Kampuni ya YAS ni failure katika huduma zao hasa Mix by YAS

Kampuni ya YAS ni failure katika huduma zao hasa Mix by YAS

Mshamba wa kusini

JF-Expert Member
Joined
Jun 30, 2015
Posts
2,857
Reaction score
3,593
Habari

Nimetumia mtandao huu takribani miaka 15 na hata baada ya kubadilishwa jina na umiliki kutoka tiGO kuwa YAS bado nilibaki kuwa mteja wao.

Kwa muda mchache niliotumia mtandao huu nimetokea kuchukia sana huduma zao hasa huduma yao ya Mix by YAS, hii imetokea baada ya uvumilivu wa muda mrefu mpaka leo hii nimeamua kuja hapa jukwaani.

Nimenunua umeme leo hii ni takribani siku ya tano sijapata token ya umeme huo na kila nikiwapigia simu wananiambia nisubiri. Kusubiri nitasubiri mpaka lini? Siku ya tano nikae na kiza na wasubiri nyinyi? Who is accountable?

Nawakumbusha tu FIRST IMPRESSION IS THE LAST IMPRESSION, msipokuwa makini mtapoteza wateja wengi sana kama mimi mlivyonipoteza.
 
Jana nilituma Laki moja kwa wakala wa mkoani, nikamuagiza jamaa apite hapo achukue, aisee, masaa kadhaa sms haijafika kwa wakala, jamaa kagoma kutoa hela mpate sms, mpaka nikawapigia simu ndiyo sms ikamfika wakala....Wazembe sana.
 
Back
Top Bottom