Kanda ya Ziwa ukiitoa Mwanza mikoa iliybaki inatia huruma, kuna Poverty kubwa.
KAGERA
GEITA
MARA
SIMIYU
SHINYANGA
Maendeleo ni raia kuweza kumudu life sehemu walipo, huduma za kijamii, miradi ya serikali, n.k. kwa kigezo hiki hata mikoa ya Rukwa na Ruvuma wana nafuu.
Najua kuna watu mtaleta takwimu za kipato cha mtu moja moja za mikoa, hizi takwimu zinaweza kuonesha baadhi ya mikoa ya kanda ya ziwa wapo vizuri lakini hiki sio kipimo kizuri kwasababu hesabu zinazofanyika ni kuchukua mapato yote ya mkoa halafu unagawanywa kwa idadi ya watu wote mpaka watoto wachanga, na ukiangalia mikoa ya kanda ya ziwa kuna rasilimali kama madini lakini wanufaika wakubwa ni makampuni ya nje, hizo pesa zinazopatikana ndizo zinagawanywa na idadi ya watu wote wa mkoa. hiki sio kipimo kizuri.