Kamwe usiolewe na mwanaume asiyeweza kukulipia mahari

Kamwe usiolewe na mwanaume asiyeweza kukulipia mahari

Yupo aliyewahi kuolewa kwa ubeti wa shairi???
Atakuwa hajitambui haki ya nani
Unasemaje kwa aliyeolewa kwa mahari ya biblia. Yaani jamaa baada ya kulipa mahari baba mkwe akiachikua akaindaika majina ya mume na mke na kuwarudishia kama zawadi. Technically jamaa alioa bila mahari je hii ndoa ni batili kwa mawazo ya hili bandiko hapa?
 
Winnie Kilemo kuna vitu huwa anaandika huko facebook hadi namwonea huruma,,,, wakati flani namwona kama mtu aliyekaa kwenye wokovu miaka mingi ila ni mchanga kwenye mambo ya kiroho (kifalme)

mi nadhani angeaza kwa kushauri wazazi kutopanga mahari kubwa sana , au angeshauri mabinti wanaoposwa wawambie wazazi wao kwamba mtarajiwa wangu hana uwezo kwaio msipange mahari kubwa!

anyway, ukitumia biblia, anaetakiwa kulipiwa mahari ni binti kigori tu. ndivyo torati inavyoeleza. ukikuta sio kigori warudishie wenye mtoto nao warudishe mahari!
Mbavu zangu 😂 😂 😂
 
Mahari is overrated, mahari kwa dunia ya sasa haina maana yoyote. Kwani zamani walitoa mahari kwa sababu zipi, I thought ni asante kwa wazazi kimtunza binti yao hadi anaolewa akiwa kigori(kigoli).

Leo unaoa mke wa watu huko, walishajitwalia wengi kabla yako wewe unakuja kuhalalishwa tu na kujibebea, kuongeza laana katika uzao wako.

Mahari for the purity nakubali, Ila kwa sisi tuliojiharibu, sioni mantiki hata kidogo.
Nakazia
 
Jacob alichunga Mifugo miaka mingi tu.....ili aoe,
Labban( kama sijakosea) akampa Dada wa binti aliyekusudiwa, Jacob akasema anamtaka chaguo lake lile lile,
Akaambiwa achunge tena mifugo ili apewe huyo anayemtaka.
Jumla ya miaka unaweza fika 10, alitumia kuchunga mifugo ili aoe.
Hii ni adhabu tosha.
Aisee hiii ni zaidi ya adhabu tosha mamaeee 😂 😂 😂 😂
 
Sijakataa kwamba ni utamaduni.

Kuwa utamaduni hakuondoi ukweli kwamba ni utamaduni unaomfanya mwanamke kuwa bidhaa.

Na kuna watu wakiona bidhaa haifai, wakimpa mwanamke talaka, wanadai sehemu ya mahari waliyolipa.

Huko Africa hususan, kitu kuwa utamaduni haimaanishi ni kizuri.

Kuna sehemu nyingi bado wanawake wanakatwa visimi kwa minajili ya utamaduni. Huu ni utamaduni, lakini si mzuri.

Ukisoma tamaduni za Africa, kihistoria, mwanamke na mtoto ni kama mali za mwanamme tu.

Na ndiyo maana machifu walikuwa na wake wengi, watoto wengi. Ni alama ya utajiri.

Na kwa kuwa mwanamke ni bidhaa kwa tamaduni hizi, basi anawekewa bei rasmi.

Na bei hiyo inaitwa mahari.

Jamii yenye mahari haiwezi kuwa na usawa wa watu.

Anayelipa mahari, ceteris paribus, atajiona yuko juu kwenye ndoa.

Ukikubali mahari na kusema mwanamke ni mtumwa wa mwanamme, sina tatizo nawe.

Ukikubali mahari na kusema mwanamke ni sawa na mwanamme kiutu, hapo naona kuna uongo.

Kwa sababu kama mahari ni utamaduni wa zawadi tu, kwa nini familia ya mwanamme haipewi zawadi ikawa mwanamme anatoa mahari kwa mwanamke na mwanamke anatoa mahari kwa mwanamme? Mahari iwe exchange of gifts tu?

After all, reciprocity is the height of diplomacy and love.

Mahari ni bei ya kununua mke.

Inawezekana ni kitu muhimu katika jamii masikini, kuzuia watu masikini wasioweza ku maintain family kuoa.

Lakini, kwenye jamii zilizovuka mto huo, boti hilo halihitajiki.

Ndiyo maana jamii zilizoendelea kielimu na kiuchumi zimeondokana na utamaduni huu.

Lakini labda huko Africa tunauhitaji bado.

Hayo yote hayabadilishi ukweli kwamba mahari ni bei ya kununua mke kama bidhaa.
Kiranga baba.
Nilitaka tu kukusalimia.
Siku nyingi sana.
Nimefurahi uko mzima.
 
Wahindi mwanamke ndie anaetoa mahari! Imekaaje! Hakuna anaestahili kulipa mahari, wote wametunzwa na wazazi wao. Ni kiasi tu cha kuachana na wazazi na kuambatana na mpendwa wako. Shukrani zitoka kwa pande zote mbili
Well said ..inashangaza sana ati shukurani kwa wazazi kumtunza binti kwani mtoto wakiume alilelewa mtaani (chokoraa)mbona wazazi wao hawapewi shukurani !?? Hii mifumo mingine ya kipuuzi sijui ililetwa na nani duniani
 
Sijakataa kwamba ni utamaduni.

Kuwa utamaduni hakuondoi ukweli kwamba ni utamaduni unaomfanya mwanamke kuwa bidhaa.

Na kuna watu wakiona bidhaa haifai, wakimpa mwanamke talaka, wanadai sehemu ya mahari waliyolipa.

Huko Africa hususan, kitu kuwa utamaduni haimaanishi ni kizuri.

Kuna sehemu nyingi bado wanawake wanakatwa visimi kwa minajili ya utamaduni. Huu ni utamaduni, lakini si mzuri.

Ukisoma tamaduni za Africa, kihistoria, mwanamke na mtoto ni kama mali za mwanamme tu.

Na ndiyo maana machifu walikuwa na wake wengi, watoto wengi. Ni alama ya utajiri.

Na kwa kuwa mwanamke ni bidhaa kwa tamaduni hizi, basi anawekewa bei rasmi.

Na bei hiyo inaitwa mahari.

Jamii yenye mahari haiwezi kuwa na usawa wa watu.

Anayelipa mahari, ceteris paribus, atajiona yuko juu kwenye ndoa.

Ukikubali mahari na kusema mwanamke ni mtumwa wa mwanamme, sina tatizo nawe.

Ukikubali mahari na kusema mwanamke ni sawa na mwanamme kiutu, hapo naona kuna uongo.

Kwa sababu kama mahari ni utamaduni wa zawadi tu, kwa nini familia ya mwanamme haipewi zawadi ikawa mwanamme anatoa mahari kwa mwanamke na mwanamke anatoa mahari kwa mwanamme? Mahari iwe exchange of gifts tu?

After all, reciprocity is the height of diplomacy and love.

Mahari ni bei ya kununua mke.

Inawezekana ni kitu muhimu katika jamii masikini, kuzuia watu masikini wasioweza ku maintain family kuoa.

Lakini, kwenye jamii zilizovuka mto huo, boti hilo halihitajiki.

Ndiyo maana jamii zilizoendelea kielimu na kiuchumi zimeondokana na utamaduni huu.

Lakini labda huko Africa tunauhitaji bado.

Hayo yote hayabadilishi ukweli kwamba mahari ni bei ya kununua mke kama bidhaa.
Well said indeed kongole sana mkuu
 
Hayo ya kuumbwa kwa ulimwengu umehadithiwa tu kama sehemu ya stories za mfumodume.

Unaelewa story ya Adam ni ya Wayahudi tu.

Wachina, Wajapan, Wahindi, Waafrika wanaojitambua, hawamtammbui Adam kama mtu wa kwanza?

Unaelewa story ya Adam sehemu nyingi ndiyo iliyopandikiza mfumodume uliomkandamiza mwanamke mpaka akawa bidhaa mpaka leo?

Jibu lako halipingi hoja yangu.

Jibu lako linaiongezea nguvu hoja yangu.
Hahahaha sure indeed
 
Yupo aliyewahi kuolewa kwa ubeti wa shairi???
Atakuwa hajitambui haki ya nani
Saint hu mtazamo wako unaishia katika hizi nchi za mataifa ya africa mashariki ambazo zimeapply mafundisho ya waislam na wakristo na kuyageuza kuwa utaratibu wamaisha yao .hiki unachokiamini wewe na watu wengine wenye imani sawa na yako haimanishi kwamba ndio mtazamo sahihi kwa watu wote wa dunia nzima .. Kuna watu wengine wapo hapa hapa east africa lakini Imani zao hazifungamani katiKa yale ambayo unayaamini wewe na wenzako wanaamini katika desturi zao na mambo yao maisha yao yanasonga .... Itoshe tu kusema kwamba dunia ni pana na kila watu wana taratibu zao so tusilazimishe mitazamo yetu kuweza kufanana ....

Ila kwa upande wangu still ninaona kabisa kuwa hili suala la mtoto wakike kulipiwa mahari linazidi kumkandamiza nakumfanya awe mtumwa wa mtoto wa kiume
 
Back
Top Bottom