KERO Kampuni ya Ujenzi iliyopo Madale Midizini ina changamoto ya kutotoa mikataba kwa baadhi ya wafanyakazi wake

KERO Kampuni ya Ujenzi iliyopo Madale Midizini ina changamoto ya kutotoa mikataba kwa baadhi ya wafanyakazi wake

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Mimi ni Mfanyakazi wa Kampuni ya Ujenzi wa miundombinu yenye makazi yake Madale Midizin Jijini Dar es Salaam.

Changamoto ni kwamba mpaka sasa nina Mwaka wa nne kazini ila sijawahi pewa mkataba, nakosa haki zangu muhimu, bado najulikana ni kibarua tu wa hii kampuni.

Tabia hiyo imekuwa ikitokea kwa baadhi ya Wafanyakazi na kuchangia kushusha mwamkoa wa kufa ya kazi.
 
Pole sana mkuu, sio hiyo kampuni tuu, zipo kampuni nyingi Bongo hazitaki kutoa ajira rasmi kuepuka kujibebesha mzigo wa Nssf, Paye & SDL, kama mshahara wanalipa kwa wakati hivo vitu vingine visikusumbue sana. Pambana utengeneze njia yako
 
Kuna kampuni moja mshahara 200 ila posho kwa siku ni 35, wanakimbia nssf,payee na makato mengine ya serikali
 
Kina mmoja wa mwanza nilimtafutia bajaji ya abiria tena yumo humu mwisho wa siku ananiambia mara sina leseni mara niwe msaidizi dah niliishia kucheka tuu
Hao ndio wanavunja moto wa kutosaidia wengine wenye uhitaji wa dhati
 
Tatizo jf imevamiwa na matapeli wengi sana jf ya miaka 10+ nyuma ilikua sehemu salama sana , muda mwingine unakausha tuu tusidondokee kwa wasiojulikana 😀😀😀😀😀
 
Back
Top Bottom