Kamwe usithubutu kutafuta maisha mikoani, utakosa hadi nauli ya kurudi Dar!

Kamwe usithubutu kutafuta maisha mikoani, utakosa hadi nauli ya kurudi Dar!

Nilienda iringa nilikaa kwa muda wa wiki moja, ile narudi zangu Dar nashangaa naambiwa mbona umefubaa umekuwa mweusi
Nikasema je ningekaa mwaka si ningechakaa au wangenisahau.
 
Kweli mkuu, nimwkuja kigoma nina wiki ya tatu lakini naona kabisa nimechakaa[emoji28]
 
Mikoani hivi dar hampo mikoani ni jiji nilisahau aisee kama nao ni mkoa,,kwamba wasije mikoani[emoji1787][emoji16]
 
Broooh, sawa tu. Nimekubali naishi mkoani... ila sisi wa mikoani ndio tutakuzika ujue?
Huko kwenu yamejaa majambazi acha niendelee kuishi hukuhuku.
ahahahahaha Sis, I miss you so much!! Dar pakichovu sana, pachafuuu bora Mkoani kwakweli
 
Bora msema kweli kuliko kuwa mnafiki. Kijana unaye jitafuta usije jaribu kufungasha mizigo kwenda kutafuta maisha huko mikoani, watu wa mikoani ni wabinafsi, roho mbaya, majungu na fitna.

Kijana ukiwa Dar una 85% za kutoboa hapa town, kapuku muuza maji leo mtafute baada muda utamkuta mbali sana, kikubwa creativity na flexibility tu kwenye kazi.

Dar ni hub ya domestic and multilateral companies zote hapa nchini, so fursa yoyote iwe vibarua ajira inaanzia hapa.

Soko la mazao ya wakulima wote wa huko mikoani mwao lipo hapa Dar, infrastructure facilities zote zipo hapa town.

NB: Ukitaka ufubae na uchakae vibaya kajichanganye huko mikoani kwakina Mwakarobo, Mabula Mabele nk, uone utakavyo pigwa vimbola.
Dar kuna vijana wengi kazi zao kusifia mali za watu huku wao hela yao ikishia kwenye nauli na kula na kodi ya nyumba tu
 
Back
Top Bottom