Kanisa halikupigania kabisa uhuru wa Tanganyika?

Hakuna aliyepigania uhuru wa Tanganyika
Hata Nyerere ni muongo kuwa alipigania uhuru
Muda wa uhuru ulifika na tukapewa uhuru tu
Ngara...
Inaelekea huijui historia ya uhuru wa Tanganyika na historia ya TANU.

Mwaka wa 1950 Gavana Edward Francis Twining alitoa Government Circular No. 5 kuwakumbusha Waafrika wafanyakazi wa serikali kutojihusisha na siasa.

Hii circular ilitolewa baada ya TAA kuonekana kupitia TAA Political Subcommittee iliyokuwa na wajumbe hawa😀r. Vedasto Kyaruzi (President), Abdulwahid Sykes (Secretary), Mufti Sheikh Hassan bin Ameir, Hamza Mwapachu, Sheikh Said Chaurembo, Steven Abdallah Muhando na John Rupia ikijihusisha na siasa za kudai uhuru.

Yako mengi lakini kwa sasa tuanze na kipande hiki.
 
Makanisa yote yalikuwa snitch kwa kuwa walitaka kuendelea kupokea misaada ya wazungu wakati ule hata wao walikuwa bado wagalatia kwelikweli.
Wamechomea sana mipango ya kupigania uhuru, hasa migomo ya wafanya kazi
Na hakukuwa na hata padri wala mchungaji wala kasisi wala askofu kwenye TAA wala TANU
Ila Masheikh kibao wa kumwanga walikuwa wanampelekea moto mkoloni
Halafu mkajitungisha vistori vya kibanga kampiga mkoloni muenekane mlikuwepo
 
Hao matapeli waliokuja kufanikisha ukoloni ndio wakupiganie?
 
Kanisa liltumia "abstractive administrative & technical skills" lakini Waislamu hasa wa maeneo ya Pwani, kwa kuwa walikuwa hawana elimu, wao waliwekwa mstari wa mbele ili kutekeleza mikakati iliyowekwa na wasomi wa Kikristo.

Kwa kifupi Wakristo walikuwa upande wa utawala na menejimenti zaidi, yaani back desk officers, wakati Waislamu walikuwa ni front desk officers. All in all, kwa umoja wao Uhuru wa Tanganyika ukapatikana kwa njia ya bendera na kuepusha umwagaji mkubwa wa damu.
 
Uhuru lilikuwa ni suala la muda na wakati wa uhuru ulifika tukapewa Uhuru bure kutoka Kwa Mwingereza
Sera ya league of nations (UN) ililazimu decolonization
Na ndo maana miaka ya 70/80 hakuna Taifa lilikuwa chini ya mkoloni yeyote
 
Uhuru umeletwa na watanzania regardless of their beliefs hadi kuna wachawi ndani walikua wakiroga wakoloni wanapata mabusha hayo mambo ya dini aachiwe mzee mohamed ndio niche yake hio kugawanya watanzania
 
Uhuru umeletwa na watanzania regardless of their beliefs hadi kuna wachawi ndani walikua wakiroga wakoloni wanapata mabusha hayo mambo ya dini aachiwe mzee mohamed ndio niche yake hio kugawanya watanzania
Ujoka,
Hapana si dini nimechukua Uislam kama "Field of Inquiry," yaani somo la kufanyiwa utafiti.

Si kama nataka kuzungumza kuhusu Uislam kama imani.

Hapa kuna kisa nimekuwekea cha Nyerere anakwenda kwa Ali Mwinyi Tambwe kuuliza hali ya fedha za safari ya UNO.

Mkusanyaji fedha Iddi Faiz Mafungo, Mweka Hazina wa TANU na Al Jamiatul Islammiya.

Ali Mwinyi Tambwe Secretary wa Al Jamiatul Islammiya.

Dhifa ya kumuaga Nyerere safari ya UNO ikafanyika katika jengo la Al Jamiatul Islammiya.

Kwa nini historia iwe hivi?

Hapa ndiyo inafanyika utafiti kutaka kujua.

Kutafiti historia hii na kuandika si dini.

Kwa nini Sheikh Hassan bin Ameir Mufti wa Tanganyika alikuwa akiuza kadi za TANU misikitini?

Swali linakuja kwa nini kadi za TANU hazikuuzwa makanisani?

Huu ni ukweli wa historia na yapo majibu.

Bahati mbaya wengi mnatishika na historia hii.

Nimezungumza kuhusu Dome Okochi Budohi kadi yake ya TANU ni no. 6 huyu ni Mluya kutoka Kenya.

Denis Phombeah kadi yake ya TANU No. 5 na ni kutoka Nyasaland.

Haya mambo yakoje?
Hutaki kujua historia hii?
 
Uhuru lilikuwa ni suala la muda na wakati wa uhuru ulifika tukapewa Uhuru bure kutoka Kwa Mwingereza
Sera ya league of nations (UN) ililazimu decolonization
Na ndo maana miaka ya 70/80 hakuna Taifa lilikuwa chini ya mkoloni yeyote
Ngara...
Jitulize usome historia ya Tanganyika.
 
Izato,
Huijui historia ya Tanganyika.
 
 
Hongera sana mzee wetu Mohamed! Sasa mbona wengine leo wanaumia tukichanga hela kwa ajili ya mkutano wa chadema? Historia ya baadaye itapata mtu wa kutuandika hivi?
 
Kanisa lipi?

Bila shule za Makanisa hao kina Nyerere na Wenzake wangeweza hata kudai huo uhuru?
 
Sera ya league of nations (UN) ililazimu decolonization
Na ndo maana miaka ya 70/80 hakuna Taifa lilikuwa chini ya mkoloni yeyote
Zimbabwe imepata uhuru mwaka 1980.

Namibia imepata uhuru mwaka 1990
 
Kitu kimoja ninachojua, jambo lolote likifanywa na mtu asiye Muislamu nchi hii lilitambuliwa kama Mtanzania kafanya ila likifanywa na upande wa pili, Mzee Mudi atafosisha lionekane amefanya kwasababu ya dini yake.

Niko tayari kukosolewa.
 
Nature inapingana na unachosema. Kati ya kanisa na upande wa pili hata zama hizi nani anategemea misaada?
 
Zimbabwe imepata uhuru mwaka 1980.

Namibia imepata uhuru mwaka 1990
Hiyo haina maana kuwa mtu kilaza kama Nyerere au uislam wangeweza kupigania uhuru,
Ukoloni, utumwa, ujamaa n. K ilifika muda wa kufa na hizi sera zikafa tu
Leo hakuna utumwa, ukoloni wa ujamaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…