Kanisa halikupigania kabisa uhuru wa Tanganyika?

Scars,
Unakusudia Pagani?
Kama ni hili kwangu halina shaka.

Tunazungumza wengi kuamini jambo ndiyo ukweli.

Mmekaa na historia ya uhuru wa Tanganyika na historia ya Nyerere na mlikuwa wengi hadi mimi mtu mmoja nilipokuleteeni historia nyingine.

Na raha yake hamuikubali hadi leo.
Pagani ni dini, unashindwaje kuelewa hili Mzee wangu?
 
Acha Udini wewe
Edward...
Hili si suala la dini na nimeeleza mara nyingi.

Ungeondoa hiyo "wewe," mchango wako ungependeza.

Heshima kitu cha bure.
Hapa ni mahali tunajadiliana si mahali pa kuonyeshana jeuri na kejeli.
 
Kuna watu kama Mohamed Said ambao wana mtizamo kuwa historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika imepotoshwa kwa kuwa mchango wa waislam hauelezewi kwa kina.

Lakini labda ipo pia historia iliyoachwa kuonesha mchango wa kanisa kwenye kupigania uhuru wa Tanganyika. Jee Kanisa halina mchango wowote kwenye kupigania uhuru wa Tanganyika?
Ngoja pachangamke kidogo.
 
Scars,
Usinilazimishe.
Nimekueleza msimamo wangu la hujaridhia basi mimi sina neno tuendelee na mengine.
Msimamo wako unaweza kuwa potofu na busara ni kupokea huu ukosoaji kama sehemu ya kujifunza.
 
Allen...
Ilikuwa mwaka wa 1955 TANU inahangaika kutafuta fedha za kumpeleka rais wake UNO.

Mkusanyaji fedha wa safari hii alikuwa Iddi Faiz Mafungo na ndiye alikuwa mweka hazina
wa TANU na pia Mweka Hazina wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika).

Iddi Faiz Mafungo alihudhuria mkutano wa kwanza wa TANU Ukumbi wa Arnautoglou yeye
na ndugu yake Iddi Tosiri na kadi zao za TANU zilikuwa No. 24 Iddi Faizi na No. 25 Iddi Tosiri.

Hawa walikuwa wanachama na viongozi wa Al Jamiatul Islamiyya.

Hawa ndugu wawili walikuwa wadogo zake Sheikh Mohamed Ramiyya wa Bagomoyo kwao
alikuwa kaka binamu na ndugu hawa wawili ndiyo waliompeleka Nyerere Bagamoyo kwenda kumjulisha kwa Sheikh Ramiyya.

Ilikuwa usiku na mvua kubwa inanyesha.

Mwalimu Nyerere kenda nyumbani kwa Ali Mwinyi Tambwe kuulizia hali ya michango ya safari.

Mwalimu alikuwa kashika mwamvuli.

Ali Mwinyi akamwambia Nyerere kuwa hali ya michango haijawa sawa.

Ali Mwinyi Tambwe alikuwa Secretary wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika alikuwa anakaa kwenye nyumba ya Al Jamiatul Islamiyya na mbele ya nyumba hii ndipo ilipokuwa shule.

Ali Mwinyi alikuwa mtu wa karibu sana na Nyerere.

Ali Mwinyi ndiye alikwenda na Abdul Sykes Nansio, Ukerewe kwenda kupata kauli ya mwisho ya Mwapachu kuhusu kumtia Nyerere katika uongozi wa juu wa TAA katika uchaguzi wa mwaka wa 1953.

Hamza Mwapachu alimwambia Abdul Sykes kuwa yeye bado hajabadili fikra zake.

Nyerere apewe uongozi wa TAA na mwaka unaofuatia 1954 TANU iundwe.

Kisa cha Uchaguzi wa TAA April 1953 uliofanyika Ukumbi wa Arnautoglou baina ya Abdul Sykes na Julius Nyerere ni kisa maarufu.

Safari ya UNO Ilipowiva dhifa ya kumuaga Mwalimu Nyerere ilifanyika katika jengo la Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika.

Hii kwa ufupi sana ndiyo historia ya Mwalimu Nyerere.

View attachment 3639509
Kulia Iddi Faiz Mafungo, Sheikh Mohamed Ramia, Julius Nyerere,
Saadan Abdu Kandoro na Haruna Iddi Taratibu
View attachment 3639525
Aliyevaa koti na kanzu na tarbushi ni Iddi Faiz Mafongo Uwanja wa Ndege safari ya Nyerere UNO 1955

View attachment 3639529
Jengo la Al Jamiatul Islamiyya ilipofanyika dhifa ya kumuaga Mwalimu Nyerere sadari ya kwanza UNO 1955​
Screenshot_20260802_163350_Google.jpg
 
Pagani ni dini, unashindwaje kuelewa hili Mzee wangu?
Scars,
Usinilazimishe.
Nimekueleza msimamo wangu la hujaridhia basi mimi sina neno tuendelee na mengine
Ngoja pachangamke kidogo.
Moise...
Vipi hiyo hapo chini kwa kuchangamsha Barza?:

"Kabla Abdul Sykes hajakutana na Julius Nyerere nyumbani kwake Mtaa wa Stanley na Sikukuu mwaka wa 1952 alikuwa keshakutana na Jomo Kenyatta Nairobi kwenye mkutano wa siri baina ya viongozi wa TAA na KAU mwaka wa 1950."
 
Msimamo wako unaweza kuwa potofu na busara ni kupokea huu ukosoaji kama sehemu ya kujifunza.
Scars,
Huwezi kuniamulia mimi baina ya haki na batil na sababu hivi viko wazi kabisa.
 
Scars,
Usinilazimishe.
Nimekueleza msimamo wangu la hujaridhia basi mimi sina neno tuendelee na mengine

Moise...
Vipi hiyo hapo chini kwa kuchangamsha barza?:

"Kabla Abdul Sykes hajakutana na Julius Nyerere nyumbani kwake Mtaa wa Stanley na Sikukuu mwaka wa 1952 alikuwa keshakutana na Jomo Kenyatta Nairobi kwenye mkutano wa siri baina ya viongozi wa TAA na KAU."
Imekaa uzuri ajabu mkuu wangu!
 
Hiyo haina maana kuwa mtu kilaza kama Nyerere au uislam wangeweza kupigania uhuru,
Ukoloni, utumwa, ujamaa n. K ilifika muda wa kufa na hizi sera zikafa tu
Leo hakuna utumwa, ukoloni wa ujamaa
Nchi ya Zimbabwe na Namibia zilipata Uhuru kwa kupigana vita maana wakoloni hawakutaka kupoteza makoloni yao.
 
Kuna watu kama Mohamed Said ambao wana mtizamo kuwa historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika imepotoshwa kwa kuwa mchango wa waislam hauelezewi kwa kina.

Lakini labda ipo pia historia iliyoachwa kuonesha mchango wa kanisa kwenye kupigania uhuru wa Tanganyika. Jee Kanisa halina mchango wowote kwenye kupigania uhuru wa Tanganyika?
Ukisema kanisa unamaanisha kitu gani, km ni RC hao hata leo wasingependa nchi iwe huru, maaskofu wa RC wana uraia wa Vatican na ni wazalendo zaidi kwa Vatican huku ni vibaraka wa kuchukua rasilimali zetu kuzipeleka Vatican. Wakatoliki hawakutaka kabisa uhuru
 
Kanisa linamchango katika kuupigania uhuru wa Tanganyika, lakini Msikiti una mchango mkubwa zaidi.
Kwasasa tuko pabaya zaidi kuliko wakati wa mapambano ya UHURU.

Misikiti iko upande gani??

Wakati wa Uhuru tunajua mapambano ya Mtemi Mirambo, Kinjekitile Ngwale, Mkwawa, na wengine. Kwa upande wa Pwani mapambano yalikuwa wapi??

Nje ya AA, ma TANU, mapambano ya kina Sykes yalikuwa wapi??
images.jpeg
 
Allen...
Ilikuwa mwaka wa 1955 TANU inahangaika kutafuta fedha za kumpeleka rais wake UNO.

Mkusanyaji fedha wa safari hii alikuwa Iddi Faiz Mafungo na ndiye alikuwa mweka hazina
wa TANU na pia Mweka Hazina wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika).

Iddi Faiz Mafungo alihudhuria mkutano wa kwanza wa TANU Ukumbi wa Arnautoglou yeye
na ndugu yake Iddi Tosiri na kadi zao za TANU zilikuwa No. 24 Iddi Faizi na No. 25 Iddi Tosiri.

Hawa walikuwa wanachama na viongozi wa Al Jamiatul Islamiyya.

Hawa ndugu wawili walikuwa wadogo zake Sheikh Mohamed Ramiyya wa Bagomoyo kwao
alikuwa kaka binamu na ndugu hawa wawili ndiyo waliompeleka Nyerere Bagamoyo kwenda kumjulisha kwa Sheikh Ramiyya.

Ilikuwa usiku na mvua kubwa inanyesha.

Mwalimu Nyerere kenda nyumbani kwa Ali Mwinyi Tambwe kuulizia hali ya michango ya safari.

Mwalimu alikuwa kashika mwamvuli.

Ali Mwinyi akamwambia Nyerere kuwa hali ya michango haijawa sawa.

Ali Mwinyi Tambwe alikuwa Secretary wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika alikuwa anakaa kwenye nyumba ya Al Jamiatul Islamiyya na mbele ya nyumba hii ndipo ilipokuwa shule.

Ali Mwinyi alikuwa mtu wa karibu sana na Nyerere.

Ali Mwinyi ndiye alikwenda na Abdul Sykes Nansio, Ukerewe kwenda kupata kauli ya mwisho ya Mwapachu kuhusu kumtia Nyerere katika uongozi wa juu wa TAA katika uchaguzi wa mwaka wa 1953.

Hamza Mwapachu alimwambia Abdul Sykes kuwa yeye bado hajabadili fikra zake.

Nyerere apewe uongozi wa TAA na mwaka unaofuatia 1954 TANU iundwe.

Kisa cha Uchaguzi wa TAA April 1953 uliofanyika Ukumbi wa Arnautoglou baina ya Abdul Sykes na Julius Nyerere ni kisa maarufu.

Safari ya UNO Ilipowiva dhifa ya kumuaga Mwalimu Nyerere ilifanyika katika jengo la Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika.

Hii kwa ufupi sana ndiyo historia ya Mwalimu Nyerere.

View attachment 3639509
Kulia Iddi Faiz Mafungo, Sheikh Mohamed Ramia, Julius Nyerere,
Saadan Abdu Kandoro na Haruna Iddi Taratibu
View attachment 3639525
Aliyevaa koti na kanzu na tarbushi ni Iddi Faiz Mafongo Uwanja wa Ndege safari ya Nyerere UNO 1955

View attachment 3639529
Jengo la Al Jamiatul Islamiyya ilipofanyika dhifa ya kumuaga Mwalimu Nyerere sadari ya kwanza UNO 1955​
Mapambano ya uhuru wa Tanganyika hayajaanza na AA au TANU.

Heshimuni mchango wa Kinjekitile Ngwale, Mirambo, na wengine.

Kwasasa tuko pabaya sana kama taifa, tunahitaji sauti za MISIKITI kwenye hali hii.

Tumechoka na zee zima kila siku ni stori za UDINI

👇👇👇
images.jpeg
 
Scars,
Huwezi kuniamulia mimi baina ya haki na batil na sababu hivi viko wazi kabisa.
Na lengo sio kukuamulia, mtu mwenye inferior akikosolewa hawezi kuchukulia hiyo kama challenge ya kumuongezea maarifa ambayo hakuyajua, badala yake anaona ni mtu anayejaribu kumuamulia misimamo yake.

Na kwa mantiki hii basi hata hivyo vitabu vyako na hizo makala zako kuhusu hostoria ya uhuru unayodai imepindishwa vinakosa legitimacy kwasababu nasisi tunatakiwa kukuona kwa jicho hilo hilo la mtu anayetaka kutuamulia ipi ni historia ya kweli na ipi sio.
 
Kuwa nina "inferiority complex," huo ni uoni wako hakuna wa kukuingilia.

Na kama ulivyosema mimi sina haki ya kuamua historia ipi ni ya kweli.

Nililofanya mimi nimeandika kile ninachojua kuwa ni kweli.

Anaeshughulishwa na historia hii si mimi bali ni wale wanaojitokeza kunishambulia kwa nini nimeeleza historia nyingine ya uhuru wa Tanganyika?
 
Imeafikiwa hiyoooo!
Tatizo kubwa ni kuwa na hamaki.
Hili lipo huku kwetu.

Katika mihadhara niliyofanya nje ya hapa JF watu wakisikia historia hii
kama nilivyoiandika maswali huwa imekuwaje ikaandikwa historia siyo?

Maswahili huwa katika mwelekeo huo na kutaka kujua fulani alikuwa nani
na upi mchango wake nk. nk.

Hakuna matusi wala kejeli.

1785688330480.png
 
Attachments

  • 1785687214530.png
    1785687214530.png
    1.3 MB · Views: 14
Back
Top Bottom