CCM hawawezi mrejesha mpemba tena kutawala zanzibar wahafidhina wa unguja ndio kabisaaa hawatokubali asilani mpemba watawale kwa kufuatana.
Hata 2010 Dr. Shein kuingia ikulu ikiwa ni mpemba wa kwanza kuingia ikulu ya malindi wahafidhina hao wa kiunguja wana CCM kindakindaki waliandika kwenye mbao zao za Matangazo maskani kongwe ya CCM Kisonge unguja waliandika kwa maandishi makubwa wakisema "Hizbu wawili waingia ikulu" wakimaanisha wapemba Dr. Shein na Maalim Seif(makamu wa rais)
Shida ya Zanzibar ni upemba ma uunguja, huku waunguja wakijiona wao ndio wana milki ya Visiwa hivyo.
Pamoja na yote Dr. Hussein Mwinyi bado ni chaguo bora sana kumzidi Prof Mbarawa, Mbarawa ni kutoka jimbo la Mkanyageni pemba hajawahi hata siku moja kishinda nafasi ya Kuchaguliwa na Wananchi.
Alibwagwa na Eng. Habib Mnyaa wa CUF jimbo la Mkanyageni 2010.
Hii inaomuondolea confidence mbele za watu.
Dr. Hussein tayari ameshaanza kuandaliwa kunrithi Dr. Shein.
Dr. Hussein ni mtu muungwana sana asiye na makuu kama alivyo baba ake hakika "Embe halianguki mbali na mti wake".
Kila la heri Muungwana Dr. Hussein Mwinyi unastahili.