Kamwe usiolewe na mwanaume asiyeweza kukulipia mahari

Kumbe haujui dhumuni na malengo ya mahari, unaisi mahari ipo ili kulipa fidia kwa wazazi wako et?
 
Mimi si mpangaji wa mahari.

Kwa tamaduni za Kwetu mahari hutolewa mchanganyiko yaani pesa pamoja na vitu na wala si vitu pekee wala pesa pekee.

Mahari ya kawaida tu hutolewa.
Naweza nikataja kiwango hapa wewe ukakiona kikubwa na mwingine akakiona kidogo..kwahiyo ndogo kwa mwenzio yaweza kuwa kubwa kwako.

Mimi jinsi nilivyoona wanatoa
Kwa mfano wakisema ninyi ni wa kina nani??basi mshenga wa upande wa muoaji anaweka pale kiasi cha pesa...na halazimishwi kiasi,ni mfuko wake tu utakapoishia.

Huo utaratibu wa mwanamke kumchangia mwanaume mahari haupo kwenye Biblia,sijui labda huko kwenu.

Mwanamke hawi responsible kupanga mahari.
 
Kumbe haujui dhumuni na malengo ya mahari, unaisi mahari ipo ili kulipa fidia kwa wazazi wako et?
Wewe si ndo umeanza kusema wazazi wamefanya mitaji (wanawakomoa)

Ukishaanza kusema wazazi wanafanya mahari mtaji basi ujue hujui lengo la mahari.
 
Wewe si ndo umeanza kusema wazazi wamefanya mitaji (wanawakomoa)

Ukishaanza kusema wazazi wanafanya mahari mtaji basi ujue hujui lengo la mahari.
Kama utatoza mahari isiyo endana na hali halis ya maisha ya muoaji utasema hapo kama sio kumkomoa?
 
Mimi si mpangaji wa mahari.

Kwa tamaduni za Kwetu mahari hutolewa mchanganyiko yaani pesa pamoja na vitu na wala si vitu pekee wala pesa pekee.
Hizi tamaduni kandamizi sana, halafu hili bado mmelikalia kimya watetezi wa haki za Wanawake. Mwenye jukumu la kutaja Mahari na kupanga mahari ni muolewaji, sababu maana ya Mahari ni kama Zawadi tu.
Mahari ya kawaida tu hutolewa.
Naweza nikataja kiwango hapa wewe ukakiona kikubwa na mwingine akakioba kidogo..kwahiyo ndogo kwa mwenzio yaweza kuwa kubwa kwako.
Ndoa yenye baraka ni ile ambayo mahari yake ilikuwa ni ndogo. Mwanamke ndiyo mwenye haki ya kupanga mahari, na yeye anaweza kumfanyia wepesi yule anaye tarajia kumuoa kwa mapenzi na huruma akamtajia mahari nyepesi sana (Hapa kama ingekuwa una haki ya kupanga mahari, ila sisi huki kwetu suala la Mahari ni la muolewaji). Wapo watu walio oa kwa mahari ya Pete ya Chuma, namaanisha pete ya chuma.

Wapo walio oa kwa mahari thamani ya chini ya laki moja na wengine kitanda au mkufu wa dhahabu. Ndoa jambo sahali sana.
Mimi jinsi nilivyoona wanatoa
Kwa mfano wakisema ninyi ni wa kina nani??basi mshenga wa upande wa muoaji anaweka pale kiasi cha pesa...na halazimishwi kiasi,ni mfuko wake tu utakapoishia.
Huu utaratibu unaonaje ? Uko sawa au ? Kwanini isingekuwa wewe unae olewa ndiyo utaje mahari unayo itaka ?
Huo utaratibu wa kumchangia mwanaume mahari haupo kwenye Biblia,sijui labda huko kwenu.
Kwenye Biblia kuna utaratibu gani juu ya Mahari, unaweza kutupa muongozo juu ya utolewaji wa mahari kwa mujibu wa Biblia ?
Mwanamke hawi responsible kupanga mahari.
Kwanini ? Kwa mujibu tamaduni zenu au kwa mujibu wa Biblia ? Kati ya Biblia na Tamaduni kipi unakiangalia sana na kukitanguliza dhidi ya kingine ?
 
Kama utatoza mahari isiyo endana na hali halis ya maisha ya muoaji utasema hapo kama sio kumkomoa?
Mnataka wawape bure au mnatakaje??
Mahari zinazotozwa Mbona ni za kawaida au nyie mnataka mtoe kuku mmoja basi muopoe mke?
 
Mnataka wawape bure au mnatakaje??
Mahari zinazotozwa Mbona ni za kawaida au nyie mnataka mtoe kuku mmoja basi muopoe mke?
Ww ni wa ukanda wa pwani inavyo onekana et? Ebu njoo kanda nyingne uone mahari zake ndio utajua uliyotolewa ww sio sawa na wanyo ambiwa wenzio
 
Yaani umeuliza maswali nimekujibu unaniambia tena kwanini??we vipi?
Au ulitaka majibu gani??

Umeuliza Mimi mahari yangu nikiambiwa nitaje nitataja kiasi gani nikakujibu kwamba Mimi si mpangaji wa mahari.

Umeuliza kuhusu Biblia kuhusu kumchangia mwanaume mahari nimekujibu halafu unaanza kuniuliza maswali tena.
Kama ulikuwa na majibu yako basi usingeniuliza.

Kasome Biblia utaona kila kitu kuhusu mahari,usisubiri nikusomee.

Utaratibu upo sawa tu,kama wewe unaona si sawa basi wenyewe tunaona upo sawa.

Wazazi siyo wapumbavu kiasi hicho waanze kutaja hela zisizolipika..kwahiyo acha kuwavalisha roho mbaya.
Nyie kama binti ndo mpangaji Basi jua kwetu binti si si mpangaji wa mahari.
Anayemlea binti ni wazazi na si yeye anayejilea.
 
Ww ni wa ukanda wa pwani inavyo onekana et? Ebu njoo kanda nyingne uone mahari zake ndio utajua uliyotolewa ww sio sawa na wanyo ambiwa wenzio
Si mtu wa pwani Mimi mkuu.
Ukanda gani huo nije nione?
 
Akhsante[emoji122][emoji122][emoji122]

Sielewi niliipita vipi hii comment jamani[emoji1751]
 
Kwani maana halisi ya Mahari ni nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…