ambavyo havina mwenyewe. Nikajiuliza lengo la tambo zile lilikua nini? Kama Kakoko alijua vichwa ni vya TRL ilikuaje "mwenye nyumba" akasema havina mwenyewe? Hakumuuliza Kakoko? Alidanganywa? Alijua ukweli lakini akatupotosha? Ili iweje? Kwa faida ya nani?

Kwani angesema ni vya TRL lakini vilinunuliwa bila kufuata utaratibu kungekua na tatizo gani? Kwanini aseme uongo kuwa havina mwenyewe wakati vina nembo ya TRL? Ina maana hakuona hata nembo? Au hiyo nembo iliwekwa baada ya "mwenye nyumba" kuondoka? Anyway tuendelee kumuombea.!!

Vichwa visivyojulijana ni vya nani vilivyopo bandarini
View attachment 535375

Treni ya TRL ikiwa kazini,hapo ilikua maeneo ya Dodoma. Hata kama tunadanganywa ila sasa imezidi


ILA TUNAPENDA KUHUSISHA VITU VISIVYO NA UHUSIANO, UMEWEKA HIVYO VICHWA AMBAVYO VIMELETWA TOKA 2015 KUJA KUELEZEA KITU AMBACHO UMEAMBIWA VIMESHUSHWA WIKI MBILI ZILIZOPITA. SOMA HII LINK NA ULINGANISHE NA PICHA UNAYOIHUSISHA YA VICHWA VISIVYOJULIKANA VYA NANI VILIVYOSHUSHWA WIKI MBILI ZILIZOPITA

Vichwa viwili kati ya vichwa 13 vya treni vilivyonunuliwa na TRL
unnamed.jpgs.jpg
Machi 21, 2015 tumeshuhudia tukio muhimu sana kwa TRL kupokea sehemu ya vichwa vipya vya treni vilivyoagizwa kutoka nje ya Nchi. Tumepokea vichwa viwili (2) kati ya vichwa kumi na tatu (13) vya treni vilivyonunuliwa


TRL YAPOKEA VICHWA 2 VYA TRENI TOKA AFRIKA KUSINI | Magazeti ya leo| Tanzania News |Tanzania Today
 
Kama vya njia ya umeme mnigawie niviendeleze inakuaje havina mwenyewe ivi ule wimbo wa Taifa kuna beti ina sema wageni karibuni kutazama maajabu biashara na makazi kweli haya nimaajabu wageni karibu mtazame vichwa vya treni havina mwenyewe vimeshushwa kutoka mbinguni[emoji23][emoji23][emoji22]
 
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari nchini, Engineer Deusdedit Kakoko amesema vichwa vya treni vinavyodaiwa kutelekezwa bandarini ni mali ya shirika la Reli nchini TRL na kwamba vina nembo ya TRL (Tanzania Railway Limited). Kakoko amesema TRL walinunua vichwa hivyo bila kufuata utaratibu kutoka kampuni ya EMD ya nchini Marekani, lakini vimetengenezwa na kampuni ya DCD ya nchini Afrika Kusini.

Maelezo ya Kakoko yanahitimisha taarifa "zilizovumishwa" hivi karibuni kuwa vichwa hivyo havina mwenyewe. Kwa lugha rahisi ni kwamba Engineer Kakoko amesema SI KWELI kwamba vichwa hivyo havina mwenyewe. Kakoko anasema ni vya TRL na vina nembo ya TRL.

Source:
Mmiliki wa vichwa 13 vya treni bandarini afahamika

MyTake:
Nimetafakari sana maelezo ya Kakoko nikakumbuka zile tambo za juzi kwamba tumekamata vichwa vya treni ambavyo havina mwenyewe. Nikajiuliza lengo la tambo zile lilikua nini? Kama Kakoko alijua vichwa ni vya TRL ilikuaje "mwenye nyumba" akasema havina mwenyewe? Hakumuuliza Kakoko? Alidanganywa? Alijua ukweli lakini akatupotosha? Ili iweje? Kwa faida ya nani?

Kwani angesema ni vya TRL lakini vilinunuliwa bila kufuata utaratibu kungekua na tatizo gani? Kwanini aseme uongo kuwa havina mwenyewe wakati vina nembo ya TRL? Ina maana hakuona hata nembo? Au hiyo nembo iliwekwa baada ya "mwenye nyumba" kuondoka? Anyway tuendelee kumuombea.!!

Vichwa visivyojulijana ni vya nani vilivyopo bandarini
View attachment 535375

Treni ya TRL ikiwa kazini,hapo ilikua maeneo ya Dodoma. Hata kama tunadanganywa ila sasa imezidi

Kuna kitu kinafichwa hapa.
 
hakuna mkataba mkuu

Mkuu itakuwa ni maajabu makubwa sana kama kampuni kubwa na yenye uwezo wa ku-supply mitambo mikubwa kama hiyo itatengenza na kusafirisha vichwa 13 vya treni bila mkataba.

Muda tu ndiyo utatuambia ukweli.
 
Ukiona thread kama hizi, nakumbuka wale wakemya wanalia lia watanzania wakiwawekea habari za Tanzania hapa, utasikia "huu ni uwanja wa Kenya kwanini mnaweka habari za Tanzania" Haya sasa, ndugu yemu huyu hapa kawawekea habari ya Tanzania, njoni mjadili kwa kurefu.

Hehehe wewe siku hizi umefulia, umeishiwa na hoja kiasi kwamba kwa kila mada unatafuta pa kutokea, hivi mnanunua vichwa vya treni kama karanga. Halafu they are very ugly ndio maana mumevikimbia.
 
cf969d6e1bb3064bac4cd3b52a42b0ec.jpg

View attachment 535327
KAMPUNI ya Reli Tanzania (TRL) imekanusha kuhusika na vichwa 11 vilivyoshushwa na kutelekezwa katika Bandari ya Dar es Salaam hivi karibuni. Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Deusdedit Kakoko, vichwa hivyo vilivyoshushwa na meli ya Mesina Line tangu wiki iliyopita, na kwamba ni mali ya TRL.

Akizungumza na gazeti hili Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo, Masanja Kadogosa alisema TRL haihusiki kwa namna yoyote na vichwa hivyo kwa kuwa hakuna taarifa zozote zinahusu uagizwaji wake.

Alisema pia kwa mujibu wa Sheria ya Manunuzi, kampuni hiyo inapofanya manunuzi yoyote lazima kuwepo na mkataba wa makubaliano na kampuni husika inayouza bidhaa, lakini haina mkataba wowote unaohusu ununuzi wa vichwa hivyo.

Alieleza kuwa taratibu za manunuzi zinafahamika kwani endapo kampuni hiyo ingeagiza vichwa hivyo ingetakiwa kupeleka mtu wake kwa ajili ya ukaguzi wakati vinatengenezwa na mara baada ya kutengenezwa kabla ya kupakiwa kwenye meli. “Lakini hiyo kitu hakuna, hatukuwa na watu wetu kwa kuwa si mali yetu,” alieleza.

Pamoja na hayo, alisema ili mzigo wowote umfikie mhusika lazima kuwepo na nyaraka ya kutolea mzigo bandarini ambayo pia huwa na makubaliano mengine baina ya mnunuzi na muuzaji ambayo katika sakata hilo, TRL wamesisitiza hawana nyaraka hiyo.

Alisema TRL haivitambui vichwa hivyo kwa kuwa si mali yake. “Hivi ni vichwa vikubwa sasa kwanini tuvikatae kama ni vyetu, ila ukweli ni kwamba hatuvitambui kabisa,” alieleza mkuu huyo wa reli nchini.

Juzi wakati akizundua Mradi wa Uboreshaji wa Bandari ya Dar es Salaam (DSMGP), Rais John Magufuli aliibua hoja hiyo ya vichwa vya treni kushushwa bandarini na kutekelezwa bila kuwa na mwenyewe na kuitaka TPA pamoja na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, kufuatilia kwa kina suala hilo.

Dk Magufuli alisema anazo taarifa za kushushwa kwa vichwa vya treni takribani 15 katika bandari hiyo, ambavyo mmiliki wake hafahamiki na meli iliyovileta imeshaondoka. Hata hivyo, mkurugenzi wa mamlaka hiyo ya TPA Kakoko pamoja na kuthibitisha kushushwa kwa vichwa hivyo kutoka kwa meli ya Mesina Line, iliyobeba mzigo huo kutoka kwa Komazi Trading Co, alibainisha wazi kuwa vichwa hivyo ni vya TRL.

Alisema vichwa hivyo ni awamu ya pili iliyoagizwa tangu serikali ya awamu ya nne miaka mitatu iliyopita, ambapo awamu ya kwanza ilishaletwa na vichwa vyake kuchukuliwa na hadi leo vinatumiwa na TRL.

Alifafanua kuwa baada ya uchunguzi wa TPA ilibaini kuwa kuna mgogoro unaoendelea kati ya TRL na kampuni ya Komazi na kwamba TRL ilishagoma kuvichukua vichwa hivyo lakini suala hilo, halikutaarifiwa kwa TPA

Chanzo: Habari leo

My Take:

Kama hawavitaki wamgawie Askofu Gwajima wa ufufuo na Uzima kwani anatafuta vichwa Treni.


Jamaa anapenda sifa ka Herode anataka kila siku asifiwe na watu na kupigiwa makofi. anatafuta kuandikwa wenye fenti page za magazeti
 
Wamevikataa kwa kuwa waliagiza bila ya kuwa na Mkataba nao then bikishafika ndio watengeneze Mkataba wa back date tarehe kuonesha Mkataba ulianza kabla ya kuagiza

Hawakutegemea kuwa JPM angekagua Bandari hivi karibuni, kukiri maana yake ni kuagiza kienyeji hali ambayo ingepelekea Kufukuzwa kazi na kupigwa kitu cha Miney laundering na uhujumu Uchumi
Haya yote shida kwetu sasa .vichwa vimeshalipiwa kuchukua hamtaki shauri ya siasa za ndani .wameona dawa nikuwatupia treni zenu hapo mchukue imsichukue shauri yenu.kama ni ukaguzi fanyieni msifanye shauri yenu.
 
ILA TUNAPENDA KUHUSISHA VITU VISIVYO NA UHUSIANO, UMEWEKA HIVYO VICHWA AMBAVYO VIMELETWA TOKA 2015 KUJA KUELEZEA KITU AMBACHO UMEAMBIWA VIMESHUSHWA WIKI MBILI ZILIZOPITA. SOMA HII LINK NA ULINGANISHE NA PICHA UNAYOIHUSISHA YA VICHWA VISIVYOJULIKANA VYA NANI VILIVYOSHUSHWA WIKI MBILI ZILIZOPITA

Vichwa viwili kati ya vichwa 13 vya treni vilivyonunuliwa na TRL
unnamed.jpgs.jpg
Machi 21, 2015 tumeshuhudia tukio muhimu sana kwa TRL kupokea sehemu ya vichwa vipya vya treni vilivyoagizwa kutoka nje ya Nchi. Tumepokea vichwa viwili (2) kati ya vichwa kumi na tatu (13) vya treni vilivyonunuliwa


TRL YAPOKEA VICHWA 2 VYA TRENI TOKA AFRIKA KUSINI | Magazeti ya leo| Tanzania News |Tanzania Today
Kama hichi ulichoandika hapa unakiamini basi nina imani unaamini kuwa hivyo vichwa vilivyoshushwa juzi ni vya TRL, waangalie makabrasha yao vizuri

Sent from my LG-D955 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom