Mchosis
JF-Expert Member
- Oct 25, 2012
- 247
- 66
Mjinga ni wewe na huyo muagizaji asiyejulikana. heshimu wenzako!
Sasa si wavitumie ujue sisi ni wajinga sana[/QUOTE}
Sasa si wavitumie ujue sisi ni wajinga sana[/QUOTE}
Hata kama mikataba ni ya kilofa akubaliane tu?hakuna mkataba mkuu
Ndugu usishangae. Naona tunaanza kurudi kwenye enzi za wana wa Izraeli walipokuwa wanashushiwa mikate (mana). Hivyo tusishangae kuona tunashushiwa vichwa vya treni. Ni jambo la kushukuru piaKwa nini Sirro asikamate hawa watu wakaisaidie police ''wakiwa kureee ndani''? Yaani vichwa vikubwa hivyo vinapotea njia na kuibukia Darisalama kweli? ama kweli maajabu hayatokaa yaishe Nchi hii.
Hao si ndio wale wale wanaopinga kila kitu. Yaani athari za serikali zilizopita kutunyima elimu, ndio tunaona matokeo yake kwenye mawazo ya watu kama hawaHata kama mikataba ni ya kilofa akubaliane tu?
Tatizo la shamba la bibi kila mtu ana mamlaka ya kupanda na kuvuna apendacho hata kama hali ya hewa na udongo haviruhusu. Ili mradi uonekane umelima.
Si ndio hapo. Wanajitapa humu halafu wakati wa uchaguzi 'wakishapewa ...........' wanasahau hizi kauli😛Sharif kwani kura yako ni turufu??
Nchi kumbe inaweza tekwa kupitia bandari yetu. Kama vichwa vya treni vinaingia then hatujui muingizani then tunasema nchi ina usalama?
Ndugu yangu, hzi sanaa za serikali hii utaziweza? Kila mtu sasa hivi anaogopa. Hapa kuna ujinga wa ajabu unaendelea. Nina hakika TPA kabla ya kushusha walijiridhisha na documents, hata kama zilikuwa zimeghushiwa lakini nina hakika documents za mzigo zilikuwepo. Ila sarakasi inayoendelea kati ya TRL na hao waliowatengenezea ndiyo inasababisha sintofahamu hiyo. TRL watatueleza vizuri imekuwaje mzigo ukashushwa "nyumbani" kama walishakataa order isiendelee kutengenezwa.Sasa ilikuwaje TPA wakakubali kushushwa kwa kitu ambacho mmiliki hajatajwa kwenye bill of landing
Hilo ndio swali la msingi.Mimi najiuliza tu ni nani alivilipia?
MwakyembeeeeeeHapo kuna waziri wa ccm lazima anahusika kuagiza
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari nchini, Engineer Deusdedit Kakoko amesema vichwa vya treni vinavyodaiwa kutelekezwa bandarini ni mali ya shirika la Reli nchini TRL na kwamba vina nembo ya TRL (Tanzania Railway Limited). Kakoko amesema TRL walinunua vichwa hivyo bila kufuata utaratibu kutoka kampuni ya EMD ya nchini Marekani, lakini vimetengenezwa na kampuni ya DCD ya nchini Afrika Kusini.
Maelezo ya Kakoko yanahitimisha taarifa "zilizovumishwa" hivi karibuni kuwa vichwa hivyo havina mwenyewe. Kwa lugha rahisi ni kwamba Engineer Kakoko amesema SI KWELI kwamba vichwa hivyo havina mwenyewe. Kakoko anasema ni vya TRL na vina nembo ya TRL.
Source:
Mmiliki wa vichwa 13 vya treni bandarini afahamika
MyTake:
Nimetafakari sana maelezo ya Kakoko nikakumbuka zile tambo za juzi kwamba tumekamata vichwa vya treni ambavyo havina mwenyewe. Nikajiuliza lengo la tambo zile lilikua nini? Kama Kakoko alijua vichwa ni vya TRL ilikuaje "mwenye nyumba" akasema havina mwenyewe? Hakumuuliza Kakoko? Alidanganywa? Alijua ukweli lakini akatupotosha? Ili iweje? Kwa faida ya nani?
Kwani angesema ni vya TRL lakini vilinunuliwa bila kufuata utaratibu kungekua na tatizo gani? Kwanini aseme uongo kuwa havina mwenyewe wakati vina nembo ya TRL? Ina maana hakuona hata nembo? Au hiyo nembo iliwekwa baada ya "mwenye nyumba" kuondoka? Anyway tuendelee kumuombea.!!
Vichwa visivyojulijana ni vya nani vilivyopo bandarini
View attachment 535375
Treni ya TRL ikiwa kazini,hapo ilikua maeneo ya Dodoma. Hata kama tunadanganywa ila sasa imezidi
Rais anajua kinachoendelea.Aliposema havina mwenyewe,alijua TRL watavikataa.Mbona the alphabets T,R ana L aliziona.Jamani hivi walioviandika TRL ni mataahira?Hata hivyo kwa kuwa manufacturers wanafahamika,ni rahisi ku-trace back na kujua nani aliagiza.![]()
View attachment 535327
KAMPUNI ya Reli Tanzania (TRL) imekanusha kuhusika na vichwa 11 vilivyoshushwa na kutelekezwa katika Bandari ya Dar es Salaam hivi karibuni. Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Deusdedit Kakoko, vichwa hivyo vilivyoshushwa na meli ya Mesina Line tangu wiki iliyopita, na kwamba ni mali ya TRL.
Akizungumza na gazeti hili Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo, Masanja Kadogosa alisema TRL haihusiki kwa namna yoyote na vichwa hivyo kwa kuwa hakuna taarifa zozote zinahusu uagizwaji wake.
Alisema pia kwa mujibu wa Sheria ya Manunuzi, kampuni hiyo inapofanya manunuzi yoyote lazima kuwepo na mkataba wa makubaliano na kampuni husika inayouza bidhaa, lakini haina mkataba wowote unaohusu ununuzi wa vichwa hivyo.
Alieleza kuwa taratibu za manunuzi zinafahamika kwani endapo kampuni hiyo ingeagiza vichwa hivyo ingetakiwa kupeleka mtu wake kwa ajili ya ukaguzi wakati vinatengenezwa na mara baada ya kutengenezwa kabla ya kupakiwa kwenye meli. “Lakini hiyo kitu hakuna, hatukuwa na watu wetu kwa kuwa si mali yetu,” alieleza.
Pamoja na hayo, alisema ili mzigo wowote umfikie mhusika lazima kuwepo na nyaraka ya kutolea mzigo bandarini ambayo pia huwa na makubaliano mengine baina ya mnunuzi na muuzaji ambayo katika sakata hilo, TRL wamesisitiza hawana nyaraka hiyo.
Alisema TRL haivitambui vichwa hivyo kwa kuwa si mali yake. “Hivi ni vichwa vikubwa sasa kwanini tuvikatae kama ni vyetu, ila ukweli ni kwamba hatuvitambui kabisa,” alieleza mkuu huyo wa reli nchini.
Juzi wakati akizundua Mradi wa Uboreshaji wa Bandari ya Dar es Salaam (DSMGP), Rais John Magufuli aliibua hoja hiyo ya vichwa vya treni kushushwa bandarini na kutekelezwa bila kuwa na mwenyewe na kuitaka TPA pamoja na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, kufuatilia kwa kina suala hilo.
Dk Magufuli alisema anazo taarifa za kushushwa kwa vichwa vya treni takribani 15 katika bandari hiyo, ambavyo mmiliki wake hafahamiki na meli iliyovileta imeshaondoka. Hata hivyo, mkurugenzi wa mamlaka hiyo ya TPA Kakoko pamoja na kuthibitisha kushushwa kwa vichwa hivyo kutoka kwa meli ya Mesina Line, iliyobeba mzigo huo kutoka kwa Komazi Trading Co, alibainisha wazi kuwa vichwa hivyo ni vya TRL.
Alisema vichwa hivyo ni awamu ya pili iliyoagizwa tangu serikali ya awamu ya nne miaka mitatu iliyopita, ambapo awamu ya kwanza ilishaletwa na vichwa vyake kuchukuliwa na hadi leo vinatumiwa na TRL.
Alifafanua kuwa baada ya uchunguzi wa TPA ilibaini kuwa kuna mgogoro unaoendelea kati ya TRL na kampuni ya Komazi na kwamba TRL ilishagoma kuvichukua vichwa hivyo lakini suala hilo, halikutaarifiwa kwa TPA
Chanzo: Habari leo
My Take:
Kama hawavitaki wamgawie Askofu Gwajima wa ufufuo na Uzima kwani anatafuta vichwa Treni.
PppupppoppiNimeipenda sentensi yako ya mwisho, "Tuendelee kumuombea", ukweli kabisa hakuna njia nyingine yeyote inayoweza kuliokoa hili taifa zaidi ya maombi. Hata nchi ya Kusadikika naona ilikuwa na unafuu ukilinganisha na hapa kwetu.
Nimeipenda sentensi yako ya mwisho, "Tuendelee kumuombea", ukweli kabisa hakuna njia nyingine yeyote inayoweza kuliokoa hili taifa zaidi ya maombi. Hata nchi ya Kusadikika naona ilikuwa na unafuu ukilinganisha na hapa kwetu.
😀 wa Shaggy nn?Kuna wimbo unaitwa " It wasn't me".
Nimeukumbuka ghafla.😀😀😀