Kamwe usiolewe na mwanaume asiyeweza kukulipia mahari

khaa kumbe pm yako iko wazi? mbona pm yangu hujawahi kujibu[emoji44][emoji44][emoji44]
Sijawahi kuiona[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Hakuna mtu aliyewahi kunitumia message nisijibu..sina dharau hizo.
 
Saint Anne Hivi unafahamu kuwa mapenzi ya Wawili na wanayo yafanya huwa hayaingiliwi? Hivi unajua kuwa mwanaume kutolea mahari na mzazi au babu ni moja ya jukumu la mzazi kwa mila flani fani na makabila flani, hii ni jadi na mila za wengi sana labda kama ww umekulia sehem ambapo hujui mila zenu au ukoo wenu huwa ahmfanyi haya.
sasa iko hivi:
Mwanaume na mwanamke wanapo kutana huwa inategemea na namna walivyo kutana, wapo walio rubuniana kwa kuendeana kwa waganga ili mmoja ampate mwingine, na wapo ambao Neema ya mwenyezi Mungu iliwakutanisha ili waoane, wapo wengine ambao walikutana kwa tamaa ya mwanamke ilimradi naye aonekane tu kuwa ana mume na kujitoa kulazimisha mwanaume atoe mahari kwao.

1. Sasa ushauri unao utoa kwa wanawake sijui umezingatia nini hapo kati ya hivyo.
Niseme tu kwamba, kama Mungu alitoa neema ya kuwakutanisha Me na KE waoane yaliyomo huko ndani kwao haituhusu wote, maamuzi yao huko ndani haituhusu wote, pesa na mali ni zao wanajiamulia wenyewe bila hata ya ushauri wetu sisi, wataendelae kuyafanya yao wanayo yaona ni vema na muhimu.

2. Ndoa nyingi zina changamoto na wao huwa wanayatatua wenyewe kama wajuavyo na kwa misingi ya wao kukutana na kukubaliana kuoana, wote hawafanani kwenye utatuzi wa matatizo yao ndio maana unakuta wengine yanawashinda kabisa wanaamua kuachana na wenza wao, Mara nyingi wanaokutana na matatizo kwenye ndoa ni wale ambao misingi yao ni mibovu toka walivyokutana na kuamua kuoana. ila niseme tu kwamba mwanamke au mwanaume huwa anajua kusema samahani kwa mwenzie pale anapojitambua kuwa alichokifanya alikosea na maisha huwa inaendelea.

3. Mwanamke kuamua kumpa mwanaume mahari kwenda kutoa kwao kwanza inaweza ikawa mwanaume pesa hizo hana ila anacho kidogo ndio mke anampa ili aongeze, hii sio dharau, sio dhambi, sio kosa, na sio kuwa inavunja heshima hata kidogo, kuvunja heshima ni pale ambapo mwanamke ataonekana hana adabu na hajitambui kuwa maisha ya leo sio ya kesho, mkiwa wawili na mwili mmoja yote yaliyomo kwenu ni ya wote si ya mtu mmoja mnatafuta ili mlee familia na maisha yaende.

4. Mila ya wazazi kuwaowea wanaume hakuna anayeweza kuifuta au kuipinga, unaweza ukawa na pesa zako taslimu za kuoa ila mzazi atakwambia chukua na hiki uongeze ukatoe kama mahali, mtoto mwenye akili na hekima humshukuru sana mzazi wake na huchanganya mahali yote na kuipeleka kunakohusika kwa kutumia utaratibu wa makabila, labda kwenu haipo, ila kwa wengine lipo, au mwanaume huwa anaitwa na mzazi anaulizwa mwanangu una sh ngapi ili mahari itolewe, mwanaume huwa anajibu nina hata 200 baba huwa anaikubali na kuchanganya na mali zingine, kama hata iyo 200 hana kabisa baba huwa anamwambia usiwe na wasiwasi tutalimaliza mzazi antoa anachoweza na badae kilicho baki kijana atamalizia akipata.

Kwa kifupi ni kwamba mwanaume kupewa mahari na mwanamke kupeleka kwao itakuwa na matokea mazuri kuwa ni mbaya au ni vizuri kutokana na misingi ya mlivyokutana, mkakubaliana na mnavyoshibana, mwanamke kusikitika ni kwamba kuna makosa kwenye misingi ya wao kukutana na kukubaliana waoane, ila kama ni kwa neema ya mwenyezi Mungu na misingi iliyojengwa na Mungu hakuna majuto kammwe.

Kuhusu mwanaume kutolewa mahari na wazazi haishangazi, ni mila ipo toka enzi hizo za mababu lazima tujue hilo, na haikwepeki, kwa mlio ishi mjini huwa mnaona kama dharau ni vile hawaelewi utaratibu huu na misingi yake, ukitolewa mahali na wazazi haimanishi kuwa mwanamke atakuwa ni wa ukoo, huo ni uongo. utaratibu wa mila za wengine ni kuwa ukishaolewa lazima uende ukaishi kwanza na wakwe zako kwa muda flani na wakukabidhi jiko.... hili halimaanishi ni mke wa ukoo no.
UBARIKIWE
 
Kwa akili zako jinsi zilivyo humu na Kama ndizo hizo unazo basi ana hasara.

Stress nadhani utakuwa nazo wewe boss.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…