Kampuni ya Reli Tanzania(TRL) yavikana vichwa vya Treni, yataka virudishwe vilipotoka

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari nchini, Engineer Deusdedit Kakoko amesema vichwa vya treni vinavyodaiwa kutelekezwa bandarini ni mali ya shirika la Reli nchini TRL na kwamba vina nembo ya TRL (Tanzania Railway Limited). Kakoko amesema TRL walinunua vichwa hivyo bila kufuata utaratibu kutoka kampuni ya EMD ya nchini Marekani, lakini vimetengenezwa na kampuni ya DCD ya nchini Afrika Kusini.

Maelezo ya Kakoko yanahitimisha taarifa "zilizovumishwa" hivi karibuni kuwa vichwa hivyo havina mwenyewe. Kwa lugha rahisi ni kwamba Engineer Kakoko amesema SI KWELI kwamba vichwa hivyo havina mwenyewe. Kakoko anasema ni vya TRL na vina nembo ya TRL.

Source:
Mmiliki wa vichwa 13 vya treni bandarini afahamika

MyTake:
Nimetafakari sana maelezo ya Kakoko nikakumbuka zile tambo za juzi kwamba tumekamata vichwa vya treni ambavyo havina mwenyewe. Nikajiuliza lengo la tambo zile lilikua nini? Kama Kakoko alijua vichwa ni vya TRL ilikuaje "mwenye nyumba" akasema havina mwenyewe? Hakumuuliza Kakoko? Alidanganywa? Alijua ukweli lakini akatupotosha? Ili iweje? Kwa faida ya nani?

Kwani angesema ni vya TRL lakini vilinunuliwa bila kufuata utaratibu kungekua na tatizo gani? Kwanini aseme uongo kuwa havina mwenyewe wakati vina nembo ya TRL? Ina maana hakuona hata nembo? Au hiyo nembo iliwekwa baada ya "mwenye nyumba" kuondoka? Anyway tuendelee kumuombea.!!
Kuwa na nembo sio utambulisho wa umiliki wa asset yoyote bali nyaraka zinazohamisha umiliki husika. Kwani kila gari yenye nembo ya Toyota ni mali ya Toyota?, maelezo yako wazi kuwa utaratibu wa kuvinunua haukua sawa thts y Rais hajui.....
 
Inaelekea unajifunza kuandika
1 mkuu unatoa povu sana kunywa maji kidogo..
Kiki zinamwisho ila mwisho wa hii kick ni mbaya zaidi...mwambieni uyo mzee wa kaya aache kuropoka ropoka
Pale alikua anatafuta platform ya kumuongelea lowassa.
 
Kuwa na nembo sio utambulisho wa umiliki wa asset yoyote bali nyaraka zinazohamisha umiliki husika. Kwani kila gari yenye nembo ya Toyota ni mali ya Toyota?, maelezo yako wazi kuwa utaratibu wa kuvinunua haukua sawa thts y Rais hajui.....
Kwaiyo unataka kutuambia kama company iliyotengeneza ivo vichwa inaitwa TRL.
Bill of loading lazima ilionesha mmiliki wa ivo vichwa au cmpny agent.
Na mkulu anajua ilo lakini katika kupendezesha story akasema amjui mmiliki. Iv bandari gani inashusha mzigo bila documents???
 
Port inatumiwa na zaidi ya nchi 7 sio mizigo yote ni mali ya Tanzania so fraudulent wanaweza kutumia mwanya huo.
 
Niliandika mapema humu kuwa walivikimbia Vichwa vyao kwa kuwa walinunua Kama unanunua Condom Dukani
 
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari nchini, Engineer Deusdedit Kakoko amesema vichwa vya treni vinavyodaiwa kutelekezwa bandarini ni mali ya shirika la Reli nchini TRL na kwamba vina nembo ya TRL (Tanzania Railway Limited). Kakoko amesema TRL walinunua vichwa hivyo bila kufuata utaratibu kutoka kampuni ya EMD ya nchini Marekani, lakini vimetengenezwa na kampuni ya DCD ya nchini Afrika Kusini.

Maelezo ya Kakoko yanahitimisha taarifa "zilizovumishwa" hivi karibuni kuwa vichwa hivyo havina mwenyewe. Kwa lugha rahisi ni kwamba Engineer Kakoko amesema SI KWELI kwamba vichwa hivyo havina mwenyewe. Kakoko anasema ni vya TRL na vina nembo ya TRL.

Source:
Mmiliki wa vichwa 13 vya treni bandarini afahamika

MyTake:
Nimetafakari sana maelezo ya Kakoko nikakumbuka zile tambo za juzi kwamba tumekamata vichwa vya treni ambavyo havina mwenyewe. Nikajiuliza lengo la tambo zile lilikua nini? Kama Kakoko alijua vichwa ni vya TRL ilikuaje "mwenye nyumba" akasema havina mwenyewe? Hakumuuliza Kakoko? Alidanganywa? Alijua ukweli lakini akatupotosha? Ili iweje? Kwa faida ya nani?

Kwani angesema ni vya TRL lakini vilinunuliwa bila kufuata utaratibu kungekua na tatizo gani? Kwanini aseme uongo kuwa havina mwenyewe wakati vina nembo ya TRL? Ina maana hakuona hata nembo? Au hiyo nembo iliwekwa baada ya "mwenye nyumba" kuondoka? Anyway tuendelee kumuombea.!!
Omba wewe sisi wengine Mungu katuzuia kuombea waropokaji.
 
TRL waliulizwa wakasema hawajasain popote kuletewa vichwa vya tren
 
Acha uchochezi! Mhe. Rais yupo Sahihi na Eng. Kakoko yupo Sahihi! Wewe hujui kama kila kitu hapa duniani kinatawaliwa na time, space, pressure & temperature? Badiliko la kimojawapo linaweza kuleta majibu tofauti!
Ni kweli kabisa mkuu, MH. Rais yuko sahihi na eng. Kakoko yuko sahihi. Yaani aliyesema 2x2 ni 4 na alisema ni 8 wote wako sawa. Asante mwalimu.
 
Ukiona thread kama hizi, nakumbuka wale wakemya wanalia lia watanzania wakiwawekea habari za Tanzania hapa, utasikia "huu ni uwanja wa Kenya kwanini mnaweka habari za Tanzania" Haya sasa, ndugu yemu huyu hapa kawawekea habari ya Tanzania, njoni mjadili kwa kurefu.
 
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari nchini, Engineer Deusdedit Kakoko amesema vichwa vya treni vinavyodaiwa kutelekezwa bandarini ni mali ya shirika la Reli nchini TRL na kwamba vina nembo ya TRL (Tanzania Railway Limited). Kakoko amesema TRL walinunua vichwa hivyo bila kufuata utaratibu kutoka kampuni ya EMD ya nchini Marekani, lakini vimetengenezwa na kampuni ya DCD ya nchini Afrika Kusini.

Maelezo ya Kakoko yanahitimisha taarifa "zilizovumishwa" hivi karibuni kuwa vichwa hivyo havina mwenyewe. Kwa lugha rahisi ni kwamba Engineer Kakoko amesema SI KWELI kwamba vichwa hivyo havina mwenyewe. Kakoko anasema ni vya TRL na vina nembo ya TRL.

Source:
Mmiliki wa vichwa 13 vya treni bandarini afahamika

MyTake:
Nimetafakari sana maelezo ya Kakoko nikakumbuka zile tambo za juzi kwamba tumekamata vichwa vya treni ambavyo havina mwenyewe. Nikajiuliza lengo la tambo zile lilikua nini? Kama Kakoko alijua vichwa ni vya TRL ilikuaje "mwenye nyumba" akasema havina mwenyewe? Hakumuuliza Kakoko? Alidanganywa? Alijua ukweli lakini akatupotosha? Ili iweje? Kwa faida ya nani?

Kwani angesema ni vya TRL lakini vilinunuliwa bila kufuata utaratibu kungekua na tatizo gani? Kwanini aseme uongo kuwa havina mwenyewe wakati vina nembo ya TRL? Ina maana hakuona hata nembo? Au hiyo nembo iliwekwa baada ya "mwenye nyumba" kuondoka? Anyway tuendelee kumuombea.!!
Anatafuta "KIKI"
 
Wana-JamiiForums tutazame picha hizi na kichwa kimoja kushoto namba 9002 picha ya kwanza tayari kinakula mzigo kama video clip hapo chini inavyo sapoti picha hizo za bandarini kuwa vichwa hivyo ni mali ya TRL kwa kichwa namba 9002 kikikatiza Dodoma na shehena ya makontena ya kutosha.

Kwa maana nyingine katika vichwa 13 visivyo na mwenyewe vichwa vingine tayari vimechukuliwa na TRL na vinafanya kazi na hivyo mzigo wote huu wa vichwa vilivyopita bandarini ni mali halali ya TRL mbali ya vile vichache alivyooneshwa Mh. Rais vilivyobaki bandarini.

pic+vichwa.jpg

Picha Source: Vichwa vya treni vyaibua utata

Tanzania Railway, Freight train タンザニア・ドドマ駅発西行き貨物列車
Freight train with 21 wagons just started from Dodoma station in Tanzania at 5:55 p.m. on June 20, Mon. 2016, near to the railroad crossing in the west of Dodoma station.

Source: Hitoshi Suzuki

c.c Majighu2015 Daudi Mchambuzi Kalikenye Maguniolaf Juma chief Titans Salary Slip FreeLancer kichomiz Nyoka Mwenye Makengeza TUJITEGEMEE permanides Pohamba BAK sharif jingalao
 
Hatari sana watu wa serikalini wanapanik lakini pia Mkuu wa Nchi awe na kifua cha kujizuia ''alichoambiwa'' kabla ya kutoa hotuba kwa Taifa kwa kufanya uchunguzi wa kina kupitia vyombo vya usalama na taasisi za serikali kuwa kuna vichwa havina mwenyewe.

Wakuu wa idara za serikali, taasisi na mashirika ya umma n.k kabla ya kutoa taarifa kwa Mkulu mfuate mawaidha ya Jakaya Kikwete kupitia Nukuu murua @jmkikwete ''Akili za kuambiwa changanya na zako''
 
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari nchini, Engineer Deusdedit Kakoko amesema vichwa vya treni vinavyodaiwa kutelekezwa bandarini ni mali ya shirika la Reli nchini TRL na kwamba vina nembo ya TRL (Tanzania Railway Limited). Kakoko amesema TRL walinunua vichwa hivyo bila kufuata utaratibu kutoka kampuni ya EMD ya nchini Marekani, lakini vimetengenezwa na kampuni ya DCD ya nchini Afrika Kusini.

Maelezo ya Kakoko yanahitimisha taarifa "zilizovumishwa" hivi karibuni kuwa vichwa hivyo havina mwenyewe. Kwa lugha rahisi ni kwamba Engineer Kakoko amesema SI KWELI kwamba vichwa hivyo havina mwenyewe. Kakoko anasema ni vya TRL na vina nembo ya TRL.

Source:
Mmiliki wa vichwa 13 vya treni bandarini afahamika

MyTake:
Nimetafakari sana maelezo ya Kakoko nikakumbuka zile tambo za juzi kwamba tumekamata vichwa vya treni ambavyo havina mwenyewe. Nikajiuliza lengo la tambo zile lilikua nini? Kama Kakoko alijua vichwa ni vya TRL ilikuaje "mwenye nyumba" akasema havina mwenyewe? Hakumuuliza Kakoko? Alidanganywa? Alijua ukweli lakini akatupotosha? Ili iweje? Kwa faida ya nani?

Kwani angesema ni vya TRL lakini vilinunuliwa bila kufuata utaratibu kungekua na tatizo gani? Kwanini aseme uongo kuwa havina mwenyewe wakati vina nembo ya TRL? Ina maana hakuona hata nembo? Au hiyo nembo iliwekwa baada ya "mwenye nyumba" kuondoka? Anyway tuendelee kumuombea.!!
Hivi tunamwombea nini? Sijawahi kusikia akisema aombewe nini! Hata mnaosema tuendelee kumuombea hamsemi tumwombee nini.
 
Kwani Mkurugenzi wa TRL amekubali kuwa aliagiza hivyo vichwa? Na waziri je,
 
Wana-JamiiForums tutazame picha hizi na kichwa kimoja kushoto namba 9002 picha ya kwanza tayari kinakula mzigo kama video clip hapo chini inavyo sapoti picha hizo za bandarini kuwa vichwa hivyo ni mali ya TRL kwa kichwa namba 9002 kikikatiza Dodoma na shehena ya makontena ya kutosha.

Kwa maana nyingine katika vichwa 13 visivyo na mwenyewe vichwa vingine tayari vimechukuliwa na TRL na vinafanya kazi na hivyo mzigo wote huu wa vichwa vilivyopita bandarini ni mali halali ya TRL mbali ya vile vichache alivyooneshwa Mh. Rais vilivyobaki bandarini.

pic+vichwa.jpg

Picha Source: Vichwa vya treni vyaibua utata

Tanzania Railway, Freight train タンザニア・ドドマ駅発西行き貨物列車
Freight train with 21 wagons just started from Dodoma station in Tanzania at 5:55 p.m. on June 20, Mon. 2016, near to the railroad crossing in the west of Dodoma station.

Source: Hitoshi Suzuki

c.c Majighu2015 Daudi Mchambuzi Kalikenye Maguniolaf Juma chief Titans Salary Slip FreeLancer kichomiz Nyoka Mwenye Makengeza TUJITEGEMEE permanides Pohamba BAK sharif jingalao

Tusubiri mtu kutumbuliwa kwa kiki
 
cf969d6e1bb3064bac4cd3b52a42b0ec.jpg

View attachment 535327
KAMPUNI ya Reli Tanzania (TRL) imekanusha kuhusika na vichwa 11 vilivyoshushwa na kutelekezwa katika Bandari ya Dar es Salaam hivi karibuni. Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Deusdedit Kakoko, vichwa hivyo vilivyoshushwa na meli ya Mesina Line tangu wiki iliyopita, na kwamba ni mali ya TRL.

Akizungumza na gazeti hili Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo, Masanja Kadogosa alisema TRL haihusiki kwa namna yoyote na vichwa hivyo kwa kuwa hakuna taarifa zozote zinahusu uagizwaji wake.

Alisema pia kwa mujibu wa Sheria ya Manunuzi, kampuni hiyo inapofanya manunuzi yoyote lazima kuwepo na mkataba wa makubaliano na kampuni husika inayouza bidhaa, lakini haina mkataba wowote unaohusu ununuzi wa vichwa hivyo.

Alieleza kuwa taratibu za manunuzi zinafahamika kwani endapo kampuni hiyo ingeagiza vichwa hivyo ingetakiwa kupeleka mtu wake kwa ajili ya ukaguzi wakati vinatengenezwa na mara baada ya kutengenezwa kabla ya kupakiwa kwenye meli. “Lakini hiyo kitu hakuna, hatukuwa na watu wetu kwa kuwa si mali yetu,” alieleza.

Pamoja na hayo, alisema ili mzigo wowote umfikie mhusika lazima kuwepo na nyaraka ya kutolea mzigo bandarini ambayo pia huwa na makubaliano mengine baina ya mnunuzi na muuzaji ambayo katika sakata hilo, TRL wamesisitiza hawana nyaraka hiyo.

Alisema TRL haivitambui vichwa hivyo kwa kuwa si mali yake. “Hivi ni vichwa vikubwa sasa kwanini tuvikatae kama ni vyetu, ila ukweli ni kwamba hatuvitambui kabisa,” alieleza mkuu huyo wa reli nchini.

Juzi wakati akizundua Mradi wa Uboreshaji wa Bandari ya Dar es Salaam (DSMGP), Rais John Magufuli aliibua hoja hiyo ya vichwa vya treni kushushwa bandarini na kutekelezwa bila kuwa na mwenyewe na kuitaka TPA pamoja na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, kufuatilia kwa kina suala hilo.

Dk Magufuli alisema anazo taarifa za kushushwa kwa vichwa vya treni takribani 15 katika bandari hiyo, ambavyo mmiliki wake hafahamiki na meli iliyovileta imeshaondoka. Hata hivyo, mkurugenzi wa mamlaka hiyo ya TPA Kakoko pamoja na kuthibitisha kushushwa kwa vichwa hivyo kutoka kwa meli ya Mesina Line, iliyobeba mzigo huo kutoka kwa Komazi Trading Co, alibainisha wazi kuwa vichwa hivyo ni vya TRL.

Alisema vichwa hivyo ni awamu ya pili iliyoagizwa tangu serikali ya awamu ya nne miaka mitatu iliyopita, ambapo awamu ya kwanza ilishaletwa na vichwa vyake kuchukuliwa na hadi leo vinatumiwa na TRL.

Alifafanua kuwa baada ya uchunguzi wa TPA ilibaini kuwa kuna mgogoro unaoendelea kati ya TRL na kampuni ya Komazi na kwamba TRL ilishagoma kuvichukua vichwa hivyo lakini suala hilo, halikutaarifiwa kwa TPA

Chanzo: Habari leo

My Take:

Kama hawavitaki wamgawie Askofu Gwajima wa ufufo na Uzima kwani anatafuta vichwa Treni.
Vituko kama hivi vilikuwa vinatokea kule Zaire ya Mobutu. Waziri aliweza hata kuingiza mabaki ya nuklia bila hata serikali kufahamu.
Hili la TRL, watengenezaji siyo wajinga kiasi hicho kuleta vichwa vya treni, vyenye nembo ya TRL wakati hawajui nani atalipa.
 
Magufuli ni rais mjinga kabisa ambaye Tanzania ishawahi kupata.

Tatizo Watanzania wengi wanafurahia ujinga wake.
 
Back
Top Bottom