Kamwe usiolewe na mwanaume asiyeweza kukulipia mahari

Na wengi wanaojilipia mahari ndoa zimewatokea puani, wameishiwa kuuliwa tu, na kuteswa Hadi kuachwa walemavu, mwanaume asiyeweza kutoa mahari na asioe kabisa aisee mpaka awe vizuri
Wanawake wengine hawahitaji mahari ili waolewe ..ukionesha nia kwao inatosha
 
Ni kweli kabisa Mkuu, alieonja na kusepa na yule aliyejisalimisha kwa wazazi wa binti mikono mitupu yupi mwenye hekima?
Ukiona mzazi anamzuia binti ye kuolewa kisa hakuna mahari Mkuu huyo achana nae kimbia kabisa usirudi tena hapo, manake utakufa kabla ya wakati wako.
 
tulipe mahari kulingana na uwezo wetu wakuu
ukiitishwa mahari ya mbuzi au kuku usiweke sifa
 
Kwani hao Wazee ndiyo wanolewa mpaka wapange Mahari yako!? Je Kati ya wwe na Wazee wako nani anamjua vizuri huyo muowaji!?
Hiyo Akhsante wanapewa wazee wala hapewi mwali.
 
Endelea kujisalimisha mikono mitupu
 
Ili iweje?
Ataambiwa atakayekuja kutoa.
Mimi kama kaka yako wa hiari siungi mkono matendo yote yanayodhalilisha na kushusha thamani ya dada zangu ikiwa ni pamoja na mambo ya mahari.Nakushauri acha kuunga mkono matendo hayo na anza kuyapiga vita kwa nguvu zote
 
Endelea kujisalimisha mikono mitupu
Kwa mtazamo wangu swala la kuishi mke na mume ni swala pana sana kikubwa huwa ni upendo na furaha, kuna vijana hawana hizo mahari pia wametoka familia zisizo na plan nzuri(duni) lakini wana upeo wa Maisha, Pia wapo watakao kutolea mahari lakini ukishaingia kwenye ndoa utajuta.
Kikubwa Maisha hayana formula, wazazi wanaoona mahari ni big deal kijana kimbiaaaa utajuta.
 
Mahari iko palepale
Furaha na amani na mengine yote uliyoyasema yako palepale.
 
Mimi kama kaka yako wa hiari siungi mkono matendo yote yanayodhalilisha na kushusha thamani ya dada zangu ikiwa ni pamoja na mambo ya mahari.Nakushauri acha kuunga mkono matendo hayo na anza kuyapiga vita kwa nguvu zote
Pole sana

Au mnataka na nyie mtolewe mahari??
Mngezaliwa wanawake basi
 
Mahari iko palepale
Furaha na amani na mengine yote uliyoyasema yako palepale
Nakubaliana na wewe endapo tu pale binti anayekazaniwa iwe isiwe lazima atolewe mahari, naye lazima awe kigori hajaguswa kabisa na mabaharia hapo ni sawa hata wakisema ng`ombe mia ni sawa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…