KERO Kanisa hili linanikera; nifanyeje?

KERO Kanisa hili linanikera; nifanyeje?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Kuna kanisa limejengwa chini ya dirisha langu. Usiku na mchana, linapiga kwaya kwa kutumia mabomba katika ibada zao. Wao hawajali kama watu wanalala au wako macho; wanashikilia ibada yao kuwa mbele.

Mara nyingine, ibada yao huendelea hadi saa 8 usiku huku wakitumia mabomba.

Nifanyeje?
Hao mashetani wadhutaki nemc, kuna sheria ya uchafuzi wa mazingira kwa kelele.
 
Utazoweya tu mpaka utazikariri kwa moyo .Bado hujajua tu kama church ni business.
 
Cha msingi kama na wewe ni mkristo nenda ukasali nao na siku za mkesha nenda ukakeshe ktk maombi utabarikiwa sana, nenda kwa iman sio kwenda kuzuga

hatua zngne ukichukua utapoteza muda na utakuwa unapingana na watu na MUNGU

au fanya jitihada uhame kama nyumba ni yako weka wapangaji wewe kakae kwingne maana kukosa usingizi utazidisha msongo wa mawazo
 
Hao mashetani wadhutaki nemc, kuna sheria ya uchafuzi wa mazingira kwa kelele.
Wala Si kelele,

Majini vichwani mwenu ndio Huwa yanawakaba yakisikia Ibada na maombi.

Mbona ninyi mnafunga maspika juu kabisa, swalaaa, swalaaaa, swalaaa swalaaaa, mbona sie tunpata USINGIZI bila kero?

Kataa majini🙏
 
Cha msingi kama na wewe ni mkristo nenda ukasali nao na siku za mkesha nenda ukakeshe ktk maombi utabarikiwa sana, nenda kwa iman sio kwenda kuzuga

hatua zngne ukichukua utapoteza muda na utakuwa unapingana na watu na MUNGU

au fanya jitihada uhame kama nyumba ni yako weka wapangaji wewe kakae kwingne maana kukosa usingizi utazidisha msongo wa mawazo
Huyo ni Islam mwenye majini, hayapendi kusikia watu wakiomba na kumsifu, huwakaba hatari.
 
Kuna kanisa limejengwa chini ya dirisha langu. Usiku na mchana, linapiga kwaya kwa kutumia mabomba katika ibada zao. Wao hawajali kama watu wanalala au wako macho; wanashikilia ibada yao kuwa mbele.

Mara nyingine, ibada yao huendelea hadi saa 8 usiku huku wakitumia mabomba.

Nifanyeje?

Utanzania ni kuvumiliana tu kama wengine wanavyovumilia adhana kwa siku mara 5...
 
Mara nyingine, ibada yao huendelea hadi saa 8 usiku huku wakitumia mabomba.

Nifanyeje?
Andamana mpaka Ikulu ukiwe umebeba Bango lenye nukuu ya vifungu vya Qur'an vinavyopinga Makelele hata ya azana kwa yale masipika au kutoa mawaidha Msikitini na spika lipo on kiasi kwamba hata wasiohusika na Ibada ya Msikitini wanawasikiliza full mikelele ya kutishana kuhusu Motoni

Ndimi mwandishi wako mtulivu Zero Minus 10
 
Hujuagi kama lile domo la bata la swalaaaaaa pia ni KERO kubwa sana..... ?? Kuwaambia kitanda chako ni kaburi hiyo shuka ni sanda sio uchawi huooo?? Kaa kwa kutulia upigwe pambio kwa jina la YESU wa nazareth
Nonsense.
 
Kuna kanisa limejengwa chini ya dirisha langu. Usiku na mchana, linapiga kwaya kwa kutumia mabomba katika ibada zao. Wao hawajali kama watu wanalala au wako macho; wanashikilia ibada yao kuwa mbele.

Mara nyingine, ibada yao huendelea hadi saa 8 usiku huku wakitumia mabomba.

Nifanyeje?
Nenda Serikali ya mtaani kwako ukawaripoti. Watawachukulia hatua
 
Na walivyokua hawana akili hawafanyi kazi ila utaskia kuna nyimbo yao moja wanaimba " Haloo mbinguni nataka gari, Halloo mbinguni nataka Ist"
Yani gari ya maana kwao ni Ist
Hizi imani zikikulevya zinatengeneza uraibu, kuna dada mmoja ni fundi nguo, mara nyingi analalamika kupoteza wateja na wateja kumjia juu kwa kuchelewesha kazi zao za nguo, muda mwingi yeye yupo kwenye haya makanisa ya mabati akikaa sana ofisini kwake hayazidi masaa mawili na akishaondoka unaweza kumuona tena baada ya wiki au zaidi. Kuna kipindi nilimpa kazi nilijuta, nguo zilikaa kwake zaidi ya wiki mbili. Ukimuuliza jibu nilikuwa kanisani na mchungaji wangu.

Kuna siku nikamwambia jaribu kubalansi mzani wa imani na kazi, unalalamika wateja wanakukimbia na hupati wateja wapya licha ya kuwa unasali sana(kulingana na malalamiko yake) kwa sababu muda mwingi unautumia zaidi huko kanisani kuliko kazini akanijibu kuwa nna ushetani ndani yangu nataka kumtenganisha na Mungu wake hata mchungaji wake alishamwambia watakuja watu wenye maneno kama mimi kumtenganisha na kanisa kwa kigezo cha kufanya kazi na kutafuta pesa ila asikubali. Nikajisemea moyoni wajinga ndio waliwao.
 
Back
Top Bottom