Kampuni ya YAS ni failure katika huduma zao hasa Mix by YAS

Sasa bahati mbaya customer service agents wa Yas hawajui huduma zao. Sijui wanawatoa wapi hawawapi training. Nimekumbana na matatizo ambayo mengine najua solutions ila sina uwezo wa kurekebisha, unapiga mhudumu hajui au anasema uongo.

Inawezekana kuna vitu vingi hawajakaa sawa hawa wawekezaji wapya.
 
Hawarudishi pesa nashangaa sana hii kampuni ni ya hovyo sana tufikishe hii habari kwa watu wetu wa karibu.
 
mwanzo una changamoto zake gentleman,

ni muhimu kuwapa muda kidogo 🐒
Changamoto ni kutapeli pesa za watu? Ukifanya malipo hawakupi huduma na hela hawarudishi huu ni wizi. Siku zote taratibu za fedha ni baada ya muda ukishindwa kutoa huduma kuna kuroll back yani unamrudishia pesa mteja na wangefanya hivi hakuna mtu angelalamika.
 
YAS ni kampuni ya hovyo wanajipunguzia CREDIBILITY sana.
 
Wanafanya spamming meseji kibao zisizo na kichwa wala miguu lakini kinachoniuma zaidi ni hili la utapeli kwenye huduma za kifedha.
 
Huo mtandao hawakujipanga.Unatuma meseji haikifi kwa mlengwa na kwako haionyeshi jibu lolote kama imefail.Ukipiga huduma kwa wateja ndo unakutana na ujinga debe.Wanaanzisha huduma ambazo hawajazifanyia utafiti wakutosha.
 
Voda wataendelea kuliteka soko la mawasiliano nchini. Huduma zao zote ni tofauti sana na huduma za mitandao mingine, kuanzia M-Pesa, Internet, Mawasiliano ya kawaida n.k voda wana ligi yao bongo.
 
Kwani ndo wameanza!? Wewe ukibadili jina leo ukajiita Mapembelo ndo utakuwa umezaliwa upya!?
Yes of course gentleman,

ikiwa uliitwa Jacob na ukabadilika na kuitwa Yasini Lazima kuna changamoto kidogo zitatokea 🐒
 
Kwa muda mchache niliotumia mtandao huu nimetokea kuchukia sana huduma zao hasa huduma yao ya Mix by YAS, hii imetokea baada ya uvumilivu wa muda mrefu mpaka leo hii nimeamua kuja hapa jukwaani.
Nilikuwa Gairo jana kwenye lodge nilokaa walikuwemo hao watu, wako busy na vikaguru hawakumbuki kama kuna wateja huduma zao zimegoma
 
Voda wataendelea kuliteka soko la mawasiliano nchini. Huduma zao zote ni tofauti sana na huduma za mitandao mingine, kuanzia M-Pesa, Internet, Mawasiliano ya kawaida n.k voda wana ligi yao bongo.
vodacom wapewe maua yao.
 
Mkuu mwenyewe soon naachana nao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…