KERO Kanisa hili linanikera; nifanyeje?

KERO Kanisa hili linanikera; nifanyeje?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Hizi imani zikikulevya zinatengeneza uraibu, kuna dada mmoja ni fundi nguo, mara nyingi analalamika kupoteza wateja na wateja kumjia juu kwa kuchelewesha kazi zao za nguo, muda mwingi yeye yupo kwenye haya makanisa ya mabati akikaa sana ofisini kwake hayazidi masaa mawili na akishaondoka unaweza kumuona tena baada ya wiki au zaidi. Kuna kipindi nilimpa kazi nilijuta, nguo zilikaa kwake zaidi ya wiki mbili. Ukimuuliza jibu nilikuwa kanisani na mchungaji wangu.

Kuna siku nikamwambia jaribu kubalansi mzani wa imani na kazi, unalalamika wateja wanakukimbia na hupati wateja wapya licha ya kuwa unasali sana(kulingana na malalamiko yake) kwa sababu muda mwingi unautumia zaidi huko kanisani kuliko kazini akanijibu kuwa nna ushetani ndani yangu nataka kumtenganisha na Mungu wake hata mchungaji wake alishamwambia watakuja watu wenye maneno kama mimi kumtenganisha na kanisa kwa kigezo cha kufanya kazi na kutafuta pesa ila asikubali. Nikajisemea moyoni wajinga ndio waliwao.
Ndo walivyo ukimshauri anahisi we una pepo na anaweza hata kukuchukia kabisa
 
Ndo walivyo ukimshauri anahisi we una pepo na anaweza hata kukuchukia kabisa
Inashangaza sana mtu siku nzima anaipotezea kanisani, bora hata iwe ni jpili basi, wiki nzima kila siku kanisani alafu bado atalalamika umasikini. Na huko kanisani wanahitaji hela sio vinginevyo.
 
Kuna kanisa limejengwa chini ya dirisha langu. Usiku na mchana, linapiga kwaya kwa kutumia mabomba katika ibada zao. Wao hawajali kama watu wanalala au wako macho; wanashikilia ibada yao kuwa mbele.

Mara nyingine, ibada yao huendelea hadi saa 8 usiku huku wakitumia mabomba.

Nifanyeje?
Kama umepanga hapo hama na kama kwako, wauzie hlo eneo, baadhi ya makanisa Tz ni mtaji wa kisiasa ndugu.
 
Kuna kanisa limejengwa chini ya dirisha langu. Usiku na mchana, linapiga kwaya kwa kutumia mabomba katika ibada zao. Wao hawajali kama watu wanalala au wako macho; wanashikilia ibada yao kuwa mbele.

Mara nyingine, ibada yao huendelea hadi saa 8 usiku huku wakitumia mabomba.

Nifanyeje?
Na bado
Hadi Yesu arudi
 
mungu wa wakristo ni kiziwi,bila mikelele hasikii abadani
 
Vumilia tu kama unavyovumilia adhana
Mkuu adhana ni dakika 2 kwa 5. Na ni asbhi saa 11 alfajiri Maombi ya walokole ni usiku wa manane hadi masaa 5 kwa 8, mbona haviendani acha chuki mkuu utazeeka kabla ya wakati wako
 
zile kelele za sakumi mbona tunavumilia tuvumiliane tu tufike.mbinguni salama
 
2004 nilipanga nyumba moja sinza mbele kuna bar ndani kelele mpaka asbh nyuma ukumbi wa sherehe balaaa uliza wapangaji mmoja akanza kuweka kwaya mpaka asbh akaja wa dini inginr akanza kuweka mahubiri mpaka asbh nkaona tunapoelekea nawsza uzazi ukawa changamoto nkahamia sehemu nkacha kodi ya miezi miwili.....

Nilipohamiaa gafla kaja jamaa kafungua kanisaa mziki mwanzo mwisho mpaka asbh nkaona hii vita n kuvumliana else utazunguka dar nzima
 
Nunua spika kubwa na wewe fungulia Qurani kila saa,

Tena itaoendeza kukiwa na watu wengi, unaweza quran nonstop volume mpaka mwisho halafu inaondoka

Wanasema dawa ya bishoo ni kuwa bishoo zaidi yake, hii hamna namba

Hata kama wewe ni mkiristo, jaribu utanipa majibu, 1 day (maximum 2)
 
Nimesoma comment zote bado sijapata jibu la namna gani wanatumia mabomba? Mabomba ndio nini?
 
Anzia kwa mjumbe wa shina, nenda serikali ya mtaaa watakupa utaratibu wa kufata kisheria..
Hatuna mjumbe wa shina. Mamlaka ya serikali yanaanzia ama serikali za mitaa kwa mijini na kwa vijijini yanaanzia serikali za vitongoji halafu serkali za vijiji ndo mambo mengine yanaendelea huko juu
 
Back
Top Bottom