John Wickzer Mulholland
JF-Expert Member
- Apr 13, 2023
- 6,656
- 14,403
Rejea Comment yangu#34 hapa juu.Maadili ya viongozi kutojihusisha na biashara, mfano waziri wa nishati kuuza majenereta hiyo hairuhusiwi.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Rejea Comment yangu#34 hapa juu.Maadili ya viongozi kutojihusisha na biashara, mfano waziri wa nishati kuuza majenereta hiyo hairuhusiwi.
State Capture.Mimi bado namshangaa mteule wa Bashe kwa nini bado Bashe anaendelea kuwa Waziri wa Kilimo. Ripoti hii inatisha sana. Kampuni ya stationery, Kampuni ambayo kisheria ya Brela hairuhusiwi kufanya biashara na Serikali, Kampuni toka Zanzibar kuruka kuja Tanzania Bara kupewa vibali. Hii inatisha sana.
Jamaa wanakula good time ya TZ,madogo wa kishombe kwenye mikopo ya bank ni mserereko wamejazana tandika,kkoo hadi posta na maduka ya simu na electronics zingine,ndio mamilionea wajao wakati vijana weusi wanaandaliwa kuwa bodaboda,sad!!Wa-Asia wataimaliza hii nchi
Halafu zinatoza shs. 1000/= ya ziada kwa kila kilo! Wizi mtupu!Je hiyo/hizo kampuni zilifanikiw kuagiza Sukari?
Sitetei ila nimemuuliza hao wasio na sifa walifanikiwa kuleta sukari ?! Maana kulisemwa bungeni makampuni ya sukari yenye sifa walipewa vibali lakini hawakuongiza sukari hata kilo moja ili kuongeza uhaba mpaka bei ifike elfu kumi na moja kwa kilo .Swali hao wasio na sifa waliingiza na kama waliingiza sukari waliuza bei gani ?! Mwisho wa siku tunataka afadhali kwa mlaji wa mwishoAcha kutetea usichokijua.
We kweli njiwa,bila kufugwa na ccm hutoboiWenye sifa walipewa vibali hawakuleta hata kilo moja.. hao wasio na sifa walifanikiwa kuleta au hawakufanikiwa .. kama walifanikiwa sioni shida mwisho wa siku lengo ni kupunguza maumivu kwa mwananchi
Hivi hizi ref number,mpaka namba za risit kazipataje pataje,atakua ana hackBodi ya Sukari ilisajili Makampuni kuingiza sukari ambayo hayakuwa na sifa kisheria na Makampuni hayo hayakuwa na rekodi yoyote ya kujihusisha na biashara ya sukari na pia uwezo wao wa kifedha ni wa kutiliwa mashaka jambo ambalo ni kinyume cha Sheria ya Sukari.
Baadhi ya Makampuni machache yaliyopewa vibali vya kuingiza sukari nchini ambayo hayana viwanda vya kuzalisha sukari nchini ni kama ifuatavyo:-
3.3.1 ITEL EAST AFRICA LIMITED ambaye Bodi ya Sukari ilimuandikia barua yenye Kumb. Ref. No. SBT/DGO/09/VOL.II/2-10 ya tarehe 2 Januari 2024 iliyosainiwa na Lusomyo Buzingo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Bodi wa Sukari ikiitarifu kampuni hiyo kuwa Serikali imeidhinisha kuingiza tani 50,000 za sukari (Kiambatisho Na. 14).
Lakini tarehe 9 Januari 2024 na tarehe 30 Januari 2024 Kampuni ya ITEL ilipewa vibali vya kuingiza tani 60,000 za sukari zaidi ya kiwango ya kiwango kilichoidhinishwa kwenye barua rejea kibali SR Na. 8652445335 na 944600548 (Kiambatisho Na. 15)
Pia vibali alivyopewa ITEL ni zaidi ya viwanda vyote vitano ambavyo jumla vimepewa tani 50,000 tu kwa maana ya tani 10,000 kila kiwanda.
Baada ya kufanya upekuzi wa BRELA tarehe 10 Juni 2024 (Kiambatisho Na. 16) ilibainika kuwa:-
Kampuni ya ITEL EAST AFRICA LIMITED imesajiliwa Tarehe 15 Februari 2013 yenye ofisi zake Ilala, Dar es Salaam, Kwa ajili ya biashara za kuuza rejareja simu, komputa, TEHAMA na vifaa vingine vya mawasiliano na sio biashara ya sukari.
Wizara ya Kilimo na Bodi ya Sukari wameipa kampuni ya ITEL kuagiza sukari wakati ni kampuni ya kuuza simu na Kampuni hiyo haina uwezo, ujuzi na weledi wa masuala ya sukari na hivyo inaweza kupelekea kuingiza sukari isiyo na ubora, kufanya udanganyifu, kukwepa kodi na kuliingiza taifa katika migogoro ya Kibiashara kimataifa.
Kampuni ya ITEL EAST AFRICA LIMITED 49% ya hisa zinamilikiwa na raia wa India
Viwanda vya ndani vinavyolipa kodi, soko la Wakulima wa miwa na kutoa ajira kwa watanzania wengi vimeachwa na kipaumbele kupewa Makampuni binafsi.
Kampuni ya ITEL EAST AFRICA LIMITED ina hisa za kawaida 1000 zenye thamani ya Tsh. 50,000,000
Kampuni hii ina mtaji mdogo na sijaona ushahidi wa kuongeza mtaji na hivyo haiwezekani kupewa kazi ya zaidi ya Tsh. Bilioni 160 kwa mara moja, nimefuatilia Financial Statements za mwaka 2020, 2021, 2022, 2023 inaonyesha Kampuni inafanya biashara ndogo na haina uwezo mkubwa kifedha. Kitendo cha kupewa vibali vya kuagiza sukari kwa mara moja zenye thamani ya Tsh. Bilioni 160 kupitia Kampuni hii inaweza ikawa ni utakasishaji wa fedha haramu, kufanya udanganyifu na kukwepa kodi.
Kampuni ya ITEL EAST AFRICA LIMITED ilihuisha taarifa zake Tarehe 19 Februari 2024 siku chache baada ya kupewa barua na vibali vya kuingiza sukari nje ya nchi kati ya tarehe 9 na 30 Januari 2024. Pengine ilikuwa kutafuta sifa za ziada.
Barua ya Bodi ya Sukari yenye Kumb. Ref. No. SBT/DGO/09/VOL.II/2-10 ya tarehe 2 Januari 2024 iliyoijulisha Kampuni ya ITEL kuruhusiwa kuagiza sukari nje ya nchi haionyeshi kama Kampuni hiyo iliwahi kuomba kibali cha kuagiza sukari kutoka nje ya nchi. Haya ni matumizi mabaya ya madaraka na inaweza kuwa kula njama kuiibia Serikali (organized crime).
Hata hivyo zipo taarifa kuwa Kampuni ya ITEL EAST AFRICA LTD inatumiwa na Kampuni ya MOHAMMED ENTERPRISES (T) LTD. kwa mgongo wa nyuma kuagiza sukari nje ya nchi kwa niaba yake. Taarifa za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) zinaonyesha kuwa mzigo wa sukari wa Kampuni ya ITEL ukifika bandarini unatolewa na Kampuni ya METL rejea nyaraka za kuondoa mzigo Bandarini za TRA (Kiambatisho Na.17), pia ziko taarifa za uhakika kuwa baada ya mzigo kutolewa Bandarini unapelekwa kwenye ICD ya Mohamed Enterprises na kutoka ICD sukari inapelekwa kwenye Godown za Mohamed Enterprises na baadaye kuuzwa rejareja na jumla rejea risiti ya TRA ya EFD Na. 32 ya tarehe 22 Februari 2024 na risiti yenye verification code na.28630946606 ya tarehe 23 Februari 2024. Iliyotolewa na Kampuni ya Mohammed Enterprises (T) LIMITED (Kiambatisho Na.18)
Mahusiano ya kibishara baina ya Kampuni ya MOHAMMED ENTERPRISES (T) LTD na ITEL EAST AFRICA LTD hayako wazi na yanaweza ikawa ni mkakati wa kutakatisha fedha haramu na kukwepa kodi za Serikali.
3.3.2 Kampuni ya J SQUARE INVESTMENT GROUP COMPANY LIMITED ambaye amepewa Kibali cha kuagiza sukari Tani 2,500 cha tarehe 22 Juni 2023 (Kiambatisho 19), na kibali hiki kilitolewa wakati uzalishaji wa viwanda vya ndani ulikuwa umeshaanza.
Baada ya kufanya upekuzi wa BRELA (Kiambatisho Na. 20) tarehe 10 Juni 2024 ilibainika yafuatayo:-
Kampuni ya J SQUARE INVESTMENT GROUP COMPANY LIMITED ilisajiliwa Tarehe 28 Oktoba 2010 yenye ofisi zake Ilala, Dar es Salaam inayojishughulisha biashara za stationary, huduma za upishi wa vyakula (event catering) na usafi wa mazingira na sio biashara ya kuagiza sukari nje ya nchi.
Kampuni ya J SQUARE INVESTMENT GROUP COMPANY LIMITED ina hisa za kawaida 1000 zenye thamani ya Tsh. 1,000,000
Kwa mapungufu haya usingetarajia Bodi ya Sukari itoe kibali na Kampuni hii ambayo suala la kuagiza sukari sio sehemu ya biashara zake na hata hisa inazomiliki zenye thamani ya Tsh. 1,000,000 kwa hali ya kawaida Kampuni hii haina uwezo wa kuagiza tani 2,500 kwa mara moja zenye thamani ya USD 2,500,000 sawa na Tsh. Bilioni 6.6. maamuzi haya ni matumizi mabaya ya madaraka na unaweza ukawa ni utakasishaji wa fedha haramu.
3.3.3 Kampuni ya Yasser Provision Store
Kampuni hii imepewa kibali Na. 9043487787 cha tarehe 2 Aprili 2024 kuingiza sukari nchini tani 10,000 nchini (Kiambatisho Na.21) na kibali kimetolewa kwa maelekezo ya Waziri wa Kilimo na sio kwa sababu nchi ina upungufu wa sukari. Rejea barua ya Bodi ya Sukari yenye Kumb. Na. SBT/DGO/C/13-23 ya Tarehe 29 Aprili 2024 iliyosainiwa na Mkurugenzi Mkuu Bodi ya Sukari, Prof. Bengesi kwenda kwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato.
(Kiambatisho Na.22)
Baada ya kufanya upekuzi wa ZBPRA na BRELA (Kiambatisho Na. 23) tarehe 13 Juni 2024 ilibainika yafuatayo:-
Kampuni hii imesajiliwa Wakala wa Usajili Biashara na Mali Zanzibar (ZBPRA) Tarehe 5 Januari 2016 na baadaye ilisajiliwa na BRELA na tarehe 4 Januari 2024 na kufungua Ofisi Mtaa wa Nyasubi, Kahama, Shinyanga.
Baada ya kupata usajili wa BRELA tarehe 4 Januari 2024, tarehe 29 Aprili 2024 akapewa kibali cha kuingiza tani 10,000 za sukari.
3.3.4 Kampuni ya ZENJ GENERAL MERCHANDISE COMPANY LIMITED
Kampuni hii ilipewa kibali No. SR No. 3925349484 cha kuingiza sukari nchini tani 60,000 tarehe 30 Aprili 2024 (Kiambatisho 24)
Baada ya kufanya upekuzi wa BRELA (Kiambatisho Na. 25) tarehe 10 Juni 2024 ilibainika yafuatayo:-
Kampuni hii haijawasilisha BRELA Financial Statements tangu mwaka 2016 hadi 2023 miaka 8 sasa. Kiufupi kampuni hili haliko hai na haliwezi kufanya biashara na Serikali.
Kampuni hii imesajiliwa Zanzibar lakini haijahuisha taarifa zake katika Mfumo wa Online Registration System (ORS) wa BRELA.
Kampuni hii imepewa vibali zaidi ya viwanda vyote 5 vinavyozalisha sukari nchini ambavyo vilipewa tani 10,000 kila kiwanda. Lakini pia uwezo wa kifedha wa kampuni hii ni wa kutilia mashaka kupewa kazi ya zaidi ya Bilioni 160.
51% ni ya ni ya NaniKuna Kashfa kubwa ya Kampuni 4 ambazo zimepewa vibali vya kuagiza sukari huku zikiwa hazina sifa wala uzoefu wa biashara ya Sukari Je ni nani wamiliki wa makampuni haya yenye nguvu kubwa hadi Waziri Bashe akaruhusu wapewe vibali vya kuagiza Tani 410,000 za sukari nje ya nchi?
Kampuni hizo zinazotajwa ni
1. ITEL EAST AFRICA LIMITED ambayo 49% ya hisa zake zinamilikiwa na raia wa India (DAR ES SALAAM)
2. Kampuni ya J SQUARE INVESTMENT GROUP COMPANY LIMITED (DAR ES SALAAM)
3 Kampuni ya Yasser Provision Store (ZANZIBAR)
4 Kampuni ya ZENJ GENERAL MERCHANDISE COMPANY LIMITED(ZANZIBAR)
Hapa ukichunguza kwa makini mama yumo kupitia hizo kampuni za Zanzibar na kijana wake hakosi,Kuna Kashfa kubwa ya Kampuni 4 ambazo zimepewa vibali vya kuagiza sukari huku zikiwa hazina sifa wala uzoefu wa biashara ya Sukari Je ni nani wamiliki wa makampuni haya yenye nguvu kubwa hadi Waziri Bashe akaruhusu wapewe vibali vya kuagiza Tani 410,000 za sukari nje ya nchi?
Kampuni hizo zinazotajwa ni
1. ITEL EAST AFRICA LIMITED ambayo 49% ya hisa zake zinamilikiwa na raia wa India (DAR ES SALAAM)
2. Kampuni ya J SQUARE INVESTMENT GROUP COMPANY LIMITED (DAR ES SALAAM)
3 Kampuni ya Yasser Provision Store (ZANZIBAR)
4 Kampuni ya ZENJ GENERAL MERCHANDISE COMPANY LIMITED(ZANZIBAR)
Issue ni procedure in place, ndio maana tuna bunge,kazi yake kutunga sheria na kanuni mbalimbali kwa ajili ya utekelezaji,hii siyo nchi waziri anaamka na kujiamulia hovyohovyo,Wenye sifa walipewa vibali hawakuleta hata kilo moja.. hao wasio na sifa walifanikiwa kuleta au hawakufanikiwa .. kama walifanikiwa sioni shida mwisho wa siku lengo ni kupunguza maumivu kwa mwananchi
Unaagizaje sukari una mtaji wa milioni hamsini?,are you serious?Nchi ilikua na shida ya sukari, waliopewa vibali wameleta Sukari Bado inaonekana ni kashfa.
Msi ingize siasa zenu za majitaka kwenye maisha ya Watanzania.
Issue ni procedure in place, ndio maana tuna bunge,kazi yake kutunga sheria na kanuni mbalimbali kwa ajili ya utekelezaji,hii siyo nchi waziri anaamka na kujiamulia hovyohovyo,
Ficha upumbavu wako
Unaagizaje sukari una mtaji wa milioni hamsini?,are serious?
Acha wendawazimu
Je ubora?,Ugonvi wa wansiasa ni wa masilahi sisi tunachojali ni sukali imeletwa na sasa hapa Mbeya imeanza kuuzwa sh. 3000 na pengine itashuka zaidi.