Kampuni ya uchimbaji madini ya Uingereza, Resources Indiana kuishitaki Serikali ya Tanzania kwa ukiukwaji wa mikataba

Kampuni ya uchimbaji madini ya Uingereza, Resources Indiana kuishitaki Serikali ya Tanzania kwa ukiukwaji wa mikataba

Kama kawaida yetu tuanze na zomea zomea ambayo haisaidii maisha yetu na ugumu wake. Muhimu tusikilize na kufahamishwa udhaifu uko wapi! Kinachofahamika ni upigaji wa awamu zilizopita bila kujali nini kinapatikana kwa wa-TZ wengine.

Kulikuwa na upuuzi kwa nchi za afrika ambao unarudiwa kwenye barua ya huyo mtu wa kampuni. Eti, foreign investment. Nchi gani imeendelea kutokana na kulegeza ili foreign investment ziingie? Foreign investment hufuata palipo pazuri basi! Sasa kama wao wanaona mazingira ni mabaya. waombe chao waondoke. Lakini nikionacho wanahangaika ili wabaki nchini kwa nguvu ya kisheria ya investments. Wabaki halafu tuwaone wataishije na usalama wao.
 
Patriot,
Haya ndio matatizo ya kutokutumia akili na elimu ndogo. Nchi zote Duniani zinalilia uwekezaji wewe unasema hakuna nchi inaendelea sababu ya uwekezaji, una akili kweli? China imeendelea kwa kuuza korosho? Au unadhani Tanzania tunaweza kuendelea kwa kuuza utumbo wa kuku?
 
Ukiisoma hiyo barua inaeleza kuna kampuni 10 tofauti ambazo zinamalalamiko ya aina moja kuhusiana na contractual dispute chanzo chake hiyo sheria ya madini.

Mbili tayari zisha wasilisha notice, ina maana zimebaki kampuni nane zingine.

Bado tu atutaki kuona kiini cha tatizo? Ukiwasikia tu wanasheria wa serikari na Kabudi pale amna contract lawyers.

Watu wanaposema wekeni hiyo mikataba wazi mpate perspective za kushindana na mabeberu mnawaona wapuuzi.

Wao wanaona kesi mnashindwa vipi ndio maana hawana shida kwenda mahakamani, wakati watanzania awajui details wawakosoe ata kupitia bunge.
 
Wakitushinda watalipwa pesa za walipa kodi.

Hawa viongozi WAZEMBE wanaotufikisha hapa sisi walipa kodi tushitaki kupitia wapi ikiwa kila media, bunge, na vyombo vinavyotuwakilisha vimevyata mkia?

Nampongeza Sirro.
 
Hakimu Mfawidhi,
Mkuu Hakimu Mfawidhi,
Kwanza usiwe na wasiwasi wowote, hivi ni vitisho tuu, hawa jamaa hawawezi kutufanya chochote wala hawawezi kutushitaki popote kwasababu tumeisha badili sheria zetu za uwekezaji kwenye sheria mpya ya madini, kwenye extractive industries tumeweka kipengele hiki
1579159308157.png

Hivyo hawa jamaa kama wana malalamiko yoyote, waende mahakama zetu za kizalendo.

Ila ile siku tulipo badili sheria, kuna watu tuliuliza humu

Sasa haya ni matokeo!.
P
 
Naamini waimba mapambio sasa nao wameanza kuelewa na kujua hali halisi. Kila siku zinavyosonga na mapambio yanazidi kupungua.
Si rahisi waimba mapambio kupunguza mapambio, kwani kwa sasa TZ sifa na kigezo mhimu sana ili uteuliwe na Mtenguzi na Mteuzi kuimba mapambio.
 
Pascal Mayalla,
Mkuu P unataka kuniambia hili kampuni la Mabeberu halina mkataba mkononi ambao tulisainiana nao? Au unafikili kwamba tutamalizana nao kibabe? Kama tuna uwezo wa kumalizana nao kibabe tungesubiri kwanza Mhe Palamagamba Kabudi aiondolee Zimbabwe vikwazo vya uchumi kama anao uwezo huo, ndipo tuwaguse hawa Mabeberu.
 
Pascal Mayalla,
Mimi sina ufahamu mzuri wa masuala ya sheria ila nina swali moja tu, Je marejeo ya sheria automatically yanafuta makubaliano ya awali? Kwanini hawa mabeberu wanataka kufungua mashitaka kwa kutumia mabadiliko ya sheria!
 

Hakuna kampuni inayofunga safari kufanya uwezekezaji wa muda mrefu haswa wa natural resources bila ya ‘stabilisation clause’ mabeberu yana experience ya kutosha kufahamu serikari za third world ubadilika na sheria sio stable.

Kwa ivyo wanajipanga mapema kwenye kulinda mikataba wanayoingia na sheria mpya, busara ilikuwa ni ku negotiate new terms zilizo fair au kutafuta angle zingine za mapungufu ya kimkataba kusimamisha.

Lakini kwa kutumia sheria mpya tu kufuta mikataba, mtakutana mahakama za usuluhishi.

Wanadhani kila mtu mtanzania uwafunge kwa kujiamulia tu kama wanavyomfanyia. Rugemalila.
 
Kama kawaida yetu tuanze na zomea zomea ambayo haisaidii maisha yetu na ugumu wake. Muhimu tusikilize na kufahamishwa udhaifu uko wapi! Kinachofahamika ni upigaji wa awamu zilizopita bila kujali nini kinapatikana kwa wa-TZ wengine.

Kulikuwa na upuuzi kwa nchi za afrika ambao unarudiwa kwenye barua ya huyo mtu wa kampuni. Eti, foreign investment. Nchi gani imeendelea kutokana na kulegeza ili foreign investment ziingie? Foreign investment hufuata palipo pazuri basi! Sasa kama wao wanaona mazingira ni mabaya. waombe chao waondoke. Lakini nikionacho wanahangaika ili wabaki nchini kwa nguvu ya kisheria ya investments. Wabaki halafu tuwaone wataishije na usalama wao.

Uko sahihi ni hatua gani tumewachukulia hao wapigaji wa hapa kwetu? Au ni yale yale ya kulindana huku tukishindwa kuwajibishana? Ilitakiwa wakati tunasumbua hiyo mikataba, watu wetu waliokuwa wameingia hiyo mikataba wawe ndani, ili hata hayo makampuni yaliyovunjiwa mikataba yao wajue kweli tuko serious. Sasa muwekezaji kaingia mkataba hata kama ni wa kinyonyaji aone basi hata viongozi aliongia nao mikataba wako jela, na sio kuwaona wakitanua kwa pesa walizowahonga, na nyingine zikiwa katika mabenki ya ughaibuni. Hamna mzungu mjinga wa hivyo.
 
Juzi ilikuwa Winshear ya Canada Leo tena hawa, sifahamu kesho atakuwa nani?

Labda Palamagamba aliliona hili alipokuwa anabadili mikataba na akaona gharama za hizi kesi ni ndogo kuliko faida ya kubadili mikataba.

Palamagamba alibadili Mikataba? Au alibadili Sheria?

-Kaveli-
 
Back
Top Bottom