Kanda za Ziwa Ukiitoa Mwanza, mikoa iliyobaki ipo nyuma sana kimaendeleo, Tatizo ni la serikali?

Kanda za Ziwa Ukiitoa Mwanza, mikoa iliyobaki ipo nyuma sana kimaendeleo, Tatizo ni la serikali?

round kick

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2025
Posts
933
Reaction score
3,051
Kanda ya Ziwa ukiitoa Mwanza mikoa iliybaki inatia huruma, kuna Poverty kubwa.

KAGERA
GEITA
MARA
SIMIYU
SHINYANGA

Maendeleo ni raia kuweza kumudu life sehemu walipo, huduma za kijamii, miradi ya serikali, n.k. kwa kigezo hiki hata mikoa ya Rukwa na Ruvuma wana nafuu.

Najua kuna watu mtaleta takwimu za kipato cha mtu moja moja za mikoa, hizi takwimu zinaweza kuonesha baadhi ya mikoa ya kanda ya ziwa wapo vizuri lakini hiki sio kipimo kizuri kwasababu hesabu zinazofanyika ni kuchukua mapato yote ya mkoa halafu unagawanywa kwa idadi ya watu wote mpaka watoto wachanga, na ukiangalia mikoa ya kanda ya ziwa kuna rasilimali kama madini lakini wanufaika wakubwa ni makampuni ya nje, hizo pesa zinazopatikana ndizo zinagawanywa na idadi ya watu wote wa mkoa. hiki sio kipimo kizuri.
 
Regional imbalance.
Mwanza imeendelea kuliko mikoa mingine kwenye kanda ya ziwa kutokana na utalii. Ukiangalia Bismarck rocks zipo Mwanza na pia Ziwa Victoria kwa sehemu kubwa ipo Mwanza kwahiyo uwekezaji mkubwa umefanyika Mwanza kutokana na geographical location yake. Ukiangalia mkoa kama Mara hautambuliki kwa chochote zaidi ya wakurya na nyumbani kwa baba wa taifa.
 
Kanda ya Ziwa ukiitoa Mwanza mikoa iliybaki inatia huruma,

KAGERA
GEITA
MARA
SIMIYU
SHINYANGA
Hapa ni JF, uwe unaenda na takwimu sio maneno makavu. Sasa anzia hapa hoja yako
F8OM9LYWcAAZiQ8.jpeg
 
Hapa ni JF, uwe unaenda na takwimu sio maneno makavu. Sasa anzia hapa hoja yako
View attachment 3304297
Hizo tathmini hazina ukamilifu

Kipato cha Mtu Mmoja Mmoja ni wastani wa mapato yote ya mkoa, yanayogawanywa kwa idadi ya watu wa eneo hilo (wakiwamo watoto wachanga).

Mikoa ya kanda ya ziwa kuna rasilimali kama Dhahabu na Almasi lakini wanufaika ni makampuni ya nje yanayoingiza pesa nyingi zinazoenda kugawanywa na idadi ya watu wa huo mkoa.

Mkoa kama Rukwa hauna rasilimali nyingi lakini angalau watu wana hali nzuri kimaisha, kuna miradi na maendeleo na huduma za kijamii.

Hicho kipimo ulichoweka kina mipaka yake, Bakhresa akihamia kijiji choka mbaya ukitumia hizo hesabu kijiji kitaonekana watu wake wanajiweza kwasababu ya pesa za Bakhresa
 
Hizo tathmini hazina ukamilifu

Mkoa kama Rukwa hauna rasilimali nyingi lakini angalau kuna miradi na maendeleo kwenye miji

Ukienda mikoa ya kanda ya ziwa maendeleo yanapimwa kwenye rasilimali mfano Dhahabu na Almasi lakini wanufaika ni makampuni ya nje
Weka takwimu zenye ukamilifu, sio maneno. Takwimu hipingwa kwa takwimu
 
Hizo tathmini hazina ukamilifu

Mkoa kama Rukwa hauna rasilimali nyingi lakini angalau kuna miradi na maendeleo kwenye miji pamoja na huduma za kijamii.

Ukienda mikoa ya kanda ya ziwa maendeleo yanapimwa kwenye rasilimali mfano Dhahabu na Almasi lakini wanufaika ni makampuni ya nje yanayopata hela nyingi, hicho kipato kinagawanywa kwa idadi ya watu wa huo mkoa wanaonekana wana maendeleo

Ni sawa na Bakhresa ahamie kijiji flani chenye maskini, kitakwimu kijiji kitaonekana watu wake wana vipato vya juu kwasababu pesa za Bakhresa zitachukuliwa ni za kijiji na kugawanywa kwa idadi ya watu.
Inamaana Rukwa maendeleo ya miji ni mkubwa
 
Kanda ya Ziwa ukiitoa Mwanza mikoa iliybaki inatia huruma,

KAGERA
GEITA
MARA
SIMIYU
SHINYANGA
Hata hio MWanza ni Mwanza mjini hapo, usha fika Sengerema huko? Kanda ya ziwa kuna Umasikini wa kutisha nenda huko Mara unaweza liaz fika Musoma Mjini na Vijijini huko kuna Poverty ya kutisha sana.

MWaka juzi nilikuwa huko nilisikitiaka sana,Fika shinyanga huko ndio balaa tupu
 
Back
Top Bottom