Inside10
JF-Expert Member
- May 20, 2011
- 29,909
- 32,414
Kanisa jipya la Anglikana lijulikanalo kama Episcopal Anglican Province Tanzania linatarajiwa kuzinduliwa Septemba 15 jijini Wilaya ya Kongwa jijini Dodoma.
Kuzinduliwa kwa kanisa hilo kunatajwa kuwapa chaguo waumini wote wa Anglikana kuamua waabudu kanisa lipi kati ya hili jipya na lililopo nchini.
Kuanzishwa kwa kanisa hili kunatajwa kurejesha na kusimamia misingi ya Kanisa la Anglikana kama ilivyokuwa miaka 60 kabla kwa mujibu wao.
Akizungumza na wanahabari, Askofu wa kanisa hilo, Elibariki Kutta amesema kuanzishwa kwa jimbo hilo jipya hakumaanishi kuwa kanisa la Anglikana limemeguka, bali inatanua wigo kwa waumini kuamua wasimame na imani ipi.
“Anglikana haijameguka. Ni moja, ila uhuru wa wewe unataka kuwa na mtazamo gani au njia ipi katika maono yako,” amesema Kutta.
Amesema kuanzishwa kwa kanisa hilo haimaanishi kuwa wameondoka Anglikana lakini wanajaribu kusimama katika misingi ya kanisa mama la Kianglikana.