Kanisa jipya la Anglikana laanzishwa Tanzania, Kuzinduliwa Septemba 15

Kanisa jipya la Anglikana laanzishwa Tanzania, Kuzinduliwa Septemba 15

Kanisa jipya la Anglikana lijulikanalo kama Episcopal Anglican Province Tanzania linatarajiwa kuzinduliwa Septemba 15 jijini Wilaya ya Kongwa jijini Dodoma.

Kuzinduliwa kwa kanisa hilo kunatajwa kuwapa chaguo waumini wote wa Anglikana kuamua waabudu kanisa lipi kati ya hili jipya na lililopo nchini.

Kuanzishwa kwa kanisa hili kunatajwa kurejesha na kusimamia misingi ya Kanisa la Anglikana kama ilivyokuwa miaka 60 kabla kwa mujibu wao.

Akizungumza na wanahabari, Askofu wa kanisa hilo, Elibariki Kutta amesema kuanzishwa kwa jimbo hilo jipya hakumaanishi kuwa kanisa la Anglikana limemeguka, bali inatanua wigo kwa waumini kuamua wasimame na imani ipi.

“Anglikana haijameguka. Ni moja, ila uhuru wa wewe unataka kuwa na mtazamo gani au njia ipi katika maono yako,” amesema Kutta.

Amesema kuanzishwa kwa kanisa hilo haimaanishi kuwa wameondoka Anglikana lakini wanajaribu kusimama katika misingi ya kanisa mama la Kianglikana.

Kama vile ni dizaini za NABII Tito tofauti dhehebu tu😄
 
Maana halisi ya Protestant..Protest..
 
Huo mshangazi na hizo nyonyo nje nje ili iweje? Anaionesha hadhira ipi?

-Kaveli-
 
Mbona sasa ndo mgawanyiko huo..wanasema sio mgawanyiko bali mtu achague imani ipi ndani ya dhehebu moja imani tofauti...how
 
..mimi sio Mkatoliki, lakini nadhani kuungama dhambi kwa dhati ni jambo kubwa sana kiimani.

..watu wanakwenda kinyume na mafundisho ya dini tena, na tena, na tena, wakisubiri kuwajibishwa watakapokwenda mbele za MUNGU.
Kisaikolojia...kuungama kunasaidia kupunguza mzigo wa majanga tunayobeba sbb unapata sehem ambayo utayaongea na hayafiki Kwa ndugu jamaa na marafiki wakaanza kukusolola!

Ndio Ile mnaambiwagwa tafuta mtu unayemuamini ongeza naye matatizo Yako, ila Sasa baada ya siku unayasikia mtaa wa Saba.

Bora kwenda Kwa padre yakheee
 
Back
Top Bottom