Kamwe usiolewe na mwanaume asiyeweza kukulipia mahari

Kamwe usiolewe na mwanaume asiyeweza kukulipia mahari

Hakuna hela inayoweza kulipa gharama walizotumia wazazi wetu kutulea..haipo!!!

Na hiyo hela ya mahari na baadhi ya vitu ni Akhsante tu!
Kama vyombo wazazi wanavyo,mashati vitenge ndo usiseme.

Vijana kuto kuoa ni uoga wao tu na fikra potofu.
Hakuna familia inayopanga kumkomoa mtoto wa kiume anayeenda kuoa.
Haipo!.
Kumbe haujui dhumuni na malengo ya mahari, unaisi mahari ipo ili kulipa fidia kwa wazazi wako et?
 
Naomba nikuulize swali bibie, kisha nitasema jambo.

Wewe ungependa mahari yako iwe pesa taslimu au kitu fulani ? Kama pesa Taslimu isiwe chini ya kiasi gani ? (Ukijibu maswali haya kuna udhia nitakwambia)

Kwani kwenye Biblia yenu, kuna sehemu iliyo kataza mume kusaidiwa kulipa mahari au kukopeshwa kwa ajili ya kulipia mahari ?

Je kwenye Biblia kumetajwa kiwango maalumu cha mahari ?

Kibwagizo
Kuna sehemu nyinyi wanawake mnakosea pindi mnapo taja mahari zenu,wengine huwa mnataka mlipiwe mahari kama mtu anaoa ukoo mzima (Samahani lakini huu mfano tu)

Namalizi "al Qasus" kisha narudi.
Mimi si mpangaji wa mahari.

Kwa tamaduni za Kwetu mahari hutolewa mchanganyiko yaani pesa pamoja na vitu na wala si vitu pekee wala pesa pekee.

Mahari ya kawaida tu hutolewa.
Naweza nikataja kiwango hapa wewe ukakiona kikubwa na mwingine akakiona kidogo..kwahiyo ndogo kwa mwenzio yaweza kuwa kubwa kwako.

Mimi jinsi nilivyoona wanatoa
Kwa mfano wakisema ninyi ni wa kina nani??basi mshenga wa upande wa muoaji anaweka pale kiasi cha pesa...na halazimishwi kiasi,ni mfuko wake tu utakapoishia.

Huo utaratibu wa mwanamke kumchangia mwanaume mahari haupo kwenye Biblia,sijui labda huko kwenu.

Mwanamke hawi responsible kupanga mahari.
 
Kumbe haujui dhumuni na malengo ya mahari, unaisi mahari ipo ili kulipa fidia kwa wazazi wako et?
Wewe si ndo umeanza kusema wazazi wamefanya mitaji (wanawakomoa)

Ukishaanza kusema wazazi wanafanya mahari mtaji basi ujue hujui lengo la mahari.
 
Wewe si ndo umeanza kusema wazazi wamefanya mitaji (wanawakomoa)

Ukishaanza kusema wazazi wanafanya mahari mtaji basi ujue hujui lengo la mahari.
Kama utatoza mahari isiyo endana na hali halis ya maisha ya muoaji utasema hapo kama sio kumkomoa?
 
Mimi si mpangaji wa mahari.

Kwa tamaduni za Kwetu mahari hutolewa mchanganyiko yaani pesa pamoja na vitu na wala si vitu pekee wala pesa pekee.
Hizi tamaduni kandamizi sana, halafu hili bado mmelikalia kimya watetezi wa haki za Wanawake. Mwenye jukumu la kutaja Mahari na kupanga mahari ni muolewaji, sababu maana ya Mahari ni kama Zawadi tu.
Mahari ya kawaida tu hutolewa.
Naweza nikataja kiwango hapa wewe ukakiona kikubwa na mwingine akakioba kidogo..kwahiyo ndogo kwa mwenzio yaweza kuwa kubwa kwako.
Ndoa yenye baraka ni ile ambayo mahari yake ilikuwa ni ndogo. Mwanamke ndiyo mwenye haki ya kupanga mahari, na yeye anaweza kumfanyia wepesi yule anaye tarajia kumuoa kwa mapenzi na huruma akamtajia mahari nyepesi sana (Hapa kama ingekuwa una haki ya kupanga mahari, ila sisi huki kwetu suala la Mahari ni la muolewaji). Wapo watu walio oa kwa mahari ya Pete ya Chuma, namaanisha pete ya chuma.

Wapo walio oa kwa mahari thamani ya chini ya laki moja na wengine kitanda au mkufu wa dhahabu. Ndoa jambo sahali sana.
Mimi jinsi nilivyoona wanatoa
Kwa mfano wakisema ninyi ni wa kina nani??basi mshenga wa upande wa muoaji anaweka pale kiasi cha pesa...na halazimishwi kiasi,ni mfuko wake tu utakapoishia.
Huu utaratibu unaonaje ? Uko sawa au ? Kwanini isingekuwa wewe unae olewa ndiyo utaje mahari unayo itaka ?
Huo utaratibu wa kumchangia mwanaume mahari haupo kwenye Biblia,sijui labda huko kwenu.
Kwenye Biblia kuna utaratibu gani juu ya Mahari, unaweza kutupa muongozo juu ya utolewaji wa mahari kwa mujibu wa Biblia ?
Mwanamke hawi responsible kupanga mahari.
Kwanini ? Kwa mujibu tamaduni zenu au kwa mujibu wa Biblia ? Kati ya Biblia na Tamaduni kipi unakiangalia sana na kukitanguliza dhidi ya kingine ?
 
Kama utatoza mahari isiyo endana na hali halis ya maisha ya muoaji utasema hapo kama sio kumkomoa?
Mnataka wawape bure au mnatakaje??
Mahari zinazotozwa Mbona ni za kawaida au nyie mnataka mtoe kuku mmoja basi muopoe mke?
 
Mnataka wawape bure au mnatakaje??
Mahari zinazotozwa Mbona ni za kawaida au nyie mnataka mtoe kuku mmoja basi muopoe mke?
Ww ni wa ukanda wa pwani inavyo onekana et? Ebu njoo kanda nyingne uone mahari zake ndio utajua uliyotolewa ww sio sawa na wanyo ambiwa wenzio
 
Hizi tamaduni kandamizi sana, halafu hili bado mmelikalia kimya watetezi wa haki za Wanawake. Mwenye jukumu la kutaja Mahari na kupanga mahari ni muolewaji, sababu maana ya Mahari ni kama Zawadi tu.

Ndoa yenye baraka ni ile ambayo mahari yake ilikuwa ni ndogo. Mwanamke ndiyo mwenye haki ya kupanga mahari, na yeye anaweza kumfanyia wepesi yule anaye tarajia kumuoa kwa mapenzi na huruma akamtajia mahari nyepesi sana (Hapa kama ingekuwa una haki ya kupanga mahari, ila sisi huki kwetu suala la Mahari ni la muolewaji). Wapo watu walio oa kwa mahari ya Pete ya Chuma, namaanisha pete ya chuma.

Wapo walio oa kwa mahari thamani ya chini ya laki moja na wengine kitanda au mkufu wa dhahabu. Ndoa jambo sahali sana.

Huu utaratibu unaonaje ? Uko sawa au ? Kwanini isingekuwa wewe unae olewa ndiyo utaje mahari unayo itaka ?

Kwenye Biblia kuna utaratibu gani juu ya Mahari, unaweza kutupa muongozo juu ya utolewaji wa mahari kwa mujibu wa Biblia ?

Kwanini ? Kwa mujibu tamaduni zenu au kwa mujibu wa Biblia ? Kati ya Biblia na Tamaduni kipi unakiangalia sana na kukitanguliza dhidi ya kingine ?
Yaani umeuliza maswali nimekujibu unaniambia tena kwanini??we vipi?
Au ulitaka majibu gani??

Umeuliza Mimi mahari yangu nikiambiwa nitaje nitataja kiasi gani nikakujibu kwamba Mimi si mpangaji wa mahari.

Umeuliza kuhusu Biblia kuhusu kumchangia mwanaume mahari nimekujibu halafu unaanza kuniuliza maswali tena.
Kama ulikuwa na majibu yako basi usingeniuliza.

Kasome Biblia utaona kila kitu kuhusu mahari,usisubiri nikusomee.

Utaratibu upo sawa tu,kama wewe unaona si sawa basi wenyewe tunaona upo sawa.

Wazazi siyo wapumbavu kiasi hicho waanze kutaja hela zisizolipika..kwahiyo acha kuwavalisha roho mbaya.
Nyie kama binti ndo mpangaji Basi jua kwetu binti si si mpangaji wa mahari.
Anayemlea binti ni wazazi na si yeye anayejilea.
 
Ww ni wa ukanda wa pwani inavyo onekana et? Ebu njoo kanda nyingne uone mahari zake ndio utajua uliyotolewa ww sio sawa na wanyo ambiwa wenzio
Si mtu wa pwani Mimi mkuu.
Ukanda gani huo nije nione?
 
Kulipiwa mahari na mwanamke huo ni upuuzi grade A. Ndo matokeo yake unaanza kupapaswa matter call kwenye mahusiano.... Hilo TUNAKUBALIANA

hilo la pili la mahari kutoka kwa wazazi ni mambo ya mila. Sisi kabila letu ng’ombe wa mahari lazima atole kwenye boma la baba sio la kwako

Vivyo hivyo na kuna maneno pale mshua anayasema anavyokukabidhi kwamba kama nilivyokuozesha wewe na wewe una jukumu la kuwalipia wanao mahari ukoo wetu ukue. So ni mambo ya taratibu tu. Ndomaana hata vikao vya kupanga mahari bwana harusi haihusiki, na pia kutokana na changamoto za kiuchumi unamkabidhi baba mahari ndo anayeenda kukutolea kama zake(Kama mshua apeche lolo)

NB: vyovyote iwavyo point yako bado inahold, kama mwanamke akiona mume/baba watoto mtarajiwa hana hata uwezo wa kujilipia mahari manaake ni kwamba huo uzao wenu watashindwa hata kuoa nao(Ni jukumu lake). na kikwetu unatengwa na wanaume wenzako hata pombe kilabuni unakunywa kwenye kibuyu cha kwako,sio cha wazee wote sumtym hata viboko utachapwa
Akhsante[emoji122][emoji122][emoji122]

Sielewi niliipita vipi hii comment jamani[emoji1751]
 
Kamwe usiolewe na mwanaume ambaye hawezi kukulipia mahari. Sikuwahi kuona kwenye Biblia mwanaume aliyepewa mke bure.

Tena wengine mnajifanya kupenda sana, unalazimisha kuolewa na mwanaume ambaye hawezi kukulipia mahari. Wengine mnaenda mbali zaidi na kuwasaidia kulipa hizo mahari.

Ukiona umemsaidia kulipa mahari usishangae na huko ndani akakuachia majukumu yote ya familia.

Kama unampenda msaidie mambo mengine lakini ikifika muda wa kulipa mahari hiyo ngoma mwache aicheze mwenyewe, ikimshinda basi huyo hakufai.

Kwanini hakufai??

Hakufai kwa sababu suala la kuoa siyo surprise ni suala la kujiandaa. Kama mchumba ameweza kununua mahitaji yake yote, atashindwaje kukulipia mahari!?!

Binti nakwambia usije thubutu kujifanya unamsaidia mwanaume kulipa mahari, hilo ni lake. Ukimpa mahari ujue umejioa mwenyewe dada.

Na wale vijana mnaolipiwa mahari na wazazi wenu pia siwaelewi jamani. Usije ukashangaa mke anakuwa wa ukoo, wao ndiyo wanamcontrol na hauwezi kufanya jambo bila wao.

Na
Winnie Kilemo
Kwani maana halisi ya Mahari ni nini?
 
Back
Top Bottom