Kanisa Katoliki halipaswi kufanya mambo ambayo wengine wanaweza kuyafanya vizuri

fazili

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2011
Posts
16,427
Reaction score
22,418
Ni wakati sasa wa Kanisa Katoliki kwenda level nyingine na kuachana na kufanya mambo ambayo kila mtu anaweza kuyafanya vizuri.

Kanisa linapaswa kujikita kutoa special education na sio tena universal education ambayo sasa inatolewa na taasisi nyingi tu nchini.

Kwa kuwa Kanisa lengo lake sio kupata faida ya fedha, basi Kanisa liwekeze kwenye shule na vyuo vikuu maaalumu kwa ajili ya elimu maalumu.

Kanisa lijikite zaidi ku-establish centers of excellence. Huo ndio wito wa Kanisa, kujipambanua na Ulimwengu.
 
Ni wakati sasa wa Kanisa Katoliki kwenda level nyingine na kuachana na kufanya mambo ambayo kila mtu anaweza kuyafanya.m vizuri.

Kanisa linapaswa kujikita kutoa special education na sio tena universal education ambayo sasa inatolewa na taasisi nyingi tu nchini.

Kwa kuwa Kanisa lengo lake sio kupata faida ya fedha, basi Kanisa liwekeze kwenye shule na vyuo vikuu maaalumu kwa ajili ya elimu maalumu.

Kanisa lijijite zaidi ku-establish centers of excellence. Huo ndio wito wa Kanisa, kujipambanua na Ulimwengu.
Kweli ndio maan hatutoi mapepo kwa waliopagawa.
Hatuombei kujazwa roho mtakatifu wala hatuamini kunena kwa lugha.
 
Tatizo la mapepo utaliona zaidi kwa watu wasiomjua vizuri Yesu Kristo na Wokovu wake. Pia ni tatizo la ujinga kwa kiasi flani kikubwa tu.

Roho Mtakatifu haji kwa kuombewa, mtu anapaswa kumkaribisha Roho Mtakatifu na kukubali kuishi na kufanya naye kazi.

Kunena kwa lugha ni kumpokea Roho Mtakatifu na kutenda naye kazi za Kimungu na sio kuropoka na kuongea lugha zisizoeleweka.
 
Katika Biblia, kuna mifano ambapo watu walijazwa Roho Mtakatifu kwa kuombewa, kama vile katika Matendo 8:14-17, ambapo mitume Petro na Yohana waliwaombea Wasamaria ili wapokee Roho Mtakatifu.

Pia katika Matendo 19:6, Paulo alipoweka mikono yake juu ya wanafunzi wa Efeso, walipokea Roho Mtakatifu.

Hata hivyo, kuna pia mifano ya watu waliopokea Roho Mtakatifu bila kuombewa na mtu mwingine, kama vile wanafunzi wa Yesu kwenye Matendo 2:1-4 siku ya Pentekoste.

Kwa hiyo, fazili ingawa mtu anaweza kujazwa Roho Mtakatifu kupitia maombi ya wengine, jambo muhimu ni moyo ulio tayari kumpokea Mungu, toba ya kweli, na imani thabiti. Roho mtakatifu haji tu kwa ubarikio, kipaimara wala komunyo, acha kusomewa neno, soma , elewa.
 
Nimedhani ungeshauri watu wasimweleze padri makosa yao ili mungu mkatoliki awasamehe kumbe umeandika UJINGA.
Kumbe dhambi zao wanamueleza Padri alaf na yeye anazichukua na kuzipeleka wapi sasa, au kwa kuhani mkuu? Hata sielewi jaman,
 
Katika imani ya Kikatoliki, waumini wanatubu dhambi zao kwa padri badala ya moja kwa moja kwa Mungu kwa sababu ya mafundisho yao kuhusu Sakramenti ya Kitubio (Upatanisho). Hii inatokana na mafundisho na Mapokeo ya Kanisa na si MUNGU.

Rumi ya kale ni dola na Serikali hivyo , watu waliambiwa watubu kwa padre na warumi walipata siri nyingi zilizowasaidia kuitawala karibu dunia yote.
 
Katika Biblia, kuna mifano ambapo watu walijazwa Roho Mtakatifu kwa kuombewa, kama vile katika Matendo 8:14-17, ambapo mitume Petro na Yohana waliwaombea Wasamaria ili wapokee Roho Mtakatifu.

Pia katika Matendo 19:6, Paulo alipoweka mikono yake juu ya wanafunzi wa Efeso, walipokea Roho Mtakatifu.

Hata hivyo, kuna pia mifano ya watu waliopokea Roho Mtakatifu bila kuombewa na mtu mwingine, kama vile wanafunzi wa Yesu kwenye Matendo 2:1-4 siku ya Pentekoste.

Kwa hiyo, fazili ingawa mtu anaweza kujazwa Roho Mtakatifu kupitia maombi ya wengine, jambo muhimu ni moyo ulio tayari kumpokea Mungu, toba ya kweli, na imani thabiti. Roho mtakatifu haji tu kwa ubarikio, kipaimara wala komunyo, acha kusomewa neno, soma , elewa.
Kabisa, wokovu lazima mtu autake mwenyewe na hata kuufanyia kazi flani ya kiroho, huwezi kusema Yesu alishamaliza yote halafu unaendelea na dhambi ukategemea wokovu, lazima utende pia. Yesu alisema imani tu bila matendo ni bure. Tunakombolewa kwa neema ndio lakini kuna matendo au kazi tunapaswa kufanya pia tukisaidiwa na neema ya Yesu.
 
Katika imani ya Kikatoliki, waumini wanatubu dhambi zao kwa padri badala ya moja kwa moja kwa Mungu kwa sababu ya mafundisho yao kuhusu Sakramenti ya Kitubio (Upatanisho). Hii inatokana na mafundisho na Mapokeo ya Kanisa na si MUNGU.

Rumi ya kale ni dola na Serikali hivyo , watu waliambiwa watubu kwa padre na warumi walipata siri nyingi zilizowasaidia kuitawala karibu dunia yote.
Sasa hapa ndio napata kuelewa, ndio maana Rumi bado ina nguvu
 
Jisomee Jesuit, utaelewa.
Mwanzilishi wake ni Ignas wa Loyola, Mhispania ambaye alikuwa mwanajeshi. Mwaka 1521 alijeruhiwa vibaya vitani. Alipokaa hospitalini muda mrefu akasikia wito wa Mungu uliobadilisha maisha yake. Kisha kuacha jeshi, akamtolea Bikira Maria upanga wake akawa "Mwanajeshi wa Kiroho". Alifuata kwa juhudi zote maisha ya kiroho na kutunga Mazoezi ya Kiroho ili kuongoza watu wamfuate Yesu Kristo.

Mwaka 1534, Ignas alikusanya vijana sita wakaweka nadhiri za ufukara, useja mtakatifu na utiifu, halafu ile ya kumtii daima Papa.

Kisha kusoma teolojia akapadrishwa. Akakusanya kikundi cha marafiki akiwaongoza kujenga maisha ya kiroho kwa njia ya mazoezi ya pekee. Wote walifuata utaratibu uleule. Kila mwaka walikutana kwa kipindi cha sala, kutafakari na kusoma kilichofuata hatua au mbinu maalumu. Wengi walianza kumfuata na chama chake kikakubaliwa na Papa mwaka 1540.

Shirika la Yesu lilikuwa chombo muhimu sana cha urekebisho wa Kikatoliki kikiwa jumuia ya mapadri iliyoongozwa na "Jenerali" wake akitumia nidhamu ya kijeshi.

Shabaha kuu ilikuwa kutetea Kanisa chini ya Papa.

Kila mwanachama alitakiwa kuwa na elimu ya juu. Hivyo Kanisa Katoliki liliimarika katika teolojia, jambo lililowahi kukazwa zaidi na Waprotestanti.

Mapadri Wajesuiti walifanya hasa kazi ya ualimu wakiunda shule na kufundisha vijana elimu pamoja na upendo kwa Kanisa Katoliki.

Mkazo mwingine ulikuwa kufufua utaratibu wa maungamo. Popote Ulaya Wajesuiti walikuwa washauri hasa wa watawala Wakatoliki. Waliposikiliza ungamo la dhambi zao walipata nafasi nzuri ya kuwapa mawazo na kusababisha hatua za serikali dhidi ya Waprotestanti.

Hivyo kwa athari ya Wajesuiti polepole Uprotestanti ulirudi nyuma katika nchi za Ulaya ambako wakazi wengi walikuwa wameanza kufuata mafundisho ya Martin Luther na Calvin lakini watawala walikuwa bado Wakatoliki.

Papa Fransisko ni wa kwanza kutokea shirika hilo.
 
Ni wakati sasa wa Kanisa Katoliki kwenda level nyingine na kuachana na kufanya mambo ambayo kila mtu anaweza kuyafanya vizuri.

Kanisa linapaswa kujikita kutoa special education na sio tena universal education ambayo sasa inatolewa na taasisi nyingi tu nchini.

Kwa kuwa Kanisa lengo lake sio kupata faida ya fedha, basi Kanisa liwekeze kwenye shule na vyuo vikuu maaalumu kwa ajili ya elimu maalumu.

Kanisa lijikite zaidi ku-establish centers of excellence. Huo ndio wito wa Kanisa, kujipambanua na Ulimwengu.
umeandika ujinga, una umri gani wewe?
 
umeandika ujinga, una umri gani wewe?
Pangua hoja siyo mleta hoja.
Machiz, machawa na mateja nao wanazeeka, umri hauna uhusiano wowte na hoja tamilifu.
Wenye umri wakondio walishauri UDART ijengwe jangwani kwa visingizio kibao.
Wenye elimuna umri ndio waliosema FOLENI DAR ES SALAAM ni kielelezo cha maisha Bora.

# Wajinga mnazeeka.
 
Nimedhani ungeshauri watu wasimweleze padri makosa yao ili mungu mkatoliki awasamehe kumbe umeandika UJINGA.
Wasimweleze Padri ila kwenye mikutano ya hadhara tena mbele ya live TV broadcasting, wauelezee umati wa watu ushuhuda wao wa dhambi walizotenda!
 
Back
Top Bottom