Kampuni ya Sola ya Mysol ni Majambazi, Wananchi iogopeni kama UKIMWI

Shalom Wana JF, mimi ni mgeni humu Jamii Forums,
Nimesoma tuhuma mbalimbali kuhusu hiyo Kampuni ya ENGIE Mysol. Binafsi ninaifahamu maana nilishawahi kufanya kazi hapo nikiwa likizo yangu ya masomo ya Shahada ya Uzamivu(Sabbatical Leave)kuanzia mwaka 2018. Niliajiriwa full time kama Risk Analyst lakini muda mwingi nilikuwa nautumia masomoni UDSM hivyo katika mwezi mzima nilikuwa naweza kuonekana ofisini kwao Arusha siku mbili au tatu kisha naondoka zangu. Hata baada ya kumaliza PhD yangu November 2020, niliendelea kufanya nao kazi huku nikiendelea na Ajira yangu Mama so Mshahara wao na viposho vya safari vilikuwa ni kwa ajili ya Projects zangu za Ujenzi tu na kula Bata[emoji3]

Tuhuma zimetolewa nyingi lakini kuhusu hilo la MD Mr. Mugambi kutaka kubaka mfanyakazi ofisini naomba NILIPINGE kwa nguvu zote. Namfahamu huyo Mzee(kweli ni Mkenya)lakini ni mtu MUUNGWANA sana na nina uhakika hawezi kufanya uhuni huo(kwa hilo nitamtetea mpaka kaburini). Kuhusu huyo Veronica Kahama kimsingi hata mimi nilishawahi kukorofishana maana alitaka kunipanda kichwani(kipindi hiko nilikuwa naripoti kwake). Nakumbuka tulizinguana mbele ya MD na huyo Dada akatamka kwamba hataki mimi niripoti kwake[emoji2]na mimi nikamjibu palepale kwani na mimi nataka kuripoti kwako, kwendaaa[emoji1787]ndio siku hiyohiyo nikabadilishiwa Reporting Line nikaanza kuripoti kwa mshkaji Adam Kamanda.

Na kabla ya Kikao siku hiyo, nilishawahi kukwaruzana na huyo Dada na nakumbuka nilimpigia simu MD Mugambi na nikamwambia amwambie huyo Dada nitamtandika makofi sitakagi ujinga. Hivyo kwa kifupi huyo Dada ni mzinguaji na ndio maana hata siku ya mwisho nilimtukana matusi ofisini pale tukafikishana mpaka Central Polisi Arusha. Zaidi ya hapo naamini wafanyakazi wengine wote ni watu waungwana akiwemo Mkurugenzi Mkuu Mr.Mugambi.

Hilo la tuhuma za kwamba ni Kampuni ya MATAPELI, Majambazi nk naomba nisilijibu maana katika utendaji wangu wa kazi sikuwahi kuona matukio hayo zaidi ya wao kama Kampuni kuibiwa sana na wateja nami kwa kadri ya uwezo wangu nilijitahidi kupambana na wahalifu mbalimbali.
For God And My Country
 
Umesema vyema. Watu kutoa tuhuma kwa wafanyakazi sio ofya kabisa. Na kuisema kampuni ni ya kitapeli sio sahihi.
 
Kwanini usifanye ww hio biashara na ndugu zako?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…