Hizi tamaduni kandamizi sana, halafu hili bado mmelikalia kimya watetezi wa haki za Wanawake. Mwenye jukumu la kutaja Mahari na kupanga mahari ni muolewaji, sababu maana ya Mahari ni kama Zawadi tu.
Ndoa yenye baraka ni ile ambayo mahari yake ilikuwa ni ndogo. Mwanamke ndiyo mwenye haki ya kupanga mahari, na yeye anaweza kumfanyia wepesi yule anaye tarajia kumuoa kwa mapenzi na huruma akamtajia mahari nyepesi sana (Hapa kama ingekuwa una haki ya kupanga mahari, ila sisi huki kwetu suala la Mahari ni la muolewaji). Wapo watu walio oa kwa mahari ya Pete ya Chuma, namaanisha pete ya chuma.
Wapo walio oa kwa mahari thamani ya chini ya laki moja na wengine kitanda au mkufu wa dhahabu. Ndoa jambo sahali sana.
Huu utaratibu unaonaje ? Uko sawa au ? Kwanini isingekuwa wewe unae olewa ndiyo utaje mahari unayo itaka ?
Kwenye Biblia kuna utaratibu gani juu ya Mahari, unaweza kutupa muongozo juu ya utolewaji wa mahari kwa mujibu wa Biblia ?
Kwanini ? Kwa mujibu tamaduni zenu au kwa mujibu wa Biblia ? Kati ya Biblia na Tamaduni kipi unakiangalia sana na kukitanguliza dhidi ya kingine ?