Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mwacheni JPM apumzike jamani, mkichunguza, mnamuumbuaVyombo vya ulinzi na usalama nchini Tanzania vyadaiwa vimeanza uchunguzi dhidi ya Makamu Mwenyekiti wa Kampuni ya Ujenzi ya Yapı Merkezi Bwana Erdem Arioglu.Vyanzo mbalimbali vinaeleza kuwa Arioglu anatuhumiwa kuwa sababu kubwa ya kuchelewa kukamilika kwa mradi wa SGR huku akiwatendea visivyo makandarasi wa Kitanzania kwa kuwacheleweshea malipo yao.
Raia huyo wa Uturuki pia anatuhumiwa kuingilia siasa za ndani za Tanzania kwa kutoa rushwa kwa Wabunge mbalimbali kukwamisha miradi mbalimbali ya maendeleo kupitia michango yao Bungeni.Bunge la Tanzania linatarajiwa kutoa taarifa baada ya uchunguzi huku baadhi ya Wabunge wakitaka raia huyo wa Uturuki kuondolewa nchini mara moja.
Mbali na tuhuma hizo kampuni hiyo pia inatajwa kuendelea kuipa Tanzania hasara ya mabilioni kutokana na ujenzi wa chini ya viwango katika baadhi ya maeneo.Eneo mojawapo ni kipande cha daraja la Nkurumah eneo la Kamata jijini Dar es Salaam ambapo kampuni hiyo iliamuriwa kuvunja na kuanza ujenzi upya baada ya kuonekana liko chini ya kiwango ikiwemo muonekana wa wazi wa nyufa kama inavyoonekana pichani!.
Katika baadhi ya maeneo ya mradi huo usanifu umekiuka angalizo kwenye njia za maji na kuzifunga jambo ambalo linahatarisha usalama wa matumizi ya mradi huo pale utakapokamilika.Athari za jambo hili zinaelezwa kuwa zitailetea nchi maafa makubwa zaidi kama ajali na hasara za ukarabati wa mabilioni pale ambapo mradi huo utakamilika.
Katika tuhumu hizo imeelezwa kwamba serikali imeunda timu ya uchunguzi huku timu nyingine ya siri ikihakiki shughuli na rushwa katika mradi huo kabla ya kutoa ripoti rasmi.
View attachment 2313893
Na atakayepewa ni yule mchina wa rais wa mawe! Firina zote hizi anazileta yeye ili mchina aweke mzigo mezani wa kumsaidia kwenye kampeni za kugombania kijiti ma maadam! Mama hajamshtukia huyo mvaa bendera Hadi Sasa.Ukute wanataka aondoke Yapi Merkezi,wamtafute ambaye atawapa wao ten percent.
Ndio anaundiwa zengwe achomolewe....Huyo JPM wenu ndo alimleta huyo hebu ondoeni utaahira hapa nyie takataka zake.
Jee munampa fedha za kufanyia kazi kwa wakati?..mturuki amechelewesha sana huu mradi.
..haiwezekani dar to moro ichukue miaka 5 na bado mradi haujakabidhiwa.
..mchina alijenga reli ya tazara, dsm to kapirimposhi, na akakabidhi mradi ndani ya miaka 5.
cc Proved
Hahahaa au wakuone mko watu kama kumi tu mna jambo lenu. Ilifika mahali hata vikundi vya Saccos vikawa vinazuiwa wakidhani wanajadili mambo ya Chadema.Acha hizo, ingekuwa enzi za mwendazake ningekutaka uvae jezi ya Chadema kisha upite barabara ya stesheni, huko ungejua kuwa CCM na vyombo vya usalama ni mapacha.
Tunaambiwa vyomba vya usalama( vipenyo) viko kila mahali sasa mbona kila kona tunapigwa vyenyewe huwa vina kazi gani?Shame kabisa, kwenye huo Mradi Jiwe alijaza Maaskari wengi, walishindwa Kujua hizo hujuma na kuzizuia wakiwa on ground ?
Chanzo ni yeye mwenyewe na aliuficha kwa gharama zote sasa umeumbuliwa.Huu uhuni usingeusikia enzi za Magufuli
.haiwezekani dar to moro ichukue miaka 5 na bado mradi haujakabidhiwa.
Akina Majaliwa Kassimu walikuwa wanashinda mitandaoni kutwambia tangu 2019 mradi umefika asilimia 75%😀😀..mturuki amechelewesha sana huu mradi.
..haiwezekani dar to moro ichukue miaka 5 na bado mradi haujakabidhiwa.
..mchina alijenga reli ya tazara, dsm to kapirimposhi, na akakabidhi mradi ndani ya miaka 5.
cc Proved
Ha hahahahaaa! Huku najua frequency hazisomi. Kila la heri!"I wish I kud be IGP" 😄😄
Jee munampa fedha za kufanyia kazi kwa wakati?
Halafu unalinganisha mchina wa enzi ya Mao Zedong na leo hii wapi kwa wapi? Miaka 50+ nyuma!
Nilikuwa namjibu huyo aliyesema mchina ana Bei nafuu, ikiwa hajui mchina ndio ana Bei kubwa
Kuna sababu za kuchelewa, huu mradi unategemea donors. Sio kwamba pesa ipo tu bank. Hata bwawa linachelewa Kuna sababu zipo.
Aalafu huyo mchina nimekuambia kapewa kipande cha Isaka Mwanza. Kaangalie kinachoendelea.
Na hata hivyo kishapewa tena kipande kingine cha Tabora kigoma. Hivyo Kama unawapenda wachina Subiri watajenga tu wana vipande vingi na vikubwa tu
Jiwe ndio alieileta hiyo kampuniHuyu SSH ni janga na chawa wake TAKUKURU
Utavunjwa mkataba, kampuni itadai fidia na italipwa haraka, kumbe wanajilipa wenyewe.Inatafutwa sababu ya kupiga hela
Ujenzi wa dar Moro ni fedha za ndani na mkopo kutoka AFDB. Na huu mkopo wa AFDB mbona ulikuwa wazi tu. ni Kama ilivyokuwa Daraja la tanzanite ambalo limejengwa kwa mkopo na pesa za ndani. Yote haya yalikuwa reported kwa umma...kipande nilichohoji ucheleweshaji wake ni Dar to Morogoro.
..maelezo ya serikali yalikuwa kipande hicho kinajengwa kwa kutumia fedha za ndani, sio mkopo, donors / wafadhili.
..sijahoji kuhusu Moro Dom Makutupora. Lakini pia ninavyokumbuka fedha za kipande hicho ni mkopo toka kwa mabenki ya ulaya / mabeberu.
..mimi nilikuwa mmoja wa wanaJF waliotetea Yapi Merkez waliposhinda tender. Niliangalia rekodi yao ya ujenzi Dubai, Qatar, etc nikaamini wako vizuri. Sijui ni kwanini wamechelewesha mradi huu kwa kiwango hiki.
..hata Wachina wakichelewesha kazi tutahoji kulikoni. Tunatakiwa tu-demand kazi zenye kiwango zinazokamilika kwa wakati.
Wakati wa JPM, kazi ilipigwa kwelikweli na hii hii kampuni.Wewee wa ajabu! Hii kampuni si ililetwa na JPM? Kwa hiyo ndiye aliyehongwa?
Hakuna kampuni inaletwa na raisi, utaratibu unaotumika ni single source. Ndio maana unaona hata kipande cha Tabora kwenda kigoma kapewa mchina.Wewee wa ajabu! Hii kampuni si ililetwa na JPM? Kwa hiyo ndiye aliyehongwa?