Kampuni za Yasser Provison Store na Zenj General zilizohusishwa kashfa ya Sukari na Waziri Bashe zinamilikiwa na nani

Wenye sifa walipewa vibali hawakuleta hata kilo moja.. hao wasio na sifa walifanikiwa kuleta au hawakufanikiwa .. kama walifanikiwa sioni shida mwisho wa siku lengo ni kupunguza maumivu kwa mwananchi
Ona sasa hizi akili ndogo za maccm

Unawatoto chief, au unapoiangalia nchi yako ukahusianisha na maisha ya kizazi chako kwa miaka 20 ijayo, unawaona wakiwa wanamaisha gani kiongozi, huoni wakimwagana damu kupigana na walioihodhi nchi?

Huoni kwamba wewe ni chanzo cha hayo?
 
Mbona wanasiasa wenyewe wanafanya biashara? Au hairuhusiwi?
 
Hairuhusiwi kimaadili.

Kiongozi wa umma akiteuliwa, anatakiwa akabidhi biashara zake Kwa mtu mwingine na asijihusishe na biashara muda wote awapo kiongozi Ili kuepuka Conflict of interest.
Uongo na siyo KWELI hata kidogo.

Inaruhusiwa, isipokuwa hairuhusiwi kufanya biashara na mwajiri wako katika Mazingira fulani fulani tu.
 
Usiwe mbishi!!
Naendelea kukataa, siyo KWELI kuhusu hicho ulichoeleza. Hiyo ilikuwa ni Sera ya Utawala ktk Awamu ya Kwanza ya Mwl Nyerere akiwa na Azimio lake la Arusha. Hii ilikuwa miongoni mwa sababu kubwa Sana zilifanya Utawala wake kuchukiwa na Watu wengi, kwani kupitia Sera hiyo aliweza kutaifisha biashara nyingi sana za Watu binafsi na kusababisha anguko Kuu la uchumi hapa Tanzania. Wahindi wengi sana waliporwa biashara zao pamoja na Nyumba zao ambazo nyingi siku hizi zinamilikwa na NHC.
 
Maadili ya viongozi kutojihusisha na biashara, mfano waziri wa nishati kuuza majenereta hiyo hairuhusiwi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…