wanzagitalewa
Senior Member
- Jan 25, 2018
- 128
- 84
Vyombo vya ulinzi na usalama nchini Tanzania vyadaiwa vimeanza uchunguzi dhidi ya Makamu Mwenyekiti wa Kampuni ya Ujenzi ya Yapı Merkezi Bwana Erdem Arioglu.Vyanzo mbalimbali vinaeleza kuwa Arioglu anatuhumiwa kuwa sababu kubwa ya kuchelewa kukamilika kwa mradi wa SGR huku akiwatendea visivyo makandarasi wa Kitanzania kwa kuwacheleweshea malipo yao.
Raia huyo wa Uturuki pia anatuhumiwa kuingilia siasa za ndani za Tanzania kwa kutoa rushwa kwa Wabunge mbalimbali kukwamisha miradi mbalimbali ya maendeleo kupitia michango yao Bungeni.Bunge la Tanzania linatarajiwa kutoa taarifa baada ya uchunguzi huku baadhi ya Wabunge wakitaka raia huyo wa Uturuki kuondolewa nchini mara moja.
Mbali na tuhuma hizo kampuni hiyo pia inatajwa kuendelea kuipa Tanzania hasara ya mabilioni kutokana na ujenzi wa chini ya viwango katika baadhi ya maeneo.Eneo mojawapo ni kipande cha daraja la Nkurumah eneo la Kamata jijini Dar es Salaam ambapo kampuni hiyo iliamuriwa kuvunja na kuanza ujenzi upya baada ya kuonekana liko chini ya kiwango ikiwemo muonekana wa wazi wa nyufa kama inavyoonekana pichani!.
Katika baadhi ya maeneo ya mradi huo usanifu umekiuka angalizo kwenye njia za maji na kuzifunga jambo ambalo linahatarisha usalama wa matumizi ya mradi huo pale utakapokamilika.Athari za jambo hili zinaelezwa kuwa zitailetea nchi maafa makubwa zaidi kama ajali na hasara za ukarabati wa mabilioni pale ambapo mradi huo utakamilika.
Katika tuhumu hizo imeelezwa kwamba serikali imeunda timu ya uchunguzi huku timu nyingine ya siri ikihakiki shughuli na rushwa katika mradi huo kabla ya kutoa ripoti rasmi.