Kanisa halikupigania kabisa uhuru wa Tanganyika?

Mohamed Said hivi ilikuwaje hao wazee wako wao wenyewe kabla ya kuja kwa Nyerere kuwa na mtu mwenye sifa kama Nyerere au kumzidi?

Unadhani Makao makuu ya Serikali yangekuwa kwa mfano Mbeya au Kilimanjaro, bado hao wazee wako wangekutana na Mwalimu?
 
Atheists nao pia walikuwa na mchango wao sema ndio hivyo hawapewi airtime tu.
 
Allen...
Swali lako sijalielewa hebu nifafanulie.
 
Kuna watu kama Mohamed Said ambao wana mtizamo kuwa historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika imepotoshwa kwa kuwa mchango wa waislam hauelezewi kwa kina.

Lakini labda ipo pia historia iliyoachwa kuonesha mchango wa kanisa kwenye kupigania uhuru wa Tanganyika. Jee Kanisa halina mchango wowote kwenye kupigania uhuru wa Tanganyika?

Kuna watu ni wa kuwadharau. Hawana agenda nyingine ya maana ila udini.

Udini umewahi kumsaidia nani? Ukitaka kufeli ishi kwa udini udini. Utakwama.

Mwenyezi Mungu fursa zake anawagawia binadamu wote jinsi impendezavyo.

Huyo mzee ni failure.....anatafuta sehemu ya kupata mlo
 
Atheists nao pia walikuwa na mchango wao sema ndio hivyo hawapewi airtime tu.
Scars,
Hapakuwa na Wapagani katika African Association na unaweza kulikuwa hili kwa kuwatazama waasisi wake: Kleist Abdallah Sykes, Mzee bin Sudi, Ibrahim Hamisi, Suleiman Majisu, Zibe Kidasi, Ali Said Mpima hawa Waislamu.

Cecil Matola, Rawson Watts, na Raikes Kusi hawa Wakristo.

Sasa angalia viongozi wa TAA katika TAA Political Subcommittee: Mufti Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Said Chaurembo, Hamza Mwapachu, Abdul Sykes, Dr. Vedasto Kyaruzi, Steven Abdallah Mhando na John Rupia.

Tatizo kubwa hapa JF wengi hamuijui historia ya TANU na kujifunza hamtaki.
 
Kuna watu ni wa kuwadharau. Hawana agenda nyingine ya maana ila udini.

Udini umewahi kumsaidia nani? Ukitaka kufeli ishi kwa udini udini. Utakwama.

Mwenyezi Mungu fursa zake anawagawia binadamu wote jinsi impendezavyo.

Huyo mzee ni failure.....anatafuta sehemu ya kupata mlo
Tangawizi,
Hii ni historia iliyosahihishwa hakuna dini isipokuwa naeleza mchango wa Waislamu katika kupigania uhuru.
 
Mimi nikosema mfano uhuru hatukupigia tulipewa nakuwa nimekosea
 
Scars,
Hapakuwa na Wapagani katika African Association na unaweza kulikuwa hili kwa kuwatazama waasisi wake: Kleist Abdallah Sykes, Mzee bin Sudi, Ibrahim Hamisi, Suleiman Majisu, Zibe Kidasi, Ali Said Mpima hawa Waislamu.

Cecil Matola, Rawson Watts, na Raikes Kusi hawa Wakristo.

Sasa angalia viongozi wa TAA katika TAA Political Subcommittee: Mufti Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Said Chaurembo, Hamza Mwapachu, Abdul Sykes, Dr. Vedasto Kyaruzi, Steven Abdallah Mhando na John Rupia.

Tatizo kubwa hapa JF wengi hamuijui historia ya TANU na kujifunza hamtaki.
Mzee wangu hivi mpaka leo bado unataka tuendelee kujadili swala lile lile ambalo huko nyuma tumekuwa tukikurekebisha tena na tena?

Ni mara ngapi tuseme wapagani sio Atheists?
 
Allen...
Swali lako sijalielewa hebu nifafanulie.
Kwa uelewa wangu (sisemi utafiti) kabla ya Dar es salaam kuwa makao makuu ya nchi, zama za mjerumani, makao makuu yalikuwa Tanga.

Kwa mantiki hiyo Mwalimu hakuja Dar kuwafuata hao wazee wako bali alikuja Dar kwa kuwa yalikuwa ni makao makuu ya nchi.

Na TAA na baadae TANU, vilikuwa vyama vya kuwasaidia waafrika waliokuwa wanaona wapo nje ya mfumo wa kiutawala.

Sasa unadhani kama makao makuu ya nchi yangekuwa Mbeya Mwalimu bado angekuja Dar kuwatafuta hao wazee wako wapange jinsi ya kupata uhuru wa Tanganyika.

Na ninaamini unafanya upotoshaji kuonesha uhuru ulipiganiwa Dar tu tena na waislamu pekee.

Swali langu unalodai hulielewi ni hili. Kabla ya ujio wa Mwalimu, jee hao wazee wako walikuwa na nani waliyekuwa wanaona anafaa kupigania uhuru wa Tanganyika?
 
Mimi nikosema mfano uhuru hatukupigia tulipewa nakuwa nimekosea
Hujakosea... Sisi hatukua koloni la muingereza ila uingereza ilipewa dhamana na UNO (Sasa ni UN) kuisimamia Tanganyika mpaka itakapokuwa tayari kujitawala.
 
Mzee wangu hivi mpaka leo bado unataka tuendelee kujadili swala lile lile ambalo huko nyuma tumekuwa tukikurekebisha tena na tena?

Ni mara ngapi tuseme wapagani sio Atheists?
Scars,
Huo ni uelewewa wako na sikupingi.
 
Nawakumbusha tu kua ukizungumzia kanisa ujue umewazungumzia wakoloni wenyewe na kanisa ndio limetoa huo uhuru kupitia hao wakoloni (wakokoni ndio wamisionar na wamisionar ndio makanisa)
 
Hujakosea... Sisi hatukua koloni la muingereza ila uingereza ilipewa dhamana na UNO (Sasa ni UN) kuisimamia Tanganyika mpaka itakapokuwa tayari kujitawala.
Allen...
Hili nimelijadili kwa kirefu katika kitabu cha Abdul Sykes na nikaeleza njama za Waingereza kukataa kutoka Tanganyika hata pale TAA mwaka wa 1949 walipowaomba wajitayarishe kwa hilo.

Waraka huu wa kuwaomba Waingereza wajitayarishe kuachia madaraka ulitayarishwa na TAA Political Subcommittee na mshauri wa kamati hii alikuwa Earle Seaton.
 
Kwa uelewa wangu (sisemi utafiti) kabla ya Dar es salaam kuwa makao makuu ya nchi, zama za mjerumani, makao makuu yalikuwa Tanga.

Kwa mantiki hiyo Mwalimu hakuja Dar kuwafuata hao wazee wako bali alikuja Dar kwa kuwa yalikuwa ni makao makuu ya nchi.

Na TAA na baadae TANU, vilikuwa vyama vya kuwasaidia waafrika waliokuwa wanaona wapo nje ya mfumo wa kiutawala.

Sasa unadhani kama makao makuu ya nchi yangekuwa Mbeya Mwalimu bado angekuja Dar kuwatafuta hao wazee wako wapange jinsi ya kupata uhuru wa Tanganyika.

Na ninaamini unafanya upotoshaji kuonesha uhuru ulipiganiwa Dar tu tena na waislamu pekee.

Swali langu unalodai hulielewi ni hili. Kabla ya ujio wa Mwalimu, jee hao wazee wako walikuwa na nani waliyekuwa wanaona anafaa kupigania uhuru wa Tanganyika?
Allen...
Nakuomba soma kitabu cha Abdul Sykes majibu yote ya maswali yako yamo mle kuanzia swali la udhamini hadi hili la kiongozi wa kudai uhuru.

Abdul Sykes alimtaka Chief David Kidaha Makwaia aongoze harakati za kudai uhuru.

Hii ilikuwa 1950.
 
Scars,
Huo ni uelewewa wako na sikupingi.
Hapana Mzee wangu, hili sio swala ambalo lipo kwa mujibu wa uelewa wangu.

Ni jambo ambalo lipo universal/global, lipo hivi ulimwengu kote kwa wale wote wanaojua historia basi hili haliwezi kuwasumbua.

Na sikutegemea kama ningekutana na aina hii ya ubishi au ugumu kwenye kulielewa hili swala, kutoka kwa mtu mwenye kalba yako ambaye ni mbobezi kwenye maswala ya historia.

Vitu vidogo kama hivi ukiwa unashindwa kuvitofautisha, kwa watu ambao ni curiousity vinaweza kuwafanya waweke doubts juu ya mambo mengi ambayo umekuwa ukiyafanya kuhusu historia ya nchi hii.
 
Kanisa linamchango katika kuupigania uhuru wa Tanganyika, lakini Msikiti una mchango mkubwa zaidi.
Msikiti na uhuru wapi na wapi..wazanzibari ni kielelezo hadi leo wana chukia watanganyika kisa kupiganiwa uhuru wao na wabara kwa kumuondoa muarabu ...ndiyo maana sasa hivi waarabu ndiyo wenye kupewa uongozi wa juu kule zenji
 
Hapana Mzee wangu, hili sio swala ambalo lipo kwa mujibu wa uelewa wangu.

Ni jambo ambalo lipo universal/global, lipo hivi ulimwengu kote kwa wale wote wanaojua historia basi hili haliwezi kuwasumbua.

Na sikutegemea kama ningekutana na aina hii ya ubishi au ugumu kwenye kulielewa hili swala, kutoka kwa mtu mwenye kalba yako ambaye ni mbobezi kwenye maswala ya historia.

Vitu vidogo kama hivi ukiwa unashindwa kuvitofautisha, kwa watu ambao ni curiousity vinaweza kuwafanya waweke doubts juu ya mambo mengi ambayo umekuwa ukiyafanya kuhusu historia ya nchi hii.
Scars,
Unakusudia Pagani?
Kama ni hili kwangu halina shaka.

Tunazungumza wengi kuamini jambo ndiyo ukweli.

Mmekaa na historia ya uhuru wa Tanganyika na historia ya Nyerere na mlikuwa wengi hadi mimi mtu mmoja nilipokuleteeni historia nyingine.

Na raha yake hamuikubali hadi leo.
 
Back
Top Bottom