Kuna tatizo kubwa sana kwa ma binti kuolewa au kuuza katika umri mdogo. Kwanza hajaandaliwa kimakuzi kuweza kulea mimba, hana elimu ya kutosha ya uzazi, hawajajiandaa kiuchumi nk matokeo yake ni kuzaa watoto wenye utapia mlo ambayo inapelekea udumavu wa akili. Udumavu wa akili ni tatizo kubwa kitaifa kwa sasa kwa sababu unapelekea kuwa na jamii mzigo. Jamii inakuwa mzigo kwa sababu haina uwezo mkubwa wa kiakili wa kufikiri na kutatua changamoto nyingi za maisha. Jamii mzigo inategemea eti viongozi ndiyo watawaletea maendeleo mpaka kwenye kaya zao. Sasa hivi kwa mfano kuna ukame na maji hakuna, sasa jamii mzigo badala ya kufikiria waitane wawili watatu majirani wauze mfugo mmoja mmoja au miwili, ili wachimbe walau kisima cha kawaida wapate maji, au kipindi cha mvua waitane kitongojini kwao wachimbe lambo lao dogo la maji liwasaidie wakati wa kiangazi, wao pesa wabaenda kunywea na kuongea wake (vibinti vya miaka 15) huku wanasubiri serikali. Jamii mzigo mama mjazimzito haendi clinic mapema mpaka mimba inafika miezi 5 au zaidi. Na akienda akipewa vile vidonge vya wajawazito hawamezi wanatupa kwa kukosa elimu. Mtoto akizaliwa na matatizo kama vichwa vikubwa au mgongo wazi wao wanakimbilia kusema kalogwa. Kwa ujumla hii jamii mzigo ndiyo inayoburuzwa sana na wanasiasa kwa kupewa ahadi hewa na kulishwa propaganda za hovyo mpaka wakati mwingine wanauwana wenyewe kwa wenyewe kwa sababu ya tofauti za kisiasa. Jamii mzigo uwezo wa kufikiri na kuleta mabadiliko ni mdogo sana.