Rula ya Mafisadi
JF-Expert Member
- Dec 28, 2024
- 404
- 852
Allahmdulillah!
Nilipata heshima ya kuhudumu kwenye nafasi mbalimbali za chama chetu kuanzia nyumbani Mkuranga, kisha Uenyekiti wa Mkoa wa Pwani. Niliiongoza Kanda ya Pwani kwa miaka mitano wakati wa mawimbi makali ya mwendazake, na nikahudumu katika Kamati Kuu ya Chama kwa miaka 5.
Kwa uzoefu huo, nafikiri nimejifunza kwa kiasi kikubwa kuwajua vyema viongozi wetu, kuelewa changamoto zetu, na kushuhudia fursa zilizopo kwa ajili ya maendeleo ya chama chetu.
Ili chama chetu kiendelee kuwa na nafasi ya kuaminika na kuleta tija kwa jamii tunayoihudumia, na ili kufanikisha kiu yetu ya mabadiliko tunayoyapigania kwa zaidi ya miaka 30, *_naamini sasa ni wakati muafaka wa kufanya MABADILIKO YA UONGOZI. Tunapaswa kuishi kile tunachohubiri na kuonyesha mfano wa utendaji wenye dira na ufanisi
Kwa dhati kabisa, naamini Tundu Antipas Lissu ndiye anayestahili kuwa nahodha wetu mkuu katika kipindi hiki.
Ze Mwenyekitiz,
Baraka Mwago
Mwenyekiti Mstaafu wa Mkoa wa Pwani na Kanda ya Pwani.
Jumapili December 29, 2024
Mfurumwambao, Mkuranga.