KERO Kanisa hili linanikera; nifanyeje?

KERO Kanisa hili linanikera; nifanyeje?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Kuna kanisa limejengwa chini ya dirisha langu. Usiku na mchana, linapiga kwaya kwa kutumia mabomba katika ibada zao. Wao hawajali kama watu wanalala au wako macho; wanashikilia ibada yao kuwa mbele.

Mara nyingine, ibada yao huendelea hadi saa 8 usiku huku wakitumia mabomba.

Nifanyeje?

HAWANA TOFAUTI NA WALE WANAOKIMBIZA SWALA. ASUBUHI ASUBUHI. NI SHIDA SANA HIZI. DINI ZENU. HAPO HAMIA KARIBU NA MSIKITI UAMSHWE KWA KELELE ZA KUKIMBIZA SWALA MJINI. HILO KANISA KALISHTAKI KWA MWENYEKITI WA MTAA.
 
Wapo lakini ni wa CCM na siyo wa serikali, kwa serikali huanzia mtaa na kitongoji
Ooh! Mie sijui hata, ila naona watu hutambulisbwa na hao wajumbe wa shina kwenye serikali zao za mitaa.. Kuna siku nilikuwa nakipengele kwenda kwa mwenyekiti akanirudisha kwa mjumbe
 
Fanya hivi.... Chukua pembe la Ng'ombe kisha weka damu ndani yake kisha likae siku 6 mpka 7. Tafuta kitambaa chekundu na cheusi lifunge, baada ya hapo saa tisa usiku litupie kwenye hilo kanisa​
 
Huu ndiyo ujinga umejaaa Afrika.Mbona Ibada za Jadi hazina ma horn speakers kuwakera watu?
Fanya Ibada zako na Mungu wako anakusikia hata bila Kelele.Jenga Nyumba za Ibada,weka fensi na weka sound proof:Sauti ziishie ndani.Mbona huko Dini zilikotoka hakuna Makelele?Israel na Uarabuni hakuna kelele.Sasa Afrika Nani kaleta ujinga?Hilo kanisa uliza kama limesajiriwa,uliza kama Ardhi Yao imepangwa kama Eneo la Ibada.
 
Nadhan tatizo ni huu mbanano wa mjini..makanisa hayana nafasi kabisa ukitoka nje ya kanisa tu tayar uko mtaani....ukikuta kanisa lina eneo la kutosha (plot I mean) kama baadhi ya makanisa ya Roman Catholic & KKKT kwanza sauti inakua contained ndani kwa kiasi kikubwa na hata inayotoka inaishia njee tu eneo husika sauti inayofika kwa raia jirani at least inakua na unafuu..
 
Kuna kanisa limejengwa chini ya dirisha langu. Usiku na mchana, linapiga kwaya kwa kutumia mabomba katika ibada zao. Wao hawajali kama watu wanalala au wako macho; wanashikilia ibada yao kuwa mbele.

Mara nyingine, ibada yao huendelea hadi saa 8 usiku huku wakitumia mabomba.

Nifanyeje?
Nenda wizara ya ardhi waje waangalie matumizi ya hicho kiwanja wanachotumia kama si kwa ajili ya nyumba ya ibada itabidi wachague mawili. Kuhama au waache shughuli zenye usumbufu kwa wengine.
 
Nadhan tatizo ni huu mbanano wa mjini..makanisa hayana nafasi kabisa ukitoka nje ya kanisa tu tayar uko mtaani....ukikuta kanisa lina eneo la kutosha (plot I mean) kama baadhi ya makanisa ya Roman Catholic & KKKT kwanza sauti inakua contained ndani kwa kiasi kikubwa na hata inayotoka inaishia njee tu eneo husika sauti inayofika kwa raia jirani at least inakua na unafuu..
Haya yanayoota bila maono ya mbali ndio shida. Kiwanja cha makazi mtu unajenga nyumba ya ibada kwangu mimi ni kukosa maono na hiyo taasisi ni mtu.
 
Back
Top Bottom