Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nina zaidi ya miaka 15 natumia tigo lakini baada ya kubadili kina tu... huduma zao nyingi zimepungua ubora... mbaya zaidi lililoniudhi hadi kutaka kuwa na mpango wa kuwakimbia kabisa... dkk na mb kukimbia kama upepo.... pia mtandao kukosa ubora.. ukiongea na mtu unakatakata vibaya mno... hadi keroHabari
Nimetumia mtandao huu takribani miaka 15 na hata baada ya kubadilishwa jina na umiliki kutoka tiGO kuwa YAS bado nilibaki kuwa mteja wao.
Kwa muda mchache niliotumia mtandao huu nimetokea kuchukia sana huduma zao hasa huduma yao ya Mix by YAS, hii imetokea baada ya uvumilivu wa muda mrefu mpaka leo hii nimeamua kuja hapa jukwaani.
Nimenunua umeme leo hii ni takribani siku ya tano sijapata token ya umeme huo na kila nikiwapigia simu wananiambia nisubiri. Kusubiri nitasubiri mpaka lini? Siku ya tano nikae na kiza na wasubiri nyinyi? Who is accountable?
Nawakumbusha tu FIRST IMPRESSION IS THE LAST IMPRESSION, msipokuwa makini mtapoteza wateja wengi sana kama mimi mlivyonipoteza.