Kanisa Katoliki Jimbo la Bukoba limemsimamisha Padre Rwegoshora kufuatia tuhuma za kuhusika mauaji ya Asimwe Novath

Padre kufikia hatua hiyo ina maana kuna shida kwenye udahili wa hawa viongozi wa KANISA, watu wanaingia upadre bila wito bali shida za familia zao ndio zinawapeleka kanisani kwa imani ya maisha mazuri.
Watu hubadilika, na ni binadamu si malaika. Kufikia daraja la upadre ni safari ndefu ya kimasomo na malezi, wengi huanza wakiwa vijana kabisa, ila kila mtu na hulka yake.
 
Hii ng'ombe nyingine inataka kuleta utetezi kwamba huyo padri wenu hakua sawa kiakiri. Huyo anaonekana ni mzoefu wa hayo mambo na yeye ndiye sponsor wa zoez la mauaji.
1. Fr hapa ametajwa kama mtuhumiwa wa kushiriki mauaji. 2. Hakuna muuaji bado aliyetajwa. 3. Polisi watakusanya ushahidi na kama utakuwa na uzito 4. watuhumiwa watakuwa na kesi ya kujibu. 5. Kutafuta utetezi kwa jinsi gani wao si wahusika. 6. Mahakama itapima ni ushahidi wa upande gani na ni wa nani unamtia hatiani. 7. Itatoa hukumu na adhabu. 8. Atakaye ona hajaridhika atakata rufaa. 9. Hivyo, kutoa hukumu kwa sasa na kuwaona watuhumiwa kama wenye hatia ni kuonyesha tu hatujui Katiba, sheria ya kanuni ya adhabu na ya mwendo wa makosa ya jinai zinasemaje. 10. Na mbaya zaidi katika mambo haya tunakimbilia kunyoosheana vidole kutokana na chuki za kiimani tunazo'entertain'. Bure kabisa!
 
Mahakamani ni mfumo tu ambao tunaufata ila ukiangalia katika uhalisia wa jambo watu wamekutwa na viungo vya mtoto bado unasubiri had mahakama iamua ndo ujiridhishe kua wao ndio waliohusika.
 
Hii ng'ombe nyingine inataka kuleta utetezi kwamba huyo padri wenu hakua sawa kiakiri. Huyo anaonekana ni mzoefu wa hayo mambo na yeye ndiye spons

Mahakamani ni mfumo tu ambao tunaufata ila ukiangalia katika uhalisia wa jambo watu wamekutwa na viungo vya mtoto bado unasubiri had mahakama iamua ndo ujiridhishe kua wao ndio waliohusika.
Kwa hiyo, unadhani nikikufikiria kwamba wewe ni mnyang'anyi, unakuwa mnyang'anyi kweli kwa vile "mahakama ni mfumo..." tu? Watu wangapi huwa inasemekana wamekutwa na mali ya wizi, lakini kwenye kutoa ushahidi unakuta hakuna kitu kama hicho na ndiyo maana inatakiwa kwenye tuhuma tujiridhishe kwanza ndipo tuhukumu? Lazima tuzoeze akili zetu kuchambua na kutofautisha vitu na ndiyo maana pia polisi wanapomaliza upelelezi kuna chombo kingine ambacho kipo kwa ajili ya kutoa haki: ama kwa kukubaliana na upelelezi ulivyokwenda au kwa kutofautiana nao na inabidi kusiwe na vipengele vinavyoleta mashtaka kwenye ushahidi unaotolewa. Sasa wewe kujua X au Y kahusika au hahusiki huwa huna njia ya kutumia, i.e. huwa hutumii akili kutofautisha vitu, unaamini tu kwamba tuhuma ni kweli kama Mimi ninavyoweza kudhani kwamba wewe ni mwizi?
 
Kwahiyo wakatoliki ndio wamemtuma akafanye biashara ya viungo vya binadamu? sio kila mtu ana akili lakini. Hata wewe jichunguze vizuri 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣
Mbona uwa mnasema waislam ni MAGAIDI. Na wewe jichunguze kama unaakili au umejaza matope.
 
Izi Dini mbona kama zinaelekea kuonekana kama ni za kimichongo sana....Miaka si mingi ukweli utajulikana
 
Mkuu hizi dini tulizoletewa zina mengi ndani yake,halafu waliotuletea hizi vizazi vya sasa na vijavyo si vya wafia dini kama sisi tulioletewa
 
Jamaa fala sana kama kweli kahusika. Kiongozi wa dini akianguka anaanguka na mamia.

Imagine wale waliokua wanamuamini leo wanasikia ivi. Aaggh.
 
Aisee Dunia inakokwenda sio kabisa hawa watu wamepata mafundisho miaka nenda rudi wao ndio wanafikia kufanya ukatili ambao hata wasiopata hizo Elimu zao za dini hawawezi kufanya...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…