Kampuni ya Reli Tanzania(TRL) yavikana vichwa vya Treni, yataka virudishwe vilipotoka

Hii nchi ina maajabu mengi sijui kwa nn hayaingizwi kwenye kitabu cha maajabu ya dunia?
 
Manunuzi ya ndege yalifuata utaratibu? Nawaza tu
 
Hapa ninachokiona hivyo vichwa viliagizwa na TRL na waziri wao kwa wakati huo awamu ya nne, sasa waziri mpya wa uchukuzi akiangalia mkakati wa awamu ya tano hayo madude ni useless comparing with magu idea of SGR, Kinachotokea sasa ni wanunuzi kukataa mzigo, (wateja wanakuwa vigeu geu... Mimi ni mfanyabiashara), je ni nani atamfunga paka kengele?.
 
 
Anachokihitaji Pombe atakaporudi ofisini ni kwa mmiliki wa vichwa hivyo kujulikana...la sivyo kuna mtu ataingia matatani.

Ni hivi jingalao, mwenye maelezo ya hivyo vichwa ni waziri Mwakyembe. Mbona imekuwa ni kuzunguka mbuyu au Magu naye ameeanza kuingiza baridi sasa baada ya kuona vita vinakula na watoto wake?
 
Anachokihitaji Pombe atakaporudi ofisini ni kwa mmiliki wa vichwa hivyo kujulikana...la sivyo kuna mtu ataingia matatani.
Waliovishusha sio vichaa, wahusika wako serikalini sasa watu wanaoneana aibu, mbona wengine wanafukuzwa kwa kutajwa tu jukwaani lakini hili mpaka mali imefika kunakua na kigugumizi. Double standards
 
Baba mwenye nyumba wa nchi hii ni Raisi, hivyo kila kitu kinachohusu ndani ya Nyumba yake ni lazima apate taarifa zilizonyooka.
Wewe na hao wanafiki wenzio mnataka kupotosha umma wa watanzania ionekane kwamba mh. Raisi katudanganya. Wewe ndiyo mpotoshaji mkubwa pia ni muongo mkubwa na hicho kikundi chenu kidogo ambacho kazi yenu kugeuza maneno ya ukweli ili yaonekane ni uongo.
Tahadhali kwa nyie ambao mnajifanya hamjui kuwa Mali za nchi hii ilikuwa inaishia kwenye matumbo ya wabaya wachache. Mtakwenda na maji pasipo kupata msaada wa msamaria mwema.
 
Nimeipenda sentensi yako ya mwisho, "Tuendelee kumuombea", ukweli kabisa hakuna njia nyingine yeyote inayoweza kuliokoa hili taifa zaidi ya maombi. Hata nchi ya Kusadikika naona ilikuwa na unafuu ukilinganisha na hapa kwetu.
 
Acha uchochezi! Mhe. Rais yupo Sahihi na Eng. Kakoko yupo Sahihi! Wewe hujui kama kila kitu hapa duniani kinatawaliwa na time, space, pressure & temperature? Badiliko la kimojawapo linaweza kuleta majibu tofauti!
 

Mkuu nakubaliana na wewe.

Wanachosahau ni kuwa kama vichwa viliagizwa na TRL hata kama ni management ya zamani, bado ni mali ya TRL.

Nadhani huyu Mkurugenzi mkuu anasahau kuwa TRL ni taasisi, hivyo anatakiwa kuheshimu mikataba iliyoingiwa na watangulizi wake hata kama yeye binafsi hakubaliani nayo.
 
Ni hivi jingalao, mwenye maelezo ya hivyo vichwa ni waziri Mwakyembe. Mbona imekuwa ni kuzunguka mbuyu au Magu naye ameeanza kuingiza baridi sasa baada ya kuona vita vinakula na watoto wake?
Kuingiza baridi ndio nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…