Tetesi: Kampuni ya Yapi Merkezi kuchunguzwa kwa rushwa na kuingilia mambo ya ndani Tanzania

Tetesi: Kampuni ya Yapi Merkezi kuchunguzwa kwa rushwa na kuingilia mambo ya ndani Tanzania

Kuna zengwe linapikwa hapo sio bure
MaCCM ni mbwa mwitu mwenzao akichafuka na damu wanamtafuna.
Haihitaji degree kuliona hilo huyu mwamba wanataka kumnyang'anya tender ili waweke mtu wao ambaye watakula 1O% yao kila mgao ukitoka ku fund ujenzi.

Hilo zengwe ni kubadili timu ya fisi tu 😁😁😁 kama walivyobadili kwenye ishu ya vichwa vya treni kwa kisingizio kuwa alieagizwa alishindwa kuvileta kwa wakati.

R.I.p Magufuli yani sahizi wataelewa kuwa waliokuwa wanamkwamisha ni wapiga madili.
 
Raia huyo wa Uturuki pia anatuhumiwa kuingilia siasa za ndani za Tanzania kwa kutoa rushwa kwa Wabunge mbalimbali kukwamisha miradi mbalimbali ya maendeleo kupitia michango yao Bungeni.Bunge la Tanzania linatarajiwa kutoa taarifa baada ya uchunguzi huku baadhi ya Wabunge wakitaka raia huyo wa Uturuki kuondolewa nchini mara moja.
Huu mradi unahujumiwa makusudi au ni mwendelezo wa Siasa tu ?
Pascal Mayalla JokaKuu zitto junior Tindo
 
Kuna mahali watu Wa napambana kupata hii kazi na tayari wameshapewa awamu nyingine... Sasa ni kutengeneza mazingira ya kuonesha huyu mkandarasi hafai ili maamuzi ya kuleta wengine tena wachina yaonekane yana maana
 
Msijitoe ufahamu hata Sisi tunajua Kila kitu. Nani aliwaleta hawa Waturuki kama siyo JPM na timu yake? Nani mtetezi mkubwa wa kampuni hii baada ya kulambishwa hadi anagombana na kumtishia Mbunge wa Sumbawanga Aeshi Hillary kama siyo Msukuma Kasheku wa Geita?
Yapi Merkezi wamejenga miradi kibao nchini Saudi Arabia, wamejenga metro mjini Dubai, wamejenga miundombinu mingi nchini Algeria, ni wajenzi wa miundombinu mingi sana kwao Uturuki.

Utetezi wako wa kiwendawazimu kwamba nani aliwaleta hauna mantiki. Kama wamekosea hatua gani mmechukua? Kwahiyo kila kitu wakikosea mtamlaumu aliyewaleta, kazi yenu nini nyie mizimu?

Mbona hakuna nchi waliwahi fanya miradi wakalalamikiwa kwamba wana ubora mdogo au matatizo. Simamia nchi acheni upuuzi, hamna solution kila siku kulalamika sijui mwaka 2015 fulani alifanya hivi ndio maana 2022 inakuwa hivi
 
Someni miradi waliyojenga Yapi Merkezi duniani Major Projects.

Watashindwa nini kulaza mavyuma hayo na kumwaga zege. Kwanini mnataka kulazimisha kwamba hawawezi, kwanini msiwasimamie & kuchukua hatua na mbona hamtaji hao wabunge waliokula rushwa na hamuwafungulii mashtaka. Subiri zamu yenu kutimuliwa maofisini itafika tu.

Yani nyinyi hamna kitu mnaweza kazi kulalamika. Wananchi wanalalamika na serikali inalalamika. Sasa si mtoke mjiajiri tulalamike wote na tuchague wanaofanya kazi.

Na yule mkandarasi wa bwawa la umeme mnataka mseme nini. Hiyo lift tangu January hadi leo haijafika. Na wenyewe mtasingizia hawana uwezo wakati miradi yao kwao Egypt inajulikana
 
Bunge linaingiaje hapo, TISS wanafanya kazi gani, TISS walipaswa kuwa wanajua hili na mkeka ungekiwa mezani kwa Rais na Spika.

Huyo Mturuki alipaswa kuwa ashatembezwa siku nyingi, na Yarpi walipaswa kulipiswa faini kubwa sana.
 
Habari nzito hii kama taifa. Miradi mikubwa kama hii inatakiwa nchi ijitayarishe ktk kila nyanja.

Kuanzisha mradi kwa kustukiza kufuatia tamko, badala ya tamko hilo kujadiliwa kwa kina kuona vipi litatekelezwa, athari zake kiuchumi, athari yake kwa bajeti ya nchi, kimazingira, uwezo wa nchi kufanya usimamizi wa karibu wa utekelezeji n.k

Miradi mikubwa inatakiwa iangaliwe kwa upana na masuala mtambuka kutiliwa maanani ili uweze kumsimamia mkandarasi vizuri uwezo wake na aina ya modeli ya ujenzi anayojinadi nayo au kuitumia katika utekelezaji za mradi husika

Build-Operate-Transfer systems

1659612146007.png



TOKA MAKTABA:
Tarehe 12 November 2017

Zitto: Inawezekanaje Serikali ikasaini mkataba wa shilingi Trilioni 7 kujenga Reli na vifaa vyote vikatoka Uturuki?

Hoja na maswali ya Zitto Kabwe, yanafaa kuwa hadidu rejea ya mjadala mpana juu ya miradi mikubwa kwenye jukwaa hili wakilishi la wananchi wote yaani JF: soma zaidi hapa chini:

 
Mradi SGR kwa jinsi ulivyokuwa unaenda elimu ya vijiwe vya kahawa inatosha kutambua kuwa tunapigwa pakubwa.
 
Kuna wadada wameajiriwa na hiyo kampuni sijui wanagongwa na hao waturuki? Sio kwa nyodo zile aisee. Ukienda kuomba kibarua ukimkuta mwanamke kwenye hizo ofisi zao bora ugeuze tu. Ukweli ni kuwa maombi hayafikishwi zaidi hutupwa kwenye dustbin.
 
Habari nzito hii kama taifa. Miradi mikubwa kama hii inatakiwa nchi ijitayarishe ktk kila nyanja.

Kuanzisha mradi kwa kustukiza kufuatia tamko, badala ya tamko hilo kujadiliwa kwa kina kuona vipi litatekelezwa, athari zake kiuchumi, athari yake kwa bajeti ya nchi, kimazingira, uwezo wa nchi kufanya usimamizi wa karibu wa utekelezeji n.k
Miradi mikubwa na ya muhimu kwa uchumi, lakini viongozi wanaihujumu bila kujali kodi za watanzani zinapotea bure,

Huo uchunguzi utapita, na hutasikia mbunge wala kiongozi akifikishwa mahakamani kwa rushwa,
 
Lengo SGR isikamilike ama! Kama ni kweli kuna tatizo mahali.
 
Unajua Chato international airport ilijengwa na MAYANGA?
Ndege zinaanguka zituapo uwanjani hapo ama zinateleza na kupitiliza kwenye mashamba ya watu!?

Au sasa hivi wanaanikia mahindi kama uwaja wa mpira wa kikapu wa kule Lindi kiasi cha kusababisha mashindano ya ligi ya mpira wa kikapu kuharishwa (rejea kipindi cha michezo kilichorushwa jana usiku kupitia redio Tumaini inayotangaza kutoka Tabata -Dar es Salaam)?
 
Ndege zinaanguka zituapo uwanjani hapo ama zinateleza na kupitiliza kwenye mashamba ya watu!?
Au sasa hivi wanaanikia mahindi kama uwaja wa mpira wa kikapu wa kule Lindi kiasi cha kusababisha mashindano ya ligi ya mpira wa kikapu kuharishwa (rejea kipindi cha michezo kilichorushwa jana usiku kupitia redio Tumaini inayotangaza kutoka Tabata -Dar es Salaam) ?
😄😄 Kwamba haujui favouritsm Ni one form of corruption sio?

"I wish I kud be IGP" 😄😄
 
Back
Top Bottom