KERO Kampuni ya SprinyTZ inakataa kutulipa ikidai hatujafanya kazi, mikataba hatujarudishiwa na NSSF hawalipi

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Habari,

Kuna kampuni inaitwa SprinyTz, iliyopo Makumbusho, Derm House, ghorofa ya tano. Kampuni hiyo inajihusisha na usambazaji wa huduma za fiber. Ilitangaza nafasi za kazi, tukatuma maombi na tarehe 1 Septemba tukaanza kazi.

Kampuni ilituajiri na kutuahidi kwenye mikataba kwamba ingetulipa mshahara wa Sh350,000 kwa mwezi, bila kujali kama tumefanya kazi au la. Kwa kweli, tulifanya kazi kwa moyo kwa sababu hatukutaka kulipwa bure. Licha ya kuwa wageni katika kazi hiyo, tulijitahidi na kufanikiwa kuleta wateja, lakini kampuni ilishindwa kuwahudumia kutokana na uzembe wao.

Sasa, mwisho wa mwezi umefika na wamekataa kutulipa, wakidai kuwa hatujafanya kazi. Mikataba tulisaini, lakini hadi leo boss hajaturudishia nakala zetu na badala yake tunaendelea kuzungushwa.

Jambo lingine ni kwamba kampuni ilituajiri na kututaka kuripoti kazini kila siku asubuhi na kuondoka jioni. Sisi hatuna namna nyingine ya kupata kipato, hivyo wanapogoma kutulipa, tunajiuliza tutaishi vipi?

Aidha, wafanyakazi wa kampuni hiyo hawana hata NSSF. Na hii si mara ya kwanza kufanya hivyo; baada ya tatizo hili kujitokeza, tuliwauliza marafiki zetu waliowahi kufanya kazi hapo na wakatuambia kuwa ni kawaida kwa kampuni hiyo kuwafanyia vijana hivyo.

Naomba mtusaidie kuupa sauti ujumbe huu ili suala hili lifuatiliwe. Ikiwezekana, muende katika ofisi zao mkachunguze hali halisi.

Nawasihi pia wengine wasitume maombi ya kazi katika kampuni hiyo hadi suala hili litakapowekwa wazi.
 
Kampuni ya wahuni hiyo
 
Back
Top Bottom