Kampuni za mabasi zilizotamba na kupotea

Nawasihi wale wasioelewa baadhi ya wamiliki wa mabasi (a.k.a matajiri) tusiseme wamefirisika bora ukae kimya kama hujui kitu.
 
sai baba, bufaroo
 
keshapotea karudi kwenye kilimo, kuna kipindi aliyojiwa na Ayo TV akasema kapumzika kwanza
Sumry bado yupo, sema kabadili jina tu.. mabasi ya mbeya to dar yameandikwa Mbeya Express...yale yanayopiga mbeya sumbawanga bado yameandikwa sumry....kwa sasa sumry ame base sana kwenye kilimo
 
Matajiri wengi wamebadili majina ya mabasi ingawa pia wapo waliofilisika. Kwa mfano njia ya Dar mpaka Moro zamani kulikuwa na basi linaitwa Makundi Coach. Sasa hivi ni BM Coach.
Njia ya Dar mpaka Tanga kulikuwa na basi linaitwa Air Shengena sasa hivi ni Tashrif;
Kulikuwa na Air Msae akabadili ikawa Metro Coach na hii Metro Coach kama kufilisika basi ni mwaka huu au mwaka jana mwishoni ila nakumbuka nilikuwa naziona basi zake pale Shekilango.
kanda ya Ziwa kulikuwa na mnyama mmoja anaitwa Ally's Sports Bus huyo anainuka Dar saa kumi na mbili asubuhi ikifika kumi na mbili jioni watu wanaitafuta Nyegezi. Huyu kaja kivingine sasa anaitwa Ally Star
Na pia kuna baadhi ya matajiri wameyapa makampuni yao majina mengine ingawa bado wanatumia yale ya zamani. Katika hili kwa mfano kuna Super Feo ndio Selous Express; kuna New Force ndio Golden Deer mkali wa Nyanda za Juu Kusini
Zuberi za Mwanza anatumia pia Kisesa.
 
Majira
Rafiki
TTBS
Lang'ata
Nzuweni
Ngorika
KBS-Mama Maeda
Muzdalfa
Msae
Moretco
KAMATA
ĎMT-Wahenga wananielewa hapa
OTC-Wahenga Nairobi-Dar 1975
 
Ally's Sports Bus ni tofauti na Ally's Star...ni biashara za Mtu na mdogo wake...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…