myoyambendi
JF-Expert Member
- Sep 13, 2013
- 166,767
- 705,461
Mimi pia nilifunga kijijini mpaka mkataba umeisha sikupata tatizo...Sio kweli mimi mwaka Wang wa 4 haijawahi kunisumbuaaaa
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mimi pia nilifunga kijijini mpaka mkataba umeisha sikupata tatizo...Sio kweli mimi mwaka Wang wa 4 haijawahi kunisumbuaaaa
Umesema vyema. Watu kutoa tuhuma kwa wafanyakazi sio ofya kabisa. Na kuisema kampuni ni ya kitapeli sio sahihi.Shalom Wana JF, mimi ni mgeni humu Jamii Forums,
Nimesoma tuhuma mbalimbali kuhusu hiyo Kampuni ya ENGIE Mysol. Binafsi ninaifahamu maana nilishawahi kufanya kazi hapo nikiwa likizo yangu ya masomo ya Shahada ya Uzamivu(Sabbatical Leave)kuanzia mwaka 2018. Niliajiriwa full time kama Risk Analyst lakini muda mwingi nilikuwa nautumia masomoni UDSM hivyo katika mwezi mzima nilikuwa naweza kuonekana ofisini kwao Arusha siku mbili au tatu kisha naondoka zangu. Hata baada ya kumaliza PhD yangu November 2020, niliendelea kufanya nao kazi huku nikiendelea na Ajira yangu Mama so Mshahara wao na viposho vya safari vilikuwa ni kwa ajili ya Projects zangu za Ujenzi tu na kula Bata[emoji3]
Tuhuma zimetolewa nyingi lakini kuhusu hilo la MD Mr. Mugambi kutaka kubaka mfanyakazi ofisini naomba NILIPINGE kwa nguvu zote. Namfahamu huyo Mzee(kweli ni Mkenya)lakini ni mtu MUUNGWANA sana na nina uhakika hawezi kufanya uhuni huo(kwa hilo nitamtetea mpaka kaburini). Kuhusu huyo Veronica Kahama kimsingi hata mimi nilishawahi kukorofishana maana alitaka kunipanda kichwani(kipindi hiko nilikuwa naripoti kwake). Nakumbuka tulizinguana mbele ya MD na huyo Dada akatamka kwamba hataki mimi niripoti kwake[emoji2]na mimi nikamjibu palepale kwani na mimi nataka kuripoti kwako, kwendaaa[emoji1787]ndio siku hiyohiyo nikabadilishiwa Reporting Line nikaanza kuripoti kwa mshkaji Adam Kamanda.
Na kabla ya Kikao siku hiyo, nilishawahi kukwaruzana na huyo Dada na nakumbuka nilimpigia simu MD Mugambi na nikamwambia amwambie huyo Dada nitamtandika makofi sitakagi ujinga. Hivyo kwa kifupi huyo Dada ni mzinguaji na ndio maana hata siku ya mwisho nilimtukana matusi ofisini pale tukafikishana mpaka Central Polisi Arusha. Zaidi ya hapo naamini wafanyakazi wengine wote ni watu waungwana akiwemo Mkurugenzi Mkuu Mr.Mugambi.
Hilo la tuhuma za kwamba ni Kampuni ya MATAPELI, Majambazi nk naomba nisilijibu maana katika utendaji wangu wa kazi sikuwahi kuona matukio hayo zaidi ya wao kama Kampuni kuibiwa sana na wateja nami kwa kadri ya uwezo wangu nilijitahidi kupambana na wahalifu mbalimbali.
For God And My Country
Kwanini usifanye ww hio biashara na ndugu zako?Pole Ndugu,nawafahamu hao Mysol na niliwahi kufanya nao kazi. Zamani walikuwa wanaitwa MOBISOL,baadaye wakabadili jina na kujiita ENGIE na sasa wanajiita MYSOL. Ni Kampuni ya WEZI tu na hakika ni MAJAMBAZI KWELIKWELI.
Wana Mkurugenzi Mkuu anaitwa Godfrey Mugambi ni Mkenya,ni zoba hatari.
Yaani ni Mkurugenzi Mkuu lakini anapelekeshwa na Mwanamke mmoja Head wa HR anaitwa Veronika Kahama hivyo Mkurugenzi Mkuu yupo kama picha tu.
USHAURI WANGU kwako MTOA MADA ni kwamba NG'OA HUO MTAMBO kauuze kisha nenda Polisi kafungue RB kwamba umeibiwa basi mchezo umeisha.
Kama walikuuzia ukiwa full kwa maana ya Panel,Betri,TV Inch 43 na vile Vitaa vyao basi NAKUSHAURI KAUUZE hutakosa Milioni Moja Na Laki Tano(1,500,000).Na hata ukiuza kifaa kimojakimoja hutakosa Tsh Milioni Moja hivyo bado utakuwa na faida nzuri tu.
NAKUHAKIKISHIA HAWANA UBAVU WA KUKUFANYA KITU CHOCHOTE IWE KUKUSHTAKI POLISI WALA MAHAKAMANI.
Bahati mbaya sipo huko lakini ningekuwepo huko ningekuja Babati kwa gharama zangu uniuzie mimi huo Mtambo na ningekupa Pesa cash.
Kikubwa ung'oe kauuze kisha nenda Polisi chukua RB kwamba umeibiwa na vibaka shughuli imeisha,HAWATAKUJA KUKUFANYA KITU CHOCHOTE NA HAWANA UBAVU HUO.
Na kama kuna Mteja mwingine yoyote humu wa hiyo Kampuni namshauri AUZE MTAMBO,achukue RB Polisi kisha anunue Sola za Bei nzuri mitaani kama SUNDAR nk.
Mtoa Mada njoo PM nikupe Elimu zaidi ya kuwakomesha hao Mbwa hata usiumize kichwa. Na kwa mtu mwingine yeyote anayetafuta Pesa humu usiumize kichwa.
Nenda kwa haohao Mysol,kopa Sola yao kwa kulipa kianzio kutegemea na ukubwa wa Sola(Watt 200 ni Tsh.285,000)(Watt 120 ni Tsh.185,000) na (Watt 80 ni Tsh 150,000)kama sikosei,kisha wakishakufungia leo,wewe kesho ung'oe kauuze huko hukosi Pesa,halafu wakija waambie ULIIBIWA NA VIBAKA na unawaonyesha RB biashara inakuwa imeisha hiyo.